Bashe: Rais Samia ametoa Sh700 milioni ujenzi skimu ya Usense mkoani Katavi yenye urefu wa 7.5km

Ni katika harakati za kuendelea kuwasifia viongozi. Hiyo hela hatoi SAMIA MFUKONI Mwake. Imetengwa katika bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/2022
 
Ametoa kwenye mshahara wake au kwenye biashara zake?

Kodi zetu ndo mnampamba kua rais ametoa? Hebu tupeni hishima walipa kodi
kwani hata kama ni kodi zenu akiusema hizo naenda kutanulia dubai utamwambia nini akisema hizo napeleka shuleni utamwambia nini? kaidhinisha ziende huko kwahiyo usikatae kuwa ametoa kwani unafikiri yeye atatoa kwenye mshahara wake? acheni ulimbukeni
 
Ametoaa mfukoni kwakeee?SEMA ameithinishaaa
 
Ametoa kwenye mshahara wake au kwenye biashara zake?

Kodi zetu ndo mnampamba kua rais ametoa? Hebu tupeni hishima walipa kodi
Kuna kitu mkuu Mr Dudumizi amekisema hapo juu, tafadhali kipitie!
 
..haya ndio mambo ya maana sio kununua midege toka kwa mabeberu na kutubebesha wanyonge mzigo wa hasara.
 
Kiukweli hii tabia ya kusema Rais katoa pesa kiasi fulani inakera sana.
Ni kweli, kwa sasa hivi inakera sana sana......ila miezi sita kurudi nyuma ilikuwa inapendeza hatari na kila aliyeitoa alipata likes za kutosha. HAKI YA NANI HII DUNIA!!!! Siku hiyo ya judgement day tutashangaa mengi sana!
 
Bashe pc

  • Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia ametoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
    Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia metoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Bashe ameyasema hayo leo Oktoba 3 alipotembelea skimu hiyo, akisema wameweka mkakati ambao utamlinda mkulima, lengo ni kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia shughuli zao za kilimo.

"Ni dhambi kuwaletea matumaini ambayo hayapo. Utaratibu uko hivi, nimempa Mhandisi siku 45 zabuni iwe imetangazwa ,watafanya michakato yao kumpata mkandarasi kwa hiyo hii skimu hii yenye wakulima 250 haitaanza kujengwa leo itachukua muda.

“Ninaamini msimu huu hata ukianza skimu haitakuwa imejengwa kwa sababu miujiza ilikuwepo wakati wa mtume Muhammad na Yesu, siku hizi hakuna miujiza," amesema Bashe na kusisitiza lazima taratibu ziwepo kufanikisha ujenzi.

Ameongeza skimu hiyo itajengwa mfereji mkuu ambao utakuwa na kilomita nane na mifereji mitano ambayo itakuwa na kilimota 7.5 kwa hiyo wakulima hao wasubiri lakini amewahakikishia zabuni itatangazwa ndani ya siku 45 na mkandarasi lazima apatikane.

"Nataka kupata majibu katika kipindi kifupi kwamba mkandarasi tayari amepatikana na taratibu zote zinaendelea vizuri, tunataka kila kitu kiwe sawa ili Waziri aje kuzindua ujenzi wa skimu hii. Serikali itawekeza fedha hizo milioni 700 ili kujenga hii skimu ya Usense maana yake lazima fedhazirudi ili tukawekeze sehemu zingine.

"Bahati mbaya miradi mingi ya umwagiliaji ambayo imewekezwa imekosa ufanisi kwa sababu viongozi wanaopewa kuisimamia wengi wanakuwa wabadhirifu kwa sababu fedha zinazochangwa zinanaishia kwenye vikao," amesema.

Bashe pcc
Pia, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kuhakikisha wakulima waliosajiriwa kwenye skimu hiyo wanapimiwa maeneo yao na kupewa hati ya umiliki wa mashamba, kila mtu awe na hati ya umiliki wa shamba lake ili wawe na uhakika ndiyo wawe na uchungu.

Kwa upande mwingine, Bashe amesema Serikali imeanzisha Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji, hivyo wakulima wa kilimo cha umwagiliaj watapewa elimu kuhusu mfuko huo, ambapo wakivuna mazao kuna mchango ambao watautoa kuchangia.

"Mkulima asilazimishwe kulipa fedha kama hajalipa kiingilio cha kujisajili, mnaweza mkakubaliana mkulima akivuna kama ni asilimia 2.5 au tatu mpige mahesabu kwa gunia za mpunga halafu zile gunia zinahifadhiwa kwenye ghala la pamoja," amefafanua Bashe.

KAZI IENDELEE
Mambo yanakwenda kisomi,hizi ndio ajira,aliyeko maeneo hayo,akalime,kilimo cha mpunga,kinalipa.Zamani ilikuwa mabibi zetu,wazee ndio kazi zao,vijana jitokezeni,ajira hiyo.
 
Nampongeza mama samia kwa kweli.2025 atapita tena.
Ila hawa mawaziri ndo wanamrudisha nyuma kwa kuchelewesha mambo.

Suala la hiyo skimu inabidi lifanyike haraka ili wakulima wanufaike.
 
Hongera raisi Samia kwa kuonesha uzalendo na upendo wa kweli kwa nchi yako. Wenye akili zilizo huru tunauona mchango wako uliotukuka ndani ya taifa letu, japo kuna wale ambao akili zao hazipo huru (yan wamezikabizi kwa viongozi wao) wanajifanya hawaoni unachokifanya. Wengi wao wanajua fika kuwa viongozi wao wamekaa bungeni zaidi ya miaka 10 hadi 15, bila hata kuacha alama ya kuchimba japo visima viwili vitatu kwa wapiga kura wao nk.
Hongera sana,ajira hizo.Mkulima mmoja,anaweza kusababisha ajira mpaka kumi,kuanzia wenye maduka ya mbegu,maduka ya zana za kilimo,madereva,tanboy,fundi wa magari,wabeba mizigo,mama lishe,wenye mashine za kukoboa,wauzaji wa mchele jumla,wauzaji wa mchele reja reja.
 
Nashangaa mtoa mada...Unamanisha Rais anamihela ameanza kugawa kama alivokua akifanya JPM?..kumbe hela za Umma viongozi wenu hujitwalia na kuzifany zao sio??
Hela ya Una,inayotumika vizuri.Matokeo mazuri,tunayaona.Hapo kwenye mpunga,ajira za kumwaga hizo.Kama uko karibu na sehemu ya kilimo,wahi shamba,uanze kilimo.
 
Bashe pc

  • Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia ametoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
    Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Rais Samia metoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya Usense na kuboresha uzalishaji wa zao la mpunga linalolimwa katika skimu hiyo iliyopo Kata ya Uruwira Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Bashe ameyasema hayo leo Oktoba 3 alipotembelea skimu hiyo, akisema wameweka mkakati ambao utamlinda mkulima, lengo ni kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia shughuli zao za kilimo.

"Ni dhambi kuwaletea matumaini ambayo hayapo. Utaratibu uko hivi, nimempa Mhandisi siku 45 zabuni iwe imetangazwa ,watafanya michakato yao kumpata mkandarasi kwa hiyo hii skimu hii yenye wakulima 250 haitaanza kujengwa leo itachukua muda.

“Ninaamini msimu huu hata ukianza skimu haitakuwa imejengwa kwa sababu miujiza ilikuwepo wakati wa mtume Muhammad na Yesu, siku hizi hakuna miujiza," amesema Bashe na kusisitiza lazima taratibu ziwepo kufanikisha ujenzi.

Ameongeza skimu hiyo itajengwa mfereji mkuu ambao utakuwa na kilomita nane na mifereji mitano ambayo itakuwa na kilimota 7.5 kwa hiyo wakulima hao wasubiri lakini amewahakikishia zabuni itatangazwa ndani ya siku 45 na mkandarasi lazima apatikane.

"Nataka kupata majibu katika kipindi kifupi kwamba mkandarasi tayari amepatikana na taratibu zote zinaendelea vizuri, tunataka kila kitu kiwe sawa ili Waziri aje kuzindua ujenzi wa skimu hii. Serikali itawekeza fedha hizo milioni 700 ili kujenga hii skimu ya Usense maana yake lazima fedhazirudi ili tukawekeze sehemu zingine.

"Bahati mbaya miradi mingi ya umwagiliaji ambayo imewekezwa imekosa ufanisi kwa sababu viongozi wanaopewa kuisimamia wengi wanakuwa wabadhirifu kwa sababu fedha zinazochangwa zinanaishia kwenye vikao," amesema.

Bashe pcc
Pia, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kuhakikisha wakulima waliosajiriwa kwenye skimu hiyo wanapimiwa maeneo yao na kupewa hati ya umiliki wa mashamba, kila mtu awe na hati ya umiliki wa shamba lake ili wawe na uhakika ndiyo wawe na uchungu.

Kwa upande mwingine, Bashe amesema Serikali imeanzisha Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji, hivyo wakulima wa kilimo cha umwagiliaj watapewa elimu kuhusu mfuko huo, ambapo wakivuna mazao kuna mchango ambao watautoa kuchangia.

"Mkulima asilazimishwe kulipa fedha kama hajalipa kiingilio cha kujisajili, mnaweza mkakubaliana mkulima akivuna kama ni asilimia 2.5 au tatu mpige mahesabu kwa gunia za mpunga halafu zile gunia zinahifadhiwa kwenye ghala la pamoja," amefafanua Bashe.

KAZI IENDELEE
Hizi SIFA ni balaa Fedha ya SERIKALI hivi Tukisema SERIKALI IMETOA HIZO FEDHA sio Sahihi?
 
Back
Top Bottom