Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Mkuu Kimbunga kuna vitu tunakosea, kwanini tuamini maneno ya Zitto ni kweli kwa kiasi hiki? Kwanza wakati anaandika hiyo barua ya ndani ya Chama, ana uhakika gani au anawezaje kututhibitishia kuwa hakuna mtu wake wa karibu akiwemo huyo Msaki aliyejua kuwa anaandika/ameandika barua yenye maudhui hayo na kisha kufanya timing ya vikao vya chama kuandika kama hicho na kukipost? Sasa katika mazingira hayo yeye Zitto sio Kirusi?

Yani Zitto kuja na kupiga porojo hapa jukwaani ndio wenye akili tunaamini sana maneno yake bila kutafakari? Si ni Zitto huyo huyo aliyekuja hapa jukwaani kuyathibitisha yaliyokuwa yakiongelewa na kina Juliana Shonza kuwa anataka kuuawa? Si ndio huyo nimechukua maneno yake nikayabandika kwenye signature yangu? Lakini si nfdio Zitto huyu huyu aliyekurupushwa juzi juzi hapa na kuandika ati hakuna kiongozi wa chama anayetaka kumuua? Kimbunga, NASISITIZA Zitto ANACHEZA NGOMA YA CCM kwa akilisana, kwa kujua ama kwa kutokujua...

CC Pasco, Ben Saanane, majebere

Mkuu nadhani kwa hilo ni watu wengi hawakumuelewa Zitto hasa ukiunganisha ni yale yaliyoandikwa wakati ule baada ya Zitto kusema kwamba ansikia kuna mambo ya kuuana. Sioni pahala ambapo Zitto alisema kwamba kuna kiongozi anataka kumuua ila sisi tuliyachukua maneno ya akina shonza na kuamini hivyo. maneno hayo yakaja yakaandikwa kwenye gazeti Zitto akakanusha. Nadhani hapa Zitto alitenda haki kwake binafsi na kwa chama. Ingekuwa jambo la kushangaza mwanasiasa kama Zitto akurupuke na kukubaliana na gazeti kwamba kuna kiongozi wa CHADEMA anataka kumuua. Hapa Zitto angekuwa mwansiasa uchwara na ndio ungekuwa mwisho wake. Alilijua hilo ndio maana akakanusha kwa kuwa anazijua siasa za nchi na za CHADEMA. Nadhani anajengewa zengwe ili ajichanganye wamlipue.
 
Zitto kama kweli ni mwanasiasa safi na anajua yupo kwenye chama sahihi alipaswa kumkemea Juliana na kundi lake palepale Shonza alipotoa tuhuma hapa jukwaani. Alinyamaza,akaacha akina Pasco wanapata ujira wao wa chee kutoka kwa wanaowatumikia, ilhali Shonza na Mwampamba na yule wa Kibaha wakimtaja Slaa bila kumung'unya maneno. Zitto alipokuja aliyathibitisha hayo ya kina Shonza bila kuondoa jina la Slaa. Alikuwa na uwezo wa kusema anawindwa auwawe lakini sio na viongozi wa Chama chake, lakini hakufanya hivyo. Maana yake ni nini? Ni kwamba aliyathibitisha ya kina Shonza, na ndio maana mjadala ule ulipopamba moto ilikuwa ni vigumu kumtenganisha Zitto na kina Shonza. Hata wewe unafahamu kuwa hadi leo hii imekuwa ngumu sana kumtofautisha zitto na kina Shonza.
Hakuna cha tofauti kati ya kile walichodai kina shonza ambacho Zitto alikithibitisha na kile kilichoandikwa kwenye Mtanzania, cha kushangaza, kila cha hapa jukwaani alikithibitisha(bila kumtaja Slaa) lakini kile cha Mtanzania alikikanusha. Ni unafiq first class alionao Zitto katika siku zake zote za siasa.

Na hili anataka kulazimisha kuwa barua hiyo haikuwekwa mtandaoni na watu wa karibu yake....what a shame to this politician?!!
 
Last edited by a moderator:
Mods mnaweza weka ile barua ya mtandaoni kwenye hii thread????? mana ilio kwa katibu mkuu ina signature. hii ya hapa haina. kwa nini nisiamini kabisa ile ya katibu mkuu haijavuja ila yake ndo imevuja? then alimtumia kwa njia gani? fax, attachment? mkono? alimpa rafiki?

Wajifanya hauwelewi au unataka kuwarudisha darasa la saba la kwanza.
 
..Ben...kama ambavyo nimemsihi Zitto akutafte mumalize tofauti zenu kwa maslahi ya CDM....pia nakushauri wewe umtafute Zitto..kwa uzuri tu...muyamalize yale mnayotofautiana. Hamna asiyejua kuwa wewe na Mh.Zitto hamna mahusiano mazuri...hili liko wazi..na ndio maana watu humu wanakuhusisha na hujuma dhidi ya Zitto...haswa pale wanaporejea issue ya masalia..

..Ningekua na uwezo ningemwomba mzee Mtei achukue muda wake (siku hizi simwoni humu JF)awakutanishe nyie vijana (haswa wewe na Zitto)ili awapatanishe....kwa manufaa ya chama chenu....maana uhusiano wenu ni muhimu kwa kujenga chama..

Mimi najiuliza sana..hivi nyie vijana chadema haiwaumi kuona mnahusishwa na kukihujumu chama chenu (hata kama mnatumiwa)!!!...mbona hamjifunzi nidhamu kwa chama chenu (na viongozi wenu)...kama wanavyofanya vijana wa ccm mfano kina January..au Nape ..Malisa hata Mwigulu....n.k..lini umeona hawa vijana wanatoka kwenye mitandao ya kijamii wanawatuhumu (tena kwa majina)viongozi wao chamani????..pamoja na kwamba chama chao ccm kimejaa uchafu (mfano mifisadi)...hawafanyi hivi kwa vile wanajua kuna taratibu za chama walizorithi za ku deal na issues (japo hazifuatwi)....wewe...na masalia (waliotemwa)mnakuja humu JF mnatoa lawama kwa viongozi wenu (tena za fitna) kama vile hamna taratibu za chama!!...alafu mnataka kesho tuwakabidhi nchi muikomboe!!kweli!....ona yale makina Shonza na Mwampamba.....yamekua kama condom sasa...yanatumika kama taka...kwa kuwa hayajitambui.....tena hata huko ccm wanadharaulika sana (kama wangejua!)....

....Labda nikupe angalizo kuhusu kiongozi wako Zitto....kwa kukusaidia (ili umuheshimu)...Zitto amefanya vitu tangible nchi hii..na anaheshimika kwa hilo..na wala si ukaribu wake kwa Dr.Slaa au Mh.Mbowe....hili lazima ulijue...rejea mifano chini
ungemshauri mtei amuite amuonye Ben Saa8 na sio kumkutanisha na zitto itakuwa kumshushia hadhi mh Zitto.
By the way unapaswa kujua kuwa Ben saa8 yuko nyuma ya mtu flani.
 
Umaarufu kazi maana kubaki kwenye midomo ya watu lazima ufanye matukio ili uendelee kuwa maarufu
 
Wanajamvi,binafsi sioni mantiki ya kumshambulia Ben Saanane kuhusu issue ya barua ya Zitto, najiuliza maswali kwa nn watu wanamhisi Ben Saanane? Inawezekana ni kwa sababu ya kilichotokea hapo nyuma na labda kwa sababu ya maneno ya akina Shonza! Zitto amesema kuna kirusi lakini hakutaja jina, na mbaya zaidi hata wanaomhisi Ben Saanane hawatoi sababu ya hisia zao! Lets be fair

Huyu ni nyoka hawezi kuaminika hata kidogo. Yeye ndo alieanzisha kikundi cha Pm7 iweje aje kuwa hero? Kwanini yeye huwa anamshambulia zitto? Hawezi kuwa mwema hata kidogo na hata anaemtumia anamjua kuwa huyu ni kinyonga.
 
Hongera sana Zitto bila ya busara na hekima zako chadema kwishney.
Viongozi wengi wa cdm siasa wameivamitu, zzk siasa ni kipaji mungu amekujalia ndio maana matokeo ya fitna zao ni hatua za kukupeleka ikulu.

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
Last edited by a moderator:
Sasa kaka we unachafuliwa kwa nani anaekujua wewe?au unataka kutuaminisha kuwa wewe ni maarufu kiasi hicho zaidi Jf?
Fikiria kazi ya kufanya au fuata ushauri uliopewa wa kugombea nafasi ya uongozi ndani ya chama au jimboni ili uwatumikie wananchi kama zitto kidogo utatuaminisha kuwa wewe ni mtu muhimu na maarufu kuliko kutumika kama nanii.

Mpe kweli huyo! Atafute kazi afanye aache kutumiwa, kadri anavyo leta porojo ndivyo watu wanamuona yeye ndio kirusi.

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
Huyu ni nyoka hawezi kuaminika hata kidogo. Yeye ndo alieanzisha kikundi cha Pm7 iweje aje kuwa hero? Kwanini yeye huwa anamshambulia zitto? Hawezi kuwa mwema hata kidogo na hata anaemtumia anamjua kuwa huyu ni kinyonga.
Acha kujisahau wewe kama anajua ni kinyonga atamtumiaje?DR.PAULIN NJOO WAGONJWA NI WENGI
 
Acha kujisahau wewe kama anajua ni kinyonga atamtumiaje?DR.PAULIN NJOO WAGONJWA NI WENGI

Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.
 
Zitto katoa wazo na kuomba hicho kirusi kitafutwe. Ni uhakika kwamba hicho kirusi kikitafutwa kinapatikana, iwe kirusi ni Zitto au ni mtu mwingine ila ni kirusi.

Kama Zitto angehusika kuvujisha hii barua asingepata hii confidence ya kuomba aliyevujisha barua atafutwe, unless amesha mframe mtu (which is possible vile vile).

Ninachokiona ni kwamba hiki kirusi kinajulikana, viongozi wakuu wenye mamlaka ya kuamua kitafutwe au kisitafutwe wanakijua na hawataki kijulikane.

Kwa nini Chadema hawataki hiki kirusi kitafutwe?
 
Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.
Sasa ndio umeandika nini hapo? DR.PAULIN NJOO HUKU
 
Target ya maadui amesharuka kihunzi. god is so good. anasema kwaajili ya Israel sitatulia wala sita sinzia mpaka niwaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. CDM is far from any touch of the enemy na wale wote waliosimama kuitetea iideology yake hakuna ambaye ataguswa na mtu yeyote....endeleeni kupoteza muda wenu!
 
Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.

Fundo la muwa asilia
 
wanasubiri upepo uende vipi lol

sasa kama Zitto hana uhakika na ukweli wa video ya Rwakatare
hadi aombe uchunguzi
why tena aseme haamini kuna watu wanataka muua?
what if uchunguzi ukisema video ni kweli?

Boss, huyu kijana kuna kitu kimoja ambacho simuelewi katika utendaji wake kichama; yeye ni deputy katibu mkuu wa Chadema na kwa nafasi hiyo anatakiwa ahudhulie vikao vyote muhimu vya chama, na kama nihivyo huko kwenye hivyo vikao ndio angekuwa anashauri mambo ambayo anadhani chama kifanye ili kujiimalisha. Sasa yeye badala ya kuzungumza hayo maoni yake kwenye mikutano ya ndani ya chama anaona ni busara kuandika barua kwa katibu mkuu wake ili iweje? Anaandika barua hizo kwa madhumuni gani badala ya kuzungumza kwenye vikao? Hata enzi ya TANU wakoloni waliwatumia watu kukivuruga chama from within nao waliitwa MALIPYOTO na wengine kama Zuberi Mtemvu wakaondoka na kuanzisha African Congress ili kuyumbisha dhamira sahihi ya kudai UHURU lakini mwisho wa yote hawakufanikiwa.
 
Yeah ther must be a mole very close to the leadership. Willy Brandt had mole as his personal secretary so was the butler to Benedict and the famous Judas. The party has to screen the transfer more carefully rather than rejoicing their exit from CCM. The is becoming rough and will ever be towards 2015, this is the time to show unity from both members and leaders at all level. Anybody can steer a ship in calm seas!!
 
Boss, huyu kijana kuna kitu kimoja ambacho simuelewi katika utendaji wake kichama; yeye ni deputy katibu mkuu wa Chadema na kwa nafasi hiyo anatakiwa ahudhulie vikao vyote muhimu vya chama, na kama nihivyo huko kwenye hivyo vikao ndio angekuwa anashauri mambo ambayo anadhani chama kifanye ili kujiimalisha. Sasa yeye badala ya kuzungumza hayo maoni yake kwenye mikutano ya ndani ya chama anaona ni busara kuandika barua kwa katibu mkuu wake ili iweje? Anaandika barua hizo kwa madhumuni gani badala ya kuzungumza kwenye vikao? Hata enzi ya TANU wakoloni waliwatumia watu kukivuruga chama from within nao waliitwa MALIPYOTO na wengine kama Zuberi Mtemvu wakaondoka na kuanzisha African Congress ili kuyumbisha dhamira sahihi ya kudai UHURU lakini mwisho wa yote hawakufanikiwa.
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni . Hilo ni swali najiuliza kila mara iweje Zitto aandike barua kwenye secretariat ambayo yeye ni kiongozi wa juu kwenye hiyo secretariat ! Huyu anaafanya hivi kutafuta support/umaarufu nje ya vikao halali vya chama bila kujua adhari zake kwa yy binafsi na chama kwa ujumla.
 
Zitto is a controversial politician! Fuatilia michango inayomhusu huku jamvini; lakini pia hata nje ya JF.

Namkumbuka Ben Saanane wakati akitumia jina la Ben; na maneno yake "Little boy among men". Misimamo yake ni crystal clear.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom