Zinedine
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,187
- 694
Nyie chekeni na watu wanaotoa barua za chama nje ya chama,huyo mtu aliyeitoa barua hiyo na kuiweka JF sio mtu wa kucheka nae kabisa,kwa maana hiyo anaelewa nini kinaendelea ndani ya chadema na ipo siku atafanya lolote lile baya juu ya chama chenu,ni wakati sasa wa kupambana na hivyo vimelea la sivyo itakuwa ni story ya kumpa nyani alinde mahindi yako
kuna kirusi ndani ya chadema,ni lazima dawa itafutwe kukiangamiza
Asante eng. kwa kutoa maoni yanayolenga kutibu badala ya kupongeza au kulaumu. Bila shaka mkakati wa haraka wa Chadema sasa uwe ni kukitoa hicho kirusi vinginevyo, nothing will move on; yaelekea huyo aliyevujisha habari ya barua hiyo alifanya moja kati ya yafuatayo:
1. alimsomea mtu kwa simu ili aiandike
2. Aliinakili kwa kalamu ili kutoingia katika mtego wa simu
3.Aliipiga picha hiyo barua kwa cimu yake na kisha kuinakili akiwa nje ya ofisi
Kimsingi watuhumiwa namba moja hapa ni source and destine ya barua kwa maana ya ZZK inakotoka na Dr. Slaa inapokwenda; kwa vile si rahisi wawili hawa kuvujisha barua hii, moja kwa moja big suspect iende kwa waliohusika na kuitoa barua hii toka kwa Zitto hadi kumfikia Katibu Mkuu. Hao wote watakaobainika kuwa ni sehemu ya dispatching ya barua hiyo, regardless/ kabla hawajathibitika, kwanza wote wahamishwe ofisi ya katibu mkuu/makao makuu.
Lakini vilevile njia nyingie ni kuwabaini wale "Big suspects" na kuwaondoa katika chain bila wao kujijua. Mathalan kuwapeleka baadhi yao hata masomoni ili wawe nje ya ofisi na Tanzania kwa ujumla au kuwabadilisha majukumu na ofisi pia then ifanye "trial & error" ya kuangalia movement ya habari za chama ikoje.
Lakini mwisho ningependa kushauri kuwa Chadema isifanye kosa la CCM, kuruhusu "wajingawajinga" kujipenyeza ndani ya chama na mwisho wa siku ndio wanaokuja hata kuomba nafasi za juu za uongozi wa chama au Taifa, na hatimaye Chama au nchi kupata watu ambao "incapable"