Bashe: Rais Samia ametoa Sh700 milioni ujenzi skimu ya Usense mkoani Katavi yenye urefu wa 7.5km

Ni katika harakati za kuendelea kuwasifia viongozi. Hiyo hela hatoi SAMIA MFUKONI Mwake. Imetengwa katika bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/2022
 
Ametoa kwenye mshahara wake au kwenye biashara zake?

Kodi zetu ndo mnampamba kua rais ametoa? Hebu tupeni hishima walipa kodi
kwani hata kama ni kodi zenu akiusema hizo naenda kutanulia dubai utamwambia nini akisema hizo napeleka shuleni utamwambia nini? kaidhinisha ziende huko kwahiyo usikatae kuwa ametoa kwani unafikiri yeye atatoa kwenye mshahara wake? acheni ulimbukeni
 
Ametoaa mfukoni kwakeee?SEMA ameithinishaaa
 
Ametoa kwenye mshahara wake au kwenye biashara zake?

Kodi zetu ndo mnampamba kua rais ametoa? Hebu tupeni hishima walipa kodi
Kuna kitu mkuu Mr Dudumizi amekisema hapo juu, tafadhali kipitie!
 
..haya ndio mambo ya maana sio kununua midege toka kwa mabeberu na kutubebesha wanyonge mzigo wa hasara.
 
Kiukweli hii tabia ya kusema Rais katoa pesa kiasi fulani inakera sana.
Ni kweli, kwa sasa hivi inakera sana sana......ila miezi sita kurudi nyuma ilikuwa inapendeza hatari na kila aliyeitoa alipata likes za kutosha. HAKI YA NANI HII DUNIA!!!! Siku hiyo ya judgement day tutashangaa mengi sana!
 
Mambo yanakwenda kisomi,hizi ndio ajira,aliyeko maeneo hayo,akalime,kilimo cha mpunga,kinalipa.Zamani ilikuwa mabibi zetu,wazee ndio kazi zao,vijana jitokezeni,ajira hiyo.
 
Nampongeza mama samia kwa kweli.2025 atapita tena.
Ila hawa mawaziri ndo wanamrudisha nyuma kwa kuchelewesha mambo.


Suala la hiyo skimu inabidi lifanyike haraka ili wakulima wanufaike.
 
Hongera sana,ajira hizo.Mkulima mmoja,anaweza kusababisha ajira mpaka kumi,kuanzia wenye maduka ya mbegu,maduka ya zana za kilimo,madereva,tanboy,fundi wa magari,wabeba mizigo,mama lishe,wenye mashine za kukoboa,wauzaji wa mchele jumla,wauzaji wa mchele reja reja.
 
Mama anatisha sana aise, tuendelee kumuombea
Twamuombea sana,Mungu ampe Afya na umri umrefu.Wanawake ni viongozi wazuri sana,kama Mama Marya(Bi Mariyamu)Mama wa Yesu,na Bi Khadia(Mke wa Mtume Muhammad).
 
Nashangaa mtoa mada...Unamanisha Rais anamihela ameanza kugawa kama alivokua akifanya JPM?..kumbe hela za Umma viongozi wenu hujitwalia na kuzifany zao sio??
Hela ya Una,inayotumika vizuri.Matokeo mazuri,tunayaona.Hapo kwenye mpunga,ajira za kumwaga hizo.Kama uko karibu na sehemu ya kilimo,wahi shamba,uanze kilimo.
 
Hizi SIFA ni balaa Fedha ya SERIKALI hivi Tukisema SERIKALI IMETOA HIZO FEDHA sio Sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…