Bashe, Tofauti ya Sukari Kutoka Brazil vs itokayo Zambia na Uganda ni ipi?

Ukienda Mbeya sukari inayotumika ni kutoka Malawi na Zambia toka kitambo,na naamini kwenye 'border' zingine Sukari toka nchi jirani itakuwa inapatikana kwa wingi na kwa haraka,nabaki najiuliza kwanini Sukari isubiriwe toka Brazil ambako ni mbali wakati nchi jirani sukari ipo ya kutosha?
 
Sukari ya Jirani zetu ni HALISI ni kama tu ya kirombero, ni Bora hivyo kwao hawatapata faida wakinunua.

Ile ya Brazil ni fake, Si halisi, ni chemicals , ni Bei pia, lakini madhara yake Kwa AFYA ni makubwa.

Nyerere allipozuia wafanyabiashara kujiingiza kwenye Uongozi aliyaona haya.

Saiz Kila kiongozi anatafuta fursa mahala apate pesa.
 
Kwenda Zambia na Uganda hata watoto wanaotambaa wanaingia kila siku pale Tunduma kwa Zambia, hivyo haichukui wiki inachukua dakika tu.
 
Hakuna nchi inayofanya hivyo. Hiyo ni dhana ya kufikirika.
Namaanisha waruhusu hiyo ya Zambia na Malawi na Uganda ishindane bei na ya Brazil. Kama nchi hizo hazina ya kutosha kutuuzia itajulikana. Kwa nini wachague kuipa Brazil monopoly ya kutuuzia sukari?
 
kiuhalisia ningekuwa mimi ndiye anayeteua ningekuwa nishafuta uteuzi muda mrefu.mpaka sukari inaadimika ina maana waziri mwenye dhamana hakuwa anajua akiba ya sukari imebaki kiasi gani? hawawezi ku predict kwamba kwa akiba hii iliyobaki hatutoboi wakaandaa mazingira rafiki ya kuagiza sukari kabla haijapanda bei? eti waziri wa kilimo wakati hasaidii taifa kulima miwa ya kutosheleza .hahhaaaaaaa. mna bahati sana aisee.nchi nyengine umeshatemwa muda mrefu
 
Na kitu Cha kushangaza ni kuwa, Kila mwaka, lazima utokee upungufu ,uhaba utangazwe, watu waagize nje ya Nchi, braziliiii!!!

Serikali za kiafrika zinareflect maisha ya uswahilini, kumchangia Jirani Yako mwenye duka Haiwezekani, mtu Yuko radhi asafiri mile kadhaa.

Malawi, Uganda na Zambia wanazalisha sukari, iweje tuagize Brazil na kusubiri Kwa miezi?
 
Nilisikia Leo kwenye EFM radio kuna wananchi walipiga simu wanalalamika sukari kuwa haikozi na haina ladha ya sukari!
Inaweza kuwa ndiyo ukweli ila nani atakusikiliza na kukutetea wewe?.

Pasipo kujitetea mwenyewe basi subiri utetewe na ugonjwa pasipo kuwa na bima card!.
 
Unajua kitu inaitwa"GMO"ni kama Maji ukikataa kuyaoga basi utayanywa.😕
Daa, Uhai wetu unazidi kufupishwa kwa kila njia huku viongozi walioshika dola wanaona mi sawa tu acha tuondoke mapema!.
 
Si nyie wenyewe huleta ubabaishaji kila mara kwenye swala la mahindi,mara Jambo dogo,oooh ooh mmezuia mahindi yasiuzwe Kenya,Acha kujitoa ufahamu wewe.
Ni Nani anayeweza vumilia upuzi kama huu uliotukuka kwa biashara zake?
Kalb hayawan
 
Si nyie wenyewe huleta ubabaishaji kila mara kwenye swala la mahindi,mara Jambo dogo,oooh ooh mmezuia mahindi yasiuzwe Kenya,Acha kujitoa ufahamu wewe.
Ni Nani anayeweza vumilia upuzi kama huu uliotukuka kwa biashara zake?
Kalb hayawan
Kwa taarifa Yako anaeletaga shida ni Kenya sio Tanzania Sasa ukisema sisi unakuwa hueleweki Kwa sababu Tzn inazalisha zaidi na inahitaji soko kushinda hao Kenya.

Niliyegemea Serikali ya Kenya iongie mkataba maalumu na NRFA/CPB Ili watengewe kiasi maalumu Cha mahitaji Yao kila mwaka (quorta) ,hii ingewasaidia kuwa na constant supply.
 
Kwa hiyo unadhani sukari kiasi gani inahitajika kwa mwezi ili tu-import? Na Zambia, Uganda na Malawi wanazalisha kiasi gani ili uagizaji wetu usiharibu Bei zao za ndani?
Pia tujulishe gharama au Bei ya hizo nchi vs. Brazil.
Au unasema tu bila data?
HATUHITAJI DATA HATUHITAJI SUKARI CHAFU TUNATAKA SUKARI.TUMESHUTUKA MPANGO WENU CHAFU.ETI KUWALINDA WAWEKEZAJI WA NDANI MBONA HAMKULINDA WA NGANO MNAAGIZA UNGA WA NGANO NJE
 
HATUHITAJI DATA HATUHITAJI SUKARI CHAFU TUNATAKA SUKARI.TUMESHUTUKA MPANGO WENU CHAFU.ETI KUWALINDA WAWEKEZAJI WA NDANI MBONA HAMKULINDA WA NGANO MNAAGIZA UNGA WA NGANO NJE
Sukari Bora itokanayo na miwa halisi IPO UG na Zambia na Malawi Kwa Jirani zetu,

Lakini viongozi wanakimbilia fake Toka Brazil isiyokoza.
 
Wewe unaesema kweli mbona bei inazidi kupaaa?
 
Ya malawi kila Siku inakamatwa, sukari na magari yaliyobeba yanataifishwa, Ila tunataka ya Brazil
 
Sukari ya Brasil inatengenezwa kutoka sweet potato.
 
Sukari ya Brazil inauzwa kwenye minada ya kimataifa huko.

Imejaa utapeli mwingi.

Huyu jamaa ni ntu wa dili dili tu.

Hakuna lolote jema hapo.
 
Hii nchi wenye dhamana wanajali matumbo yao,,
Hapo kuna mtu anaka ale 10%,

Pale Kilombero K1 na K2 inatoka sukar moja nyeupe tamu hatari,, madukani huipat, utaipata ile nyingine ya kawaida,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…