Bashe amewakuta Watanzania wananunua kilo ya mchele 1,800 sasa wananunua 3,500

CCM hii nchini iliwashinda zamani, wanalazimisha kwa kuiba kura, matokeo yake ndio haya
 
Naunga mkono Uzi huu. Ingawa Nampa pole mleta Uzi kwa kashfa anazoletewa humu na baadhi ya watu ambao nahisi wananufaika na mfumo wa Bei za vyakula kupanda. Maoni yangu; hakuna namna waziri mwenye dhamana anaweza kukwepa lawama katika hali hii! wananchi wanapata tabu sana kwa hali hii ya Sasa kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuthibiti bei za mazao/ vyakula tangu awali, basi kama Kuna maghala ya vyakula ya serikali ambayo waziri wa kilimo alifanya jitihada hizo ili kuja kusaidia wananchi, huu ni muda muafaka sasa kuyafungua na kuuzia wananchi vyakula ili mabwanyenye wachache waliojipanga Sasa kuwahujumu na kuwaumiza wananchi washindwe. Ningekuwa Mimi waziri ningetoa bei elekezi ya mahindi ,Michele na maharage. Atakae uza zaidi ya hapo, akamatwe. Nchi hii inahitaji twende hivo maana wajaja wengi,wanaojingalia wao tu. Nawasilisha hoja.
 
Wewe ni mkulima?
 
Waziri Hana kosa kwani yeye kazuia mvua isinyeshe? Unafikiri kwa kutumia nn? Jiongeze mwenyew kama UNATAKA chakula fanya kilimo cha umwagiliaji, by the way huna mtaji.
 
Wewe uko dunia gani. Kwa nini unataka mkulima apangiwe bei ili uje uchukue kwa bei ya chee. Umeambiwa kilimo ni biashara kama biashara nyingine. Basi kama nia ni kukabiliana na upungufu wa chakula na bei kuwa juu, basi kila mmoja wetu achangie. Ukiwa mfanya kazi ukatwe pesa kuchangia kupanda bei ya chakula, kuanzishwe kodi ya kulinda bei ya chakula nk nk. Siyo mzigo wote atupiwe mkulima ambaye, anapohangaika kipindi cha msimu nyie wote mnapiga miluzi mijini kungojea vya nafuu.
So kama una-hoja iwe ni kwa kila mmoja wetu.
Na tunasema, kwa mpango wa waziri wa kuwa kilimo ni biashara, basi tuiachie miaka kama kumi hivi, tutakuwa tunazungumza mambo mengine, panya road na machinga na rundo la wahitimu wa chuo kikuu kukaa kusubiria ajira za ofisini litakwisha.
Mambo ya bure bure yameichelewesha sana nchi hii. Kila mtu anatakiwa ale kutokana na jasho lake na si la mwimgine. Na maandiko yanaagiza hivyo.
 
Huyu ni waziri wa matamko tu.hana tofauti na mtu wa takwimu anasema mfumuko wa bei kwenye chakula ni himilivu halafu anafananisha maisha ya Tanzania na nchi jirani.kila nchi ina tamaduni na taratibu zake za kuishi wengine wanakula mlo mmoja kwa siku wanakuwa comfortable.
 
Pesa ni za kwao wenyewe pia??
Na haitashuka kwa sababu wanunuzi wa mazao kutoka nchi za Kenya, Uganda, Kongo, Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi wako mashambani wananunua wenyewe mazao
 
Mimi nauza first clas rice,1500 kwa kilo,karibuni wateja nipo Mburahati.
 
Inakuwaje wananunua na V8 ya milioni 500 wakati hali ya uchumi ni mbaya.
Ebu muulize Bashe anatembelea gari la thamani gani.
 


Mimi nampongeza sana Bashe bei ilikuwa chini kwasababu wananchi walizuiwa kufanya kilimo kuwa biashara na kulazimishwa na kupangiwa bei. Hili lilifanya wawekezaji wengi wasiwekeze kwenye kilimo. Bei ya sasa ndiyo bei ya ukweli na tunatakiwa kuongeza kilimo na kupunguza gharama za uzalishaji sio kuzuia wakulima kuuza chakula nje. Hivyo kama unataka bei ipungue basi unga mkono jitihada za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuhimiza umwagiliaji na kujenga magala. Kulalama tu ni utamaduni ambao hausaidii yeyote. Huwezi kushinda vijiweni mapori yapo kila mahali na kulalamikia bei wakati hutaki kufanya kazi.
 
Yaa
Yaani walewale wanaohaidi wananchi maisha mazuri ndo wanaopinga mkulima kupata bei nzuri ya mazao yake. Yaani vitu vimepanda bei madukani, lakini watu wanataka mazao ya mkulima yasipande. Kilimo sasa ni dili, tikaende kulima najua tutafurahia.
 
Wakalaumiwa sio Bashe katika Hili, Sisi Kama Taifa Tumekosa Statesmen wenye Vision ya Kulinda Hili taifa, Nyerere angekuwa Mlafi leo tungekuwa tunaongea mambo mengine but he was true statesman, Tumeachia Kundi la Wahuni ndo wame ascending na Kuhold vital positions, Sasa they dont care about inflation, Wao wanaangalia namna ya kulast longer au kwenda juu zaidi ya positions walizopo
 
Watu wanashika nafsi bila kuwa na uwezo na bado wapo.

Rais anashiriki mikutano tu huko nje ya nchi ambayo ina very little impact kwenye maisha ya watu.
 
Exactly,
 
Huo upumbavu wenu wa kufunga mipaka ulizikwa na Magufuli. Mipaka itaendelea kuwa wazi, wakulima wawauzie wateja popote ili wapate Bei nzuri.

Watanzania wana ardhi yenye rutuba na ardhi inayolimwa ni chini ya 15% ya ardhi yote. Wananchi wengi hawaoni tija kwenye kilimo sababu ya bei ndogo wanazopata. Wengi wako kwenye umachinga, ususi wa nywele, viduka vidogodogo na u mama ntilie. Hii sasa ni wakati tukatambua kuwa kilimo ni biashara na kilimo ni uchumi. TOKENI humu JF nendeni mkalime
 
Na haitashuka kwa sababu wanunuzi wa mazao kutoka nchi za Kenya, Uganda, Kongo, Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi wako mashambani wananunua wenyewe mazao
Bashe anaakili mbovu sana
 
Na haitashuka kwa sababu wanunuzi wa mazao kutoka nchi za Kenya, Uganda, Kongo, Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi wako mashambani wananunua wenyewe mazao
Halafu mtu anakuambia eti wakulima hawafaidiki bei hizi? Hivi kweli Mmalawi au Mzambia amefuata mazao shambani kwako utamuuziaje kwa Bei ya chini? Basi utakuwa TAAHIRA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…