Mwanahabari wa Taifa
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 1,588
- 956
- Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia ametoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia metoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Bashe ameyasema hayo leo Oktoba 3 alipotembelea skimu hiyo, akisema wameweka mkakati ambao utamlinda mkulima, lengo ni kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia shughuli zao za kilimo.
"Ni dhambi kuwaletea matumaini ambayo hayapo. Utaratibu uko hivi, nimempa Mhandisi siku 45 zabuni iwe imetangazwa ,watafanya michakato yao kumpata mkandarasi kwa hiyo hii skimu hii yenye wakulima 250 haitaanza kujengwa leo itachukua muda.
“Ninaamini msimu huu hata ukianza skimu haitakuwa imejengwa kwa sababu miujiza ilikuwepo wakati wa mtume Muhammad na Yesu, siku hizi hakuna miujiza," amesema Bashe na kusisitiza lazima taratibu ziwepo kufanikisha ujenzi.
Ameongeza skimu hiyo itajengwa mfereji mkuu ambao utakuwa na kilomita nane na mifereji mitano ambayo itakuwa na kilimota 7.5 kwa hiyo wakulima hao wasubiri lakini amewahakikishia zabuni itatangazwa ndani ya siku 45 na mkandarasi lazima apatikane.
"Nataka kupata majibu katika kipindi kifupi kwamba mkandarasi tayari amepatikana na taratibu zote zinaendelea vizuri, tunataka kila kitu kiwe sawa ili Waziri aje kuzindua ujenzi wa skimu hii. Serikali itawekeza fedha hizo milioni 700 ili kujenga hii skimu ya Usense maana yake lazima fedhazirudi ili tukawekeze sehemu zingine.
"Bahati mbaya miradi mingi ya umwagiliaji ambayo imewekezwa imekosa ufanisi kwa sababu viongozi wanaopewa kuisimamia wengi wanakuwa wabadhirifu kwa sababu fedha zinazochangwa zinanaishia kwenye vikao," amesema.
Kwa upande mwingine, Bashe amesema Serikali imeanzisha Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji, hivyo wakulima wa kilimo cha umwagiliaj watapewa elimu kuhusu mfuko huo, ambapo wakivuna mazao kuna mchango ambao watautoa kuchangia.
"Mkulima asilazimishwe kulipa fedha kama hajalipa kiingilio cha kujisajili, mnaweza mkakubaliana mkulima akivuna kama ni asilimia 2.5 au tatu mpige mahesabu kwa gunia za mpunga halafu zile gunia zinahifadhiwa kwenye ghala la pamoja," amefafanua Bashe.
KAZI IENDELEE