Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.

Mkuu nadhani kwa hilo ni watu wengi hawakumuelewa Zitto hasa ukiunganisha ni yale yaliyoandikwa wakati ule baada ya Zitto kusema kwamba ansikia kuna mambo ya kuuana. Sioni pahala ambapo Zitto alisema kwamba kuna kiongozi anataka kumuua ila sisi tuliyachukua maneno ya akina shonza na kuamini hivyo. maneno hayo yakaja yakaandikwa kwenye gazeti Zitto akakanusha. Nadhani hapa Zitto alitenda haki kwake binafsi na kwa chama. Ingekuwa jambo la kushangaza mwanasiasa kama Zitto akurupuke na kukubaliana na gazeti kwamba kuna kiongozi wa CHADEMA anataka kumuua. Hapa Zitto angekuwa mwansiasa uchwara na ndio ungekuwa mwisho wake. Alilijua hilo ndio maana akakanusha kwa kuwa anazijua siasa za nchi na za CHADEMA. Nadhani anajengewa zengwe ili ajichanganye wamlipue.
 

Zitto kama kweli ni mwanasiasa safi na anajua yupo kwenye chama sahihi alipaswa kumkemea Juliana na kundi lake palepale Shonza alipotoa tuhuma hapa jukwaani. Alinyamaza,akaacha akina Pasco wanapata ujira wao wa chee kutoka kwa wanaowatumikia, ilhali Shonza na Mwampamba na yule wa Kibaha wakimtaja Slaa bila kumung'unya maneno. Zitto alipokuja aliyathibitisha hayo ya kina Shonza bila kuondoa jina la Slaa. Alikuwa na uwezo wa kusema anawindwa auwawe lakini sio na viongozi wa Chama chake, lakini hakufanya hivyo. Maana yake ni nini? Ni kwamba aliyathibitisha ya kina Shonza, na ndio maana mjadala ule ulipopamba moto ilikuwa ni vigumu kumtenganisha Zitto na kina Shonza. Hata wewe unafahamu kuwa hadi leo hii imekuwa ngumu sana kumtofautisha zitto na kina Shonza.
Hakuna cha tofauti kati ya kile walichodai kina shonza ambacho Zitto alikithibitisha na kile kilichoandikwa kwenye Mtanzania, cha kushangaza, kila cha hapa jukwaani alikithibitisha(bila kumtaja Slaa) lakini kile cha Mtanzania alikikanusha. Ni unafiq first class alionao Zitto katika siku zake zote za siasa.

Na hili anataka kulazimisha kuwa barua hiyo haikuwekwa mtandaoni na watu wa karibu yake....what a shame to this politician?!!
 
Last edited by a moderator:

Wajifanya hauwelewi au unataka kuwarudisha darasa la saba la kwanza.
 
 
Umaarufu kazi maana kubaki kwenye midomo ya watu lazima ufanye matukio ili uendelee kuwa maarufu
 

Huyu ni nyoka hawezi kuaminika hata kidogo. Yeye ndo alieanzisha kikundi cha Pm7 iweje aje kuwa hero? Kwanini yeye huwa anamshambulia zitto? Hawezi kuwa mwema hata kidogo na hata anaemtumia anamjua kuwa huyu ni kinyonga.
 
Hongera sana Zitto bila ya busara na hekima zako chadema kwishney.
Viongozi wengi wa cdm siasa wameivamitu, zzk siasa ni kipaji mungu amekujalia ndio maana matokeo ya fitna zao ni hatua za kukupeleka ikulu.

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
Last edited by a moderator:

Mpe kweli huyo! Atafute kazi afanye aache kutumiwa, kadri anavyo leta porojo ndivyo watu wanamuona yeye ndio kirusi.

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
Huyu ni nyoka hawezi kuaminika hata kidogo. Yeye ndo alieanzisha kikundi cha Pm7 iweje aje kuwa hero? Kwanini yeye huwa anamshambulia zitto? Hawezi kuwa mwema hata kidogo na hata anaemtumia anamjua kuwa huyu ni kinyonga.
Acha kujisahau wewe kama anajua ni kinyonga atamtumiaje?DR.PAULIN NJOO WAGONJWA NI WENGI
 
Acha kujisahau wewe kama anajua ni kinyonga atamtumiaje?DR.PAULIN NJOO WAGONJWA NI WENGI

Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.
 
Zitto katoa wazo na kuomba hicho kirusi kitafutwe. Ni uhakika kwamba hicho kirusi kikitafutwa kinapatikana, iwe kirusi ni Zitto au ni mtu mwingine ila ni kirusi.

Kama Zitto angehusika kuvujisha hii barua asingepata hii confidence ya kuomba aliyevujisha barua atafutwe, unless amesha mframe mtu (which is possible vile vile).

Ninachokiona ni kwamba hiki kirusi kinajulikana, viongozi wakuu wenye mamlaka ya kuamua kitafutwe au kisitafutwe wanakijua na hawataki kijulikane.

Kwa nini Chadema hawataki hiki kirusi kitafutwe?
 
Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.
Sasa ndio umeandika nini hapo? DR.PAULIN NJOO HUKU
 
Target ya maadui amesharuka kihunzi. god is so good. anasema kwaajili ya Israel sitatulia wala sita sinzia mpaka niwaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. CDM is far from any touch of the enemy na wale wote waliosimama kuitetea iideology yake hakuna ambaye ataguswa na mtu yeyote....endeleeni kupoteza muda wenu!
 
Jiulize kamtumiaje Ludo na leo kamkana hadharani.
Jiulize kwanini amemtumia Rwakatale na sasa anajiandaa kumkana eti katumiwa na ccm.
Jiulize aliwezaje kumtumia Mke wake halisi na baadae kumkana na kumchukua Josephiner.
Chezea slaa wewe.
Cc Ben saa8.

Fundo la muwa asilia
 
wanasubiri upepo uende vipi lol

sasa kama Zitto hana uhakika na ukweli wa video ya Rwakatare
hadi aombe uchunguzi
why tena aseme haamini kuna watu wanataka muua?
what if uchunguzi ukisema video ni kweli?

Boss, huyu kijana kuna kitu kimoja ambacho simuelewi katika utendaji wake kichama; yeye ni deputy katibu mkuu wa Chadema na kwa nafasi hiyo anatakiwa ahudhulie vikao vyote muhimu vya chama, na kama nihivyo huko kwenye hivyo vikao ndio angekuwa anashauri mambo ambayo anadhani chama kifanye ili kujiimalisha. Sasa yeye badala ya kuzungumza hayo maoni yake kwenye mikutano ya ndani ya chama anaona ni busara kuandika barua kwa katibu mkuu wake ili iweje? Anaandika barua hizo kwa madhumuni gani badala ya kuzungumza kwenye vikao? Hata enzi ya TANU wakoloni waliwatumia watu kukivuruga chama from within nao waliitwa MALIPYOTO na wengine kama Zuberi Mtemvu wakaondoka na kuanzisha African Congress ili kuyumbisha dhamira sahihi ya kudai UHURU lakini mwisho wa yote hawakufanikiwa.
 
Yeah ther must be a mole very close to the leadership. Willy Brandt had mole as his personal secretary so was the butler to Benedict and the famous Judas. The party has to screen the transfer more carefully rather than rejoicing their exit from CCM. The is becoming rough and will ever be towards 2015, this is the time to show unity from both members and leaders at all level. Anybody can steer a ship in calm seas!!
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni . Hilo ni swali najiuliza kila mara iweje Zitto aandike barua kwenye secretariat ambayo yeye ni kiongozi wa juu kwenye hiyo secretariat ! Huyu anaafanya hivi kutafuta support/umaarufu nje ya vikao halali vya chama bila kujua adhari zake kwa yy binafsi na chama kwa ujumla.
 
Zitto is a controversial politician! Fuatilia michango inayomhusu huku jamvini; lakini pia hata nje ya JF.

Namkumbuka Ben Saanane wakati akitumia jina la Ben; na maneno yake "Little boy among men". Misimamo yake ni crystal clear.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…