BASATA: Yapo wapi maadili kwenye hii nyimbo "Darasa la saba ya Mbosso" inayohamasisha mapenzi kwa watoto wa shule?

BASATA: Yapo wapi maadili kwenye hii nyimbo "Darasa la saba ya Mbosso" inayohamasisha mapenzi kwa watoto wa shule?

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
10,488
Reaction score
20,051
Habari wana JF,

Niende moia iwa moja kwenye hoja yangu ambayo pia naileta kama swali kwa baraza la sanaa ambalo huwa linasimamia pia maadili kwenye kazi za sanaa pamoja na mamlaka zetu zote zinazohusiana na kumlinda mtoto zikiongozwa na wizara husika.

Kuna huu wimbo mpya ya msanii Mbosso inaitwa darasa la saba, kwa sasa no nyimbo inayopigwa na vyombo vingi vya habari pamoja na maeneo mbali mbali ambayo watoto wetu wadogo kabisa wqliopo shule wanaisikia na pia kujifunza mambo kutokana na nyimbo hiyo.

Tatizo kubwa lililopo kwenye nyimbo hii ni kuhamasisha mahusiano ya kingono baina ya wanafunzi. Nyimbo hii haijazingatia maslahi ya mtoto hata kidogo na hili ni hatari kwa taifa letu kama tutakubali watoto wetu waliopo mashuleni wafindishwe kuwa mapenzi ni jambo la wao kulizingatia kwa sasa.

Wakati serikali inaweka adhabu kali kwa watu wanaokatisha masomo mabinti kwa kuwapa mimba au hata kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi, basi inapaswa kuikabili nyimbo hii kwa namna itakayoona inafaa. Mheshimiwa waziri Dkt. Gwajima D ni ombi langu uweze kuifuatilia nyimbo hii na kuona namna utaweza kuhakikisha maslahi ya mtoto yanalindwa.

Mapungufu ya wimbo huu embu tufukirie je serikali inaweza kupiga nyimbo hii kwenye matukio kama, siku ya mtoto duniani, mbio za mwenge wa uhuru au hata kampeni mbali mbali?. Kama jibu ni hapana basi tutakubaliana kuwa nyombo hii haijakaa sawa kimaadili na inapaswa kuzuiliwa.

Ni rahisi kupiga nyimbo ya Mapenzi na shule ya Saida Karol kuliko hii kwa sababu Saida aliwaonya watoto wetu juu ya kuchanganya mapenzi na shule/elimu lakini huyu wa sasa Mbosso anahamasisha kuwa inawezekana na inapaswa kuchanganywa na kufaidi wakati bado upo shule.

Swala hili halipo sawa na inapaswa kushughulikiwa.

Wimbo husika inapatikana kwenye mitandao mbali mbali.

Asanteni.

CC:
Dkt. Gwajima D
 
Niliachaga kuusikiliza mziki wa bongo flava kitambo sana tena na sasa hivi mmeletwa singeli ndio mtakoma.

pop/rock za 80s, RnB za 90s na 2000s, rap songs kuanzia miaka ya 2000 kurudi nyuma ndio mziki wangu.
 
Kuna huu wimbo wa miaka 18 wa Jay Melody umefanya watoto wengi kuingia kwenye mapenzi wangali wadogo kufuatia kuhamasisha kwake kuwa hakuweza kuvumilia awe mtu mzma ayaanze mapenzi. Nyakati hizo unatoka nilikuwa na library ya computer wateja wangu wengi wa huo wimbo walikuwa vibinti vidogo, nilikuwa napata shida kuwaelimisha wasifuate mafunzo ya huo wimbo bali wausikilize tu.
 
Kwanza rekebisha uandishi, usiandike "hii nyimbo", usahihi ni huu wimbo.

Pili, Tatizo la ujumbe katika nyimbo nyingi za wasanii ni walaji. Inaonekana nyimbo za mapenzi zenye maneno makali ndio zina soko.

Wangeimba ukulima wa kisasa mngewaangalia?
 
Kuna sheria yeyote inayomkataza mwanafunzi asishiriki mapenzi angali akiwa skuli mbali na miongozo na sheria za shule? Manake hakuna sheria inayomkataza kufanya hivyo,na mara nyingi ikibainika mtu ametembea na mwanafunzi hubadilishiwa kesi na kuwa ubakaji. Au nakosea ndugu wasomaji?
 
Kuna huu wimbo wa miaka 18 wa Jay Melody umefanya watoto wengi kuingia kwenye mapenzi wangali wadogo kufuatia kuhamasisha kwake kuwa hakuweza kuvumilia awe mtu mzma ayaanze mapenzi. Nyakati hizo unatoka nilikuwa na library ya computer wateja wangu wengi wa huo wimbo walikuwa vibinti vidogo, nilikuwa napata shida kuwaelimisha wasifuate mafunzo ya huo wimbo bali wausikilize tu.
Ndugu, sikuizi watu kubalehe mapema, wengine darasa la 5 tu tayari. Kwaio ni malezi yako
 
Kuna sheria yeyote inayomkataza mwanafunzi asishiriki mapenzi angali akiwa skuli mbali na miongozo na sheria za shule? Manake hakuna sheria inayomkataza kufanya hivyo,na mara nyingi ikibainika mtu ametembea na mwanafunzi hubadilishiwa kesi na kuwa ubakaji. Au nakosea ndugu wasomaji?
Ipo, sheria ya elimu. Marekebisho ya sheria ya elimu yalifanya kuwa na mahusiano na mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa ni kosa la jinai. Tena hapo ni bila kuzingatia kabisa umri akishakuwa ni mwanafunzi wa shule tu kwisha habari yako.

Mbaya zaidi ni ikionekana una uelekeo huo wa mahusiano, na hapo sio lazima iwe umesha jamiiana naye hapana hapo ni kitendo tu chakuwa na mahusiano. Adhabu ni miaka karibu 7 jela.

Inakuwa ubakaji kama mmeshajamiiana au mmekamatwa mkijamiiana, inakuwa ubakaji kwa mujibu wa sheria. Na hapo tena kuna marekebisho ya sheria ya elimu ambayo yalisema ukiwa umempa ujauzito kuna fidia ambayo utatakiwa kulipa.

Pona yako ni kama huyo mwanafunzi ni juu ya miaka 18 au miaka 18 hapo ubakaji wa kisheria utaukwepa ila utabaki na makosa mawili, kumpa mimba na kosa la kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi. Ambapo hapo uatachezea miaka 7 na hiyo fidia ambayo ni kama milioni 5 hivi kama sijakosea.

Kifupi ni kuwa ni hatari sana kuwa na mazoea na mwanafunzi wa kike, maana hata mazoea ya kawaida tu yanaweza yakakuingiza kwenye matatizo makubwa sana maana ni ngumu kutenganisha upendo wa kawaida na upendo wa kimapenzi kati ya mwanafunzi wa kike na kijana wa kiume asiye ndugu yake.

Na hayo ni marekebisho ya sheria ya tangu 2020.
 
Tatizo lilianzia pale viongozi waliopewa dhamana kutokea pwani,kwa sababu kwa mikoa ya pwani maadili ni 0+0=0 si wakubwa kwa wadogo ni matusi mwanzo mwisho+mziki wao wa singeli umejaa matusi tu
 
Hapana jipya chini ya jua, watoto wameshaharibika kitambo sana, hivi sasa tunafanya kumwagilia na kuongezea rutuba tu.
 
Baada ya kuona mbosso amewashika pabaya mnaanza visababu vya hovyo
Kipindi nyegezi ya Diamond & rayvan inatoka mlikua wapi
 
Back
Top Bottom