Bashe, Tofauti ya Sukari Kutoka Brazil vs itokayo Zambia na Uganda ni ipi?

Salaam, Shalom!!

Tunaambiwa tusubiri mwezi tena Ili tupate sukari ya kututosha,

Ningependa kujua nini maana ya dharura?

Yaani tusubiri bunge likae ndipo libadili taratibu za kuwaondolea viwanda kuwa waagizaji pekee? Kwanini lisitoke tamko la dharura kuruhusu wafanyabiashara kuagiza sukari Toka Zambia na Uganda?

Nchi Iko kwenye uhaba wa Sukari, kwanini wafanyabiashara wasiruhusiwe kuvuka mipaka na kununua sukari hapo Jirani Zambia au Uganda?

Sukari Toka Zambia au Uganda ni wiki tu imefika.

Brazil kunani?
Hata ubora tu wa Sukari ya Kilombero imethibitika kuwa Bora kuliko ya Brazil, sukari Toka Brazil haikozi kwenye chai hata uweke vijiko 5 pia kuna tetesi kuwa sukari hiyo Toka Brazil ni GMO ,Bei Chee ila HASARA Kwa AFYA za watumiaji, cancer nk nk.

Ni muda mwafaka wa kununua sukari Kwa Jirani zetu kukidhi uhaba uliopo tukisubiri viwanda vyetu vya ndani vizalishe sukari ya kutosha.

Ombi: Tuchukue ndege yetu mpya ya mizigo ilopaki, ipakie shehena ya kutosha hapo Zambia na Uganda, ndani ya wiki shida ya sukari iwe historia.

Nawasilisha🙏
Mpaka mo afikishe mzigo. Watu wanaenda na biti mzee
 
Namaanisha waruhusu hiyo ya Zambia na Malawi na Uganda ishindane bei na ya Brazil. Kama nchi hizo hazina ya kutosha kutuuzia itajulikana. Kwa nini wachague kuipa Brazil monopoly ya kutuuzia sukari?
HATUHITAJI DATA HATUHITAJI SUKARI CHAFU TUNATAKA SUKARI.TUMESHUTUKA MPANGO WENU CHAFU.ETI KUWALINDA WAWEKEZAJI WA NDANI MBONA HAMKULINDA WA NGANO MNAAGIZA UNGA WA NGANO NJE
Haimaanishi ndiyo itatokea. Utabaki kupiga kelele lakini haiwezi kutokea. Kwani Hamna mafuso? Kachukueni hizo sukari Zambia au Uganda.
Go ahead! Kumbaf!
 
Serikali haijaruhusu kwenda huko. Inataka tukanunue Brazil. Watu wa Mbeya na Songwe wanatumia sana sukari ya Malawi na Zambia, ila ni "magendo."
 
Ndege zetu mpya kabisa zimepaki,

Tuchukue ndege Moja mpya itue pale Lusaka Zambia ipakie shehena ya kutosha sukari iwe mtaani ndani ya siku 7 tu.
Wazo zuri Ila ni hasara kwa mafuta ya ndege
Cost itakuwa juu na Bei juu
 
Hiyo sukari ya Brazil inayoitwa brown sugar ni sukari chafu na takataka za sukari ambazo ni very cheap, kama London wazungu hawali utumbo hivyo Wanigeria na Waafrika ni kujikusanyia tuu bure, the cost ni transport only!.

Sukari yote ya Zambia inapita Dar port!. Tuondoe tuu zuio la ku imports sukari, ya Uganda ipitie Mutukula, ya Zambia ipitie Tunduma, ya Malawi ipitie Kasumulu, ya Kenya ipitie Namanga na Holili, ya Rwanda ipitie Rusumo, Burundi kupitia Mayovu, Msumbiji kupitia Nakonde, it take just a day na sukari itakuwa imejaa Tanzania!.
P
Kwani Sukari ya Kilombero na viwanda vingine hapa Tanzania vinatengeneza sukari gani kama si brown sugar kwa matumizi ya nyumbani? Si kweli kwamba ni sukari chafu ila inakuwa haijaondolewa molasesi yote. Kiufupi brown sugar ina madini ya kutosha ya kasium, potasium na iron kuliko white sugar, na ni nzuri kwa chai. Si kweli kuwa sukari yote ya Zambia inaagizwa toka nje, kumbuka kampuni ya ILOVO inaoperate pia Zambia, Malawi, Tanzania na nchi nyingine kadhaa. Hapa boda za malawi na Zambia mpaka wiki mbili hadi tatu zilizopita sukari ilikuw ni Tsh 2800 kwa kilo, na tulinunua kwa matumizi ya nyumbani bila shida yoyote.
 
Salaam, Shalom!!

Tunaambiwa tusubiri mwezi tena Ili tupate sukari ya kututosha,

Ningependa kujua nini maana ya dharura?

Yaani tusubiri bunge likae ndipo libadili taratibu za kuwaondolea viwanda kuwa waagizaji pekee? Kwanini lisitoke tamko la dharura kuruhusu wafanyabiashara kuagiza sukari Toka Zambia na Uganda?

Nchi Iko kwenye uhaba wa Sukari, kwanini wafanyabiashara wasiruhusiwe kuvuka mipaka na kununua sukari hapo Jirani Zambia au Uganda?

Sukari Toka Zambia au Uganda ni wiki tu imefika.

Brazil kunani?
Hata ubora tu wa Sukari ya Kilombero imethibitika kuwa Bora kuliko ya Brazil, sukari Toka Brazil haikozi kwenye chai hata uweke vijiko 5 pia kuna tetesi kuwa sukari hiyo Toka Brazil ni GMO ,Bei Chee ila HASARA Kwa AFYA za watumiaji, cancer nk nk.

Ni muda mwafaka wa kununua sukari Kwa Jirani zetu kukidhi uhaba uliopo tukisubiri viwanda vyetu vya ndani vizalishe sukari ya kutosha.

Ombi: Tuchukue ndege yetu mpya ya mizigo ilopaki, ipakie shehena ya kutosha hapo Zambia na Uganda, ndani ya wiki shida ya sukari iwe historia.

Nawasilisha[emoji120]
Mtu anaitwa Bashe sijui basha unategemea nn?
 
Elewa kuwa anayeagiza sukari sio serikali bali ni viwanda vilevile vinavyozalisha sukari nchini ndivyo vimepewa kazi hiyo kwahiyo wananunua penye unafuu wa bei, sukari ya africa mara nyingi ni ya miwa ambayo ni bei ghari lkn ya Brazil ni sukari ya viazi mviringo bei yake ni sawa na bure.
 
Ni chain ya upigaji,

Haiwezekani Uganda na Zambia wanazalisha sukari, iweje tukiishiwa tusinunue Kwa Jirani zetu?

Iweje vibali vitolewe kuagiza sukari Brazil ambayo haikozi hata uweke vijiko 5?

Inaagizwa mbali Ili uhaba uongezeke Bei zipande, wapige pesa.
Hii sukar ya brazil ni kweli haikolez chai?
 
Tatizo la sukari ni siasa za kipumbavu na rushwa za 10%, CCM ni majanga matupu, hata umeme ni hivyo hivyo tuu, Bashe nilikuwa nafikiri ana akili lakini hili swala la sukari limeweka wazi ujinga wake ni mtupu kanisa, hafai kabisa Hana akili na inawezekana ni mla rushwa tuu
 
Elewa kuwa anayeagiza sukari sio serikali bali ni viwanda vilevile vinavyozalisha sukari nchini ndivyo vimepewa kazi hiyo kwahiyo wananunua penye unafuu wa bei, sukari ya africa mara nyingi ni ya miwa ambayo ni bei ghari lkn ya Brazil ni sukari ya viazi mviringo bei yake ni sawa na bure.
Siasa tupu na rushwa, kwanini wenye viwanda ndio wapewe uwezo wa kuagiza, acha yeyote mwenye uwezo aagize na soko litaamua na wababaishaji wote watakimbia
 
Hiyo sukari ya Brazil inayoitwa brown sugar ni sukari chafu na takataka za sukari ambazo ni very cheap, kama London wazungu hawali utumbo hivyo Wanigeria na Waafrika ni kujikusanyia tuu bure, the cost ni transport only!.

Sukari yote ya Zambia inapita Dar port!. Tuondoe tuu zuio la ku imports sukari, ya Uganda ipitie Mutukula, ya Zambia ipitie Tunduma, ya Malawi ipitie Kasumulu, ya Kenya ipitie Namanga na Holili, ya Rwanda ipitie Rusumo, Burundi kupitia Mayovu, Msumbiji kupitia Nakonde, it take just a day na sukari itakuwa imejaa Tanzania!.
P
Well said. But people in high places are not blessed with common sense.
 
Makonda mbona hili li sukari analifumvia macho?
 
Hiyo sukari ya Brazil inayoitwa brown sugar ni sukari chafu na takataka za sukari ambazo ni very cheap, kama London wazungu hawali utumbo hivyo Wanigeria na Waafrika ni kujikusanyia tuu bure, the cost ni transport only!.

Sukari yote ya Zambia inapita Dar port!. Tuondoe tuu zuio la ku imports sukari, ya Uganda ipitie Mutukula, ya Zambia ipitie Tunduma, ya Malawi ipitie Kasumulu, ya Kenya ipitie Namanga na Holili, ya Rwanda ipitie Rusumo, Burundi kupitia Mayovu, Msumbiji kupitia Nakonde, it take just a day na sukari itakuwa imejaa Tanzania!.
P
Mzee umegonga!!!
Mbona chumvi na viberiti vinapatikana kwa njia hivyo Mzee Pasco aliyo ielezea na hakuna shida!!!

Tuna viongozi wanao tuongoza siyo wabunifu kabisa

Wana akili za Kukariri
 
Elewa kuwa anayeagiza sukari sio serikali bali ni viwanda vilevile vinavyozalisha sukari nchini ndivyo vimepewa kazi hiyo kwahiyo wananunua penye unafuu wa bei, sukari ya africa mara nyingi ni ya miwa ambayo ni bei ghari lkn ya Brazil ni sukari ya viazi mviringo bei yake ni sawa na bure.
Sukari ya viazi mviringo😀😀😀

Ndomana haikozi hata utie vijiko 5,

Pia Kuna watu wanalalamika nguvu za kiume kupungua sababu za sukari fake na GMO zingine.

Sukari ya Zambia Si ghali, Sema wanahofia hawatapata supper profit ukilinganisha na fake ya Brazil.

Uzalendo Mzigo wa viongozi, utaligharimu Taifa.
 
Elewa kuwa anayeagiza sukari sio serikali bali ni viwanda vilevile vinavyozalisha sukari nchini ndivyo vimepewa kazi hiyo kwahiyo wananunua penye unafuu wa bei, sukari ya africa mara nyingi ni ya miwa ambayo ni bei ghari lkn ya Brazil ni sukari ya viazi mviringo bei yake ni sawa na bure.
Una uhakika na hili la sukari ya brazil kutokana na viazi mviringo? Nisaidie chanzo cha hii habari yako, kwani sijawahi kutana nayo popote, na kama inawezekana hiyo sukari itakuwa bei juu sana sana.
 
Back
Top Bottom