Bashar Assad akwepa mtego wa Kuiingiza Syria katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe, Hongera Urusi na Iran kwa ushauri mzuri

Bashar Assad akwepa mtego wa Kuiingiza Syria katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe, Hongera Urusi na Iran kwa ushauri mzuri

Tumbaku kabisa, mmeanza kujitekenya na kucheka wenyewe?
 
Kwani Kuna sheria ya kusoma alama za nyakati? Kwamba usiposoma hizo alama mwaka Fulani ukija kuzisoma mwaka unaofuatia utakua umekosea.?
Assad kakimbia kwa sababu kapigwa, kashindwa kulipa wanajeshi wake, kakosa support ya Warusi, Hizbollah na Wairan.

Hicho ni kipigo tu, hakuna busara hapo.
 
Na kwa nn Assad aliwaambia Urusi waufute mji wa Allepo hiyo miaka?na Urusi kwa kutumia ndege vita zake aliuuwa kila kumbe alichoona kinatembea? Mji ukageuka zaidi ya Gaza. Halafu leo wanasifiwa
Kuna watu hawana aibu. Wanafikiri ukikomalia kusema uongo, unageuka kuwa ukweli.
 
Nyote mnaweza kuwa sahihi,lakini 2011 serikali yake ilikua strong financially na bado alikua na matumaini
Hakuna wote kuwa sahihi.

Kama kweli Assad ana busara za kuepusha nchi na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa nini hakukimbia mwaka 2011 kabla vita haijaanza?

The fact kwamba hakukimbia 2011 wakati ana pesa, kakimbia 2024 alipoishiwa na pesa, maana yake ni kwamba kakimbia kwa sababu kaishiwa na pesa, si kwa sababu anataka kuiepusha nchi yake na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe kashapigana kwa miaka 13.
 
Bila shaka amechukua approach hii baada ya kuona madhara ya 2013, hivyo hajataka yajirudie
Amechukua approach hii kwa sababu kaishiwa na hela hana hata mshahara wa kuwalipa wanajeshi wake.

Amechukua approach hii kwa sababu rafiki zake Warusi, Hizbollah na Wairan waliokuwa wanamsaidia hapo awali wote wana vita zao wameshindwa kumsaidia safari hii.

Amechukua approach hii kwa sababu kashindwa, kapigwa, si kwa sababu anataka kuepusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Ya kwasasa wamagharibi walijipanga Sana kama ukraine kumkomoa Iran na Urusi bahati nzuri intelijensia za urusi na Iran wameling'amua hilo mapema, wameondoka na Assad na mabilioni ya dola na dhahabu yote waanze upya western limewauma sana hilo😆
Assad kaondoka kwa sababu kapigwa, kwa sababu rafiki zake Warusi, Hizbollah na Iran wako busy na vita vyao.

Kaondoka kwa sababu kapigwa, si kwa sababu anataka kuiepusha Syria na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Assad agreed to step down following back-channel talks with unspecified armed groups and left the country, instructing officials to conduct “a peaceful transfer of power,” the Russian Foreign Ministry said on Sunday.
Kwa nini kakubali 2024 na hakukubali 2013?
 
Unaambiwa Assad kaishiwa hela halafu rafiki zake Warusi, Hizbollah na Wairan wana vita zao wameshindwa kumsaidia.

Sasa mtu kaishiwa hela, marafiki zake wameshindwa kumsaidia, kashindwa vita, unasema katumia busara kukimbia wakati kashindwa vita?
Hizo ni propaganda tu hakuna ukweli wowote kuwa kaishiwa hela.
 
Unampangia muda wa kukubali?
Angetaka kuiepusha nchi na vita vya wenyewe kwa wenyewe angekimbia kabka haijaanza.

Mtu aliyepigana kwa miaka 13 akakimbia kwa sababu kashindwa hajaiepusha nchi na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Angetaka kuiepusha nchi na vita vya wenyewe kwa wenyewe angekimbia kabka haijaanza.

Mtu aliyepigana kwa miaka 13 akakimbia kwa sababu kashindwa hajaiepusha nchi na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Ushauri wako hata kama angeusikia hiyo miaka 13 iliyopita asingeufanyia kazi .muda sahihi wakuufanyia kazi kwa mtazamo wake ni mwaka huu
 
Acha story nyingi wewe, nani kakwambia bwana Assad ameachia madaraka kuepusha civil war? Kwani hii ndio mara ya kwanza Kukutana na jaribio la kupinduliwa au? Mbona huko nyuma alikuwa anapambana nao pasipokujali kama hiyo civil war inaweza ikatokea?

Huyu jamaa amelazimika kuachia madaraka baada ya kuona mabwana zake(Urusi na Iran) hawawezi Tena kumpa sapoti kama walivyokuwa wakimpa huko nyuma, maana hata wao wenyewe wako kwenye kipindi kigumu sana hivyo hawana rasilimali za kutumia eti wanamlinda bwana Assad na wakati wao wenyewe wanahitaji hizo rasilimali sana tu kipindi hiki, kwa hiyo walichoamua ni kumpa hifadhi yeye na familia yake basi.
 
Ngoja wachezee moto 🔥 hiyo hatua waliyofikia wameifikia kwa hisani ya Israel na wakicheza watarudishwa Idlib.
 
Ndio ni wako wewe ndio umesema
Hapana, mimi kusema hakufanyi kuwa wangu.

Nikisema Morogoro Road inasafirisha magari kutoka Dar mpaka Moro mimi kusema hivyo hakufanyi Morogoro Road kuwa yangu.

That is just a fact. Me stating a fact does not make that fact my fact.
 
Hapana, mimi kusema hakufanyi kuwa wangu.

Nikisema Morogoro Road inasafirisha magari kutoka Dar mpaka Moro mimi kusema hivyo hakufanyi Morogoro Road kuwa yangu.

That s just a fact. Me stating a fact does not make that fact my fact.
Haya
 
Back
Top Bottom