Bashe ujumbe wako murua, vazi lako laleta maswali kwa watanzania

Mkuu Kalamu
Nilichukua muda kufikiri kuhusu mada nikajikuta nalazimika kuchangia 'upuuzi'' kwasababu upuuzi ukiachwa utamalaki sote tutakuwa wapuuzi na wapuuzi wataendelea na uvumbuzi wa upuuzi.

Tumeuliza, Bashe kwa kuvaa kofia na Kanzu amekiuka dressing code ipi!

Pili, nani amesema kanzu na kofia ni mavazi ya dini fulani?
Wale Makadinali pale Vatican si wamevaa Kanzu na Kofia.
Wazee wa Kagera huvaa Kanzu na Kofia. Kilimanjaro Wazee wengi huvaa kofia.
Wanawake wa Pwani hujitanda nguo vichwani! n.k.

Nyerere alipohutubia Taifa kuhusu ugonjwa wa Kipindu pindu alivaa Baraghashia
Mkapa, Kikwete, Mwinyi na Magufuli wamevaa Kanzu na kofia kwa nyakati tofauti.
Bungeni Dodoma, Kanzu na Kofia ni sehemu ya dressing code

RC Chalamila mara ngapi amezungumzia mambo ya siasa akiwa na Kanzu na Kofia
Leo ni kipi cha ajabu! Bashe aliongelea Kilimo hakuwa na mada ya siasa ambayo ingeamsha hisia hasa kwa wapuuzi. Mbona alipotoa kauli Bungeni hatukusikia haya

Hoja ni kwamba, ukiitwa Hassan haikufanyi Mwislam. Ukiitwa John haiukufanyi Mkristo.

Vitabu vitakatifu havijaeleza dini gani ina vazi gani. Ni upuuzi tu wa Watanzania

Tukiwapa wapuuzi 'benefit of doubt' katika mada nonsense kama hizi hawataishia hapo.
Kesho watakuja na hoja ya kipuuzi zaidi, kwanini amevaa kanzu nyeupe.
Hawa ndio wanaleta joto kali unalosema na tunawajibu wa kuwakemea

Waulize waapuuzi hawa, nini 'impact' ya alichosema Bashe katika jamii yetu, mahusiano yetu na jirani, mahusiano yetu kimataifa n.k. hawana jibu kwasababu jicho lao ni katika 'trivial matters'

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Usikereke kwa vazi la Kiislamu, hivi ndivyo Masiha alivyokuwa anavaa na Wanawake kina Bikira Maria walivaa hijab na nikab!.

Wazungu ndio walibadili hizi nguo zinazovaliwa sasa, ili zisionekane ni za Kiislamu. Yesu amekulia Misri!.
P
Hilo siyo vazi la kiislamu ni vazi la Kitamaduni la watu wa Mashariki. Halihusiani na Uislamu. Wayahudi wamevaa kanzu sana tu miaka na miaka.
 
Paskali hujui chochote kuhusu historia, ungekaa kimya tu. Suti inavaliwa hadi na Xi Jinping, Al-Sisi, Erdoğan, Shigeru Ishiba, MBS, S. Jaishankar n.k
 
Tumia akili yako vizuri kilaza wewe. Huyo ni kiongozi wa serikali, huwezi kutoa press ya namna hiyo ukiwa na vazi la namna hiyo....tuacheni udini wa kipumbavu.

Mwisho; Serikali haina dini.
Mbona Nyerere alifanya hivyo sana tu. Au kwa kuwa yeye ni Mgala?
 
UONGO hakuna masista wa kanisa walioajiriwa shule au hospitali za serikali, labda kama wanajitolea tu.
Hujui wewe!
Wapo tena wengi tu kama ambavyo kuna waislam wengi tu wameajiriwa na kulipwa na serikali lakini wanafanya kazi za kanisa!
 
Hembu avae tu suti kuepusha hii milolongo yote, suti na vazi la kimataifa linakubalia kote duniani bila mbambamba, halina kipengele.
Hapa shida ni wafia dini kadhaa mkuu,-- i repeat kanzu sio dini.

Hapa shida ni maarifa machache ya wsnaolalamika ifike muda tuwe tunaambiana ukweli
 
Kuna mambo mengine yanashangaza na kustaajabisha, kwani kanzu ni msikiti Bashe kaliingiza bungeni? Na leo hii ndo Jidu kaliona hilo vazi bungeni? Kuna muongozo kwamba tamko la kiserikali vazi la kanzu lisivaliwe?
Kuna madhehebu ya kikristo huvaa kanzu nimeyashuhudia Kenya, Ethiopia na Sudan. Kenya kuna Akorino, Roho msalaba na Legion Maria huvaa kanzu na baragashia zenye msalaba mwekundu na wanawake hawatembei vichwa wazi, je hawa Jidu la Mabambasi akiwaona atawashangaa au atawalaani?
Kuna mambo ya msingi ya kujadili lakini siyo kanzu.
 
Wao watu wa haya madhehebu huwa wanaenda na kanzu zao katika shughuli za serikali, umma au biashara zao binafsi?
 
75% haina shida maana hapo karibia 50% ni wale waislam wa jina tu,, kwenye kitimoto na viti virefu baa wapo wanatwanga serengeti, hawa hawanaga shida kama wale wa swala 5 na misimamo mikali
 
Wao watu wa haya madhehebu huwa wanaenda na kanzu zao katika shughuli za serikali, umma au biashara zao binafsi?
Akorino nimemshudia, kwenye shuguli za kiserikali ya Kenya ni mbunge.
Je kuna sheria Bashe kavunja? Kama kavunja sheria ni sawa ila kama hakuna mimi sioni shida.
Pia nimeongelea pale Jidu aliposema kuhusu udini ndiyo maana nikasema siyo wote wanaovaa kanzu ni waislamu au hujanielewa ndg yangu Yoda?
 

Na sikujua kwamba apple sio tunda.
Pia hata nataka ambazo zimeshalipiwa na Malawi hazitasafirishwa, inamaana tunarudisha pesa au tungetoa kwanza mahindi ndio tulipwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…