Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,355
Mkuu mi nakunaliana na wewe kwa 101%... Nilichoandika ni kufuatia mtiririko wa matukio, zikiwemo threads na posts humu JF zilizolenga kujenga uhasama kwa Zitto, bila sababu ya msingi na kwa ushahidi dhaifu.Hapo kwenye blue sijakuelewa.Lakini napenda kutoa maoni yangu kuwa,kipindi hiki ni kipindi cha kila mtanzania mwenye moyo wa ukombozi kuchukua tahadhari kwa lile alisemalo au analoliandika ili mwisho wa siku nchi hii ikombolewe mikononi mwa mafisadi.Mh.Zitto amaeleza kwa uwazi na ameeleweka,lakini wachangiaji wa hoja ya Mh.Zitto tuwe makini tusijekuleta mgawanyiko usiokuwa na maana.Nijuavyo mimi Dr.Slaa ni katibu mkuu wa CDM na MH.Zitto ni katibu Msaidizi,sasa hizi story za watakuja kwa jina la Slaa zinatoka wapi? Msaliti anaweza asije kwa jina la mtu akaja kwa jina la chama huyo utamfanyaje? Kila mmoja wetu akiwa mlinzi wa CDM hakuna atakayebomoa mshikamano uliopo,cha kuzingatia ni kwamba tujiepushe na makundi bali tuwe kitu kimoja kuelekea 2015.
Wapo waliojitanabahisha kuwa wao ni watu wa ndani ya chama (kweli, kilikuwa na vijiushahidi kuwa ni watu wa ndani ya chama), na kuonyesha kuwa wapo karibu sana na Dr. Slaa, ili kuwajengea wanachadema hisia kuwa Dr Slaa na Zitto haziivi. Kwa bahati mbaya walifanikiwa kuwarubuni kihisia baadhi ya wanachadema.
Leo tunashuhudia kuvujishwa, kishabiki, kinafiki na kizandiki, habari za ndani za CHADEMA, kwa lengo la kutuvuruga akili.
Huwezi kuniambia kuwa aliyeweka ile barua hapa, ambaye ndiye aliweka ile video anaipenda CHADEMA, au anampenda Dr. Slaa. Lakini huwezi kukataa mtu huyo yuko karibu sana na chama, na inawezekana yuko ndani ya chama.
Kwa bahati mbaya 'mtu huyo' ambaye nia yake ni kumchonganisha Zitto, sasa amekuja clear, sio na title ya kumchonganisha tu Zitto, bali na title "CDHADEMA taifa vipande vipande!!!'... mtu aliyeko ndani ya CHADEMA!
Wengi tunamkubali Slaa kutuongoza kuindoa CCM, lakini ndugu kaangwa nikija hapa nikakwambia, "Mimi namkubali sana Slaa, na mtu wa karibu naye... na Zitto ni mtu mbaya sana na anatumiwa na CCM"... Hata kama umethibitisha kwamba kweli niko karibu na Slaa, lakini kukuambia tu hivyo haiwezi kuwa sababu ya kutosha kukufanya uanze hapo hapo kumchukia Zitto. Unapaswa asikilize nilichosema, ukipime, ufanye tafiti ndipo uwe na uhakika kama nilichosema kina mantiki...