y
Mohamedi Mtoi 
Wakuu.
Nimekutana na huu Mchango wa wakili Nyaronyo Kicheere ambaye pia ni mwanasheria wa Wilfred Lwekatare nikaona si vibaya nikawashirikisha kuusoma. Umeanza hivi...
Bandugu,
kwanza nikiri kwamba
namheshimu sana bwana zito zuberi kabwe, lakini kwa bahati mbaya sana siyaamini maneno aliyoyaandika humu jamvini
kuwa ndio ufafanuzi wake
kuhusiana na barua yake
inayoitaka chadema
kumsimamisha uongozi na
kumchunguza mkurugenzi wao wa ulinzi na usalama, mhaya mkuu wa ibwera, kagera- Bukoba - wilfred lwakatare.
Bandugu,
katika maelezo yake, zzk
anadai eti kuna kirusi katika
ngazi za juu za uongozi wa
chadema kinacho kihujumu
chama hicho kikuu cha
upinzani nchini! eti, kwa
mujibu wa zzk, kirusi hicho
ndicho id yake ilitumika
kuapulodi video inayomwonyesha lwakatare
akipanga ugaidi na kwamba Id hiyo hiyo kwa mujibu wa
uchunguzi wa zito zuberi
kabwe ndiyo iliyotumika
kuapulodi barua yake zito
kwenye mtandao!!!!!!!!!!
Bandugu,
hapa sizungumzii umuhimu au kutokuwa muhimu kwa
msimamo na barua hiyo ya
Zito bali nasema kama maneno ya zito ni ya kweli basi kirusi hicho ni zito zuberi kabwe mwenyewe.
kwa nini nasema
hivi????
nasema hivi kwa sababu nimeambiwa na
wanoko waliopo chadema
kuwa barua ya zito ni hard
copy maana ya maneno haya ni kwamba barua hiyo
imeandikwa kwenye karatasi
na kutiwa sahihi na zito
mwenyewe lakini barua iliyo
kwenye mtandao ni soft copy yaani ilitumwa kwa mtandao na walioiona wanadai kuwa haina sahihi ya zzk.
Bandugu,
ajabu ilioje ya mwenyezi
mungu subhana wa taala
mwenye kutoa neema kubwa kubwa na neema ndogondogo kwamba kwenye barua ya sasa
iliyoapolodiwa na kirusi
kilichopo ndani ya chadema
haina sahihi ya zito kuonesha kuwa imeskaniwa na kirusi ndani ya chadema???? barua ya
mtandaoni ingekuwa na sahihi hiyo ikaonekana tungekubali na kuamini kuwa kweli kuna
kirusi katika ngazi za juu za
chadema kinachovujisha siri za chama na kuswekwa
mtandaoni.
Swali: hii barua
isiyo na sahihi imetoka wapi na nani mwenye kujua siri ya barua ya zito aliyeivujisha bila kwanza kuhakikisha ina sahihi na kufanana na ile iliyopelekwa chadema???????? na mwenye tabia ya kusweka mtandaoni na kuvujisha vijambozi vingi tu
vya chama ni nani zaidi ya
zito????????
Bandugu,
mimi nyaronyo mwita
kicheere nikizingatia kwa
makini taarifa hizi za kinoko
kutoka ndani kabisa chamani nadhani ninayo haki ya kudhani kwamba barua hii imeapolodiwa na zito na kwamba id hiyo ya siri iliyotumika kuweka video ya kigaidi na barua ya siri mtandaoni ni id ya zito
mwenyewe.
Someni vizuri maelezo yangu haya halafu
mniambie kama ninalo kosa
lolote kwa kudhani na kuamini kuwa zito ndiye kirusi mwenyewe kwa barua na video ya kigaidi.
Kicheere, tungi, kigamboni,
tanganyika territory.
» Nimeuchota mchango huu kwenye jukwaa la Mabadiliko.
HAYA MAELEZO SI YA KUBEZA HATA KIDOGO, ZITTO HAAMINIKI, ANAWASILIANA NA AKINA nCHEMBA, MAKAMBA JR, TISS NA NDIO ALIYEKUWA ANAASISI KUBADILISHWA KWA UMRI WA KUGOMBEA URAIS NA WAZEE WASIGOMBEE NA MENGINE MENGI HUYU HAAMINIKI NA ANATUMIWA SANA NA CCM NA ANAPEWA PESA NYINGI SANA KWA KAZI HIYO. aLAANIWE KABISA KAMA ANATUMIWA KUZUIA UKOMBOZI WA NCHI YETU KUTOKA KWA MAKABURI WEUSI (CCM). wATANZANIA TUAMKE NA TUKATAE MBINU OVU ZA KUTA KUENDELEA KUTUKANDAMIZA.