Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Huyu Bwana ni Kati ya Wajamaa na Wazalendo wachache waliobaki katika Taifa letu.

Ili tuendelee tunahitaji wakina bashiru wengi kwenye Uongozi wa nchi na sio Wanufaika wa kuyengeneza matatizo ili wapate Fedha kupitia Matatizo.
Huyu ni mnadharia kama wanadharia wengine waliopo na waliotangulia akiwemo Nyerere. Nadharia zao zimelifikisha taifa hapa tulipo hivi sasa ambapo mkulima kwa miaka mingi amekuwa ndiyo mlisha taifa na yeye anaendelea kuvaa nguo za viraka na mazingira duni. Pindi kilimo chake kikianza kumlipa, hasa mkulima wa mazao ya nafaka na maharage ambao ndiyo wengi. Leo hii ahueni ingekuwa kubwa. Ona wakulima wa viazi mviringo na vitunguu ambavyo haviwekewi masharti wanavyonufaika.
So, wale wote wanaoshabikia kudhibiti usafirishaji wa mazao including huyu profesa mnadhanira, tunawaambia kuwa kama wana nia njema, basi suala la kukabiliana na upungufu wa chakula lisielekezwe kwa mkulima wa nafaka (mahindi) peke yake bali watu wote. Wabunge waanze kukatwa mishara na posho yao kuweka fungu la kukabiliana na njaa, serikali ipunguze matumizi na pesa inayopatikana ipelekwe kwenye huo mfuko wa njaa, wafanyakazi wote wakatwe mishahara yao na pesa iende kuimarisha food security, ipitishwe kodi maalumu ya kuchangia hili tatizo. Baada ya hapo tumpangie mkulima naye parcentange ya mazao yake kuchangia kama wengine. Bila hivyo kinachoendelea ni sawa na cha mkulima ni chako na chako ni chako.
Kwa hiyo tumwache mkulima apate haki yake hata kama kuna kiasi madalali wanapita lakini kwa kiasi kikubwa wakulima wanafaidika na wananadharia na wpenda short cut watuache na wamwache Rais na mtizamo wa kuibadilisha hii nchi.
 
Bashiru kaongea ukweli, japo watu wanamchukia ila njaa inashusha utu na heshima ya mtu
Baadae mwaka huu huu 2023,

Umetabiriwa ukame na njaa ambayo haikuwahi Kutokea tangu uhuru.

Kukauka Kwa MTO Ruvu na vyanzo vya maji ni Ishara juu ya yajayo juu ya nchi.

Tumepewa muda wa kutumia mvua kidogo kulima na kuhifadhi chakula.

Nabii asema, njaa hiyo na ukame waeza chukua Hadi miaka 3 na nusu.

USHAURI.

1. SERIKALI.

Mfute KAZI ndugu BASHE na atafutwe waziri atakayefanya jitihada ktk KILIMO na kujenga maghala ya kuhifadhi chakula.

Jambo hii lilifanywa na YUSUPH enzi za FARAO ilipotokea njaa ya miaka 7.

2.WANANCHI.

Tumieni pesa zenu kununua chakula na kutunza Kwa kadri muwezavyo Ili kustahimili yajayo.

Pia hakikisheni mnapunguza uwekezaji na matumizi yasiyo ya lazima, kiufupi tufunge mikanda.

3. WAKULIMA.

Tumieni mvua hizi kulima Kwa bidii na kutunza vyakula na msiuze.

4.WANA wa MUNGU.

Tuzidishe MAOMBI ya TOBA na REHEMA juu ya nchi yetu nzuri ya TANZANIA Ili Mungu aiondoe ADHABU juu yetu.

Ee Mwenyezi Mungu, Tunakuomba utusikie.

Aaaamen.
Yule waziri Bashe sio Kwamba hajui anajua Sana tu!

Sema ndugu zake watakula Nini!!?
 
Kuna binadamu wanajua ardhi ni chakula, hivyo kila wanapoona sehemu wanapanda chochote iwe miti ya matunda na hata mboga au chakula

Croatia kwa mfano wao wanaamini hivyo na wana 1.5m hectares kwa kilimo tu

Sisi ardhi kubwa namna hiyo tunalia njaa
Hakuna kulaumu mtu ni akili tu
 
Huyu mtu ana asili na uzoefu katika masuala ya taaluma, lkn pia ni mtu aliyekopwa kwa ajili ya sababu za kiutendaji za kisiasa. "Analysis" yake inaaminika na pia yenye mantiki, kwa mazingira na muktadha wa kijamii na kiuchumi tunayoyapitia kama taifa.

Baniani mbaya, ila kiatu chake ni dawa. Huyu ni mtu mwenye uaminifu wa milengo ya siasa za kijamaa, ila ni mtu mwenye msimamo wa kile alichoaminishwa na kukiamini.
Utashangaa wafanya maamuzi wanasema hawawezi ku intervene kwa kisingizio cha free market, kama ni free market kwanini mbolea ipo subsidized, je hiyo subsidy siyi kodi ya raia ambaye anatakiwa kupewa bei ya chakula inayoendana na kipato chake? Wanelezaje kuhusu externalities ambazo zipo kwenye kilimo chetu ambacho hakiko commercialized? Hiyo siyo induced scarcity kwakua yeye alishindwa kulinda externals kuchukua domestic food bila kuzingatia chakula ni security kwakua raia wenye njaa ni rahisi kuwa blackmailed?
Yale majibu ya Mh. Waziri sijui alishauriwa na experts wa nchi gani!
 
Kwa kweli ubunifu hauna kikomo. .
😅😅😅
Kuna binadamu wanajua ardhi ni chakula, hivyo kila wanapoona sehemu wanapanda chochote iwe miti ya matunda na hata mboga au chakula

Croatia kwa mfano wao wanaamini hivyo na wana 1.5m hectares kwa kilimo tu

Sisi ardhi kubwa namna hiyo tunalia njaa
Hakuna kulaumu mtu ni akili tu
Zile akili za Bashe alizokuwa nazo zimeishia wapi?
 
Uwezo wako wa kufikiri ndipo ulipoishia hapo kwenye ukabila.

Roho mbaya haitakufikisha popote
Sasa ukabila unatoka wapi!!?

Sinkweli kule hawalimi!!?

Roho MBAYA ipi Sasa kwani nimesema wanyimwe chakula!?nimesema waziri anajua kuwa akisitisha kwa tufani ya njaa ijayo nduguze watapata shida kwani shida iko wapi hapo!!?
 
Kuna jambo sijawahi kulielewa nchi hii na hili limekuwa linatokea mara kwa mara. Kama tuko kwenye kipindi ambacho watu hawana pesa, bidhaa si zinatakiwa zipungue bei na si kuongezea? Watu wakiwa hawana pesa, inamaanisha wanunuzi wa bidhaa wanapungua, na hilo linafanya wauzaji kupunguza bei.

Nini huwa kinatokea kinafanya hii kanuni ya uchumi isiwe inafanya kazi?
Bidhaa ili zipungue bei maana yake uzalishaji uwe mkubwa na ununuaji uwe wa haraka... hii inasaidia mzunguko wa pesa kuwa mkubwa hata kama profit margin ni ndogo ila niwaharaka faida inaonekana.
Uzalishaji ukiwa mdogo na purchasing power (uwezo wa kununua) ukawa ndogo maana yake kwanza bidhaa zinapatikana kwa bei kubwa na chache na utokaji wake niwa taratibu hivyo muuzaji analazimika kupandisha bei pia kufidia muda ambao bidhaa hazitoki... ukumbuke kwake maisha yanaendelea kama ni kula na other essential needs zinaendelea bila yeye kuingiza kwa haraka. Kwenye uchumi tunaita... Price elasticity of supply.
 
Utashangaa wafanya maamuzi wanasema hawawezi ku intervene kwa kisingizio cha free market, kama ni free market kwanini mbolea ipo subsidized, je hiyo subsidy siyi kodi ya raia ambaye anatakiwa kupewa bei ya chakula inayoendana na kipato chake? Wanelezaje kuhusu externalities ambazo zipo kwenye kilimo chetu ambacho hakiko commercialized? Hiyo siyo induced scarcity kwakua yeye alishindwa kulinda externals kuchukua domestic food bila kuzingatia chakula ni security kwakua raia wenye njaa ni rahisi kuwa blackmailed?
Yale majibu ya Mh. Waziri sijui alishauriwa na experts wa nchi gani!
Watakuja na hoja za kufunga mipak ni kuharibu soko [emoji23].
 
Jukumu la Serikali. Ni kulinda. Raia wake.

Ila kama serikali inaruhusu raia wa kigeni kununua chakula kiholela toka kwa wakulima moja kwa moja na kusababisha mfumuko wa bei inakua imefeli.

Haya ndio matatizo ya kuwapa mamlaka watu ambao sio wa asili yetu hawana uchungu wa nchi hata ikiharibika.
 
"Njaa inadhalilisha heshima na uhuru wa nchi, inatweza utu wa binadamu kwahiyo tatizo la mfumuko wa bei za vyakula ni tatizo ambalo tutake tusitake lazima tuongeze kiwango cha ubunifu kukabiliana nalo, hakuna ukomo wa ubunifu, wananchi wanakibiliana na tatizo hili.

"Nilikuwa nazungumza na wananchi mmoja amesema chakula cha asubuhi na mchana kinaunganishwa kwenye saa 5 na 6, mlo wa usiku unaunganishwa kati ya saa 11 na 12, hawasubiri kujadili mambo ya Ukraine na tabianchi, wameanza kuchukua hatua.
View attachment 2502022
Naomba kujuzwa je taifa letu limeshatangaza habari za njaa au kilichopo ni bei za bidhaa za nafaka kupanda?, wakurungwa kilio kimekuwa kikubwa sasa, liangaliwe kwa macho manne!
 
Umeeleza vizuri kwa kiasi fulani je, mapito hayo maovu pm, hayafahamu?, maana ndiyo sababu ya mama kuendelea kuwa na pm yuleyule ili kudumisha utaratibu uleule, na je vp hayupo hawa wote ni strong gears katika kuhakikisha mambo yanakaa sawa kwa kila upande, hatuwezi kumwachia kila kitu rais wetu kuna baadhi kuna kiutaalam na mengine ya kiuzoefu, na sidhani kama ni mama asiyeshaurika, it's could be something hidden!
Kwa taarifa zisizo rasmi PM amekalia kuti kavu mbele ya bi mkola yupo tu muda usogee aangalie issue zingine... kuna viwaziri vinanguvu kwa mama kuliko hata PM mara 1000. Vikijikombakomba vinawekwa mgongoni na kupulizwa taratibu... simsemi kwa ubaya bi hindu ila hana courage i mean sio shupavu kwenye kusimamia maamuzi mazito sio kwamba hawezi tu ila hana huo ujasiri ni mtu laini... she is too mother instead of leader... ndio alivyo mpole anaetaka kuwapet pet watoto wake maisha yaende. Anaumia lakini hataki kukuumiza pia na nchi inakuwa ya kipuuzi ukiwa legelege. Atakaejaribu kusimama kukemea anaoneka ame under rate maamuzi ya mkuu wake kwa hiyo inabidi wacheze kwenye bit moja kuweka maisha rahisi kwao. Bi mkola hana maamuzi kwenye mambo ya msingi ila ukimkosoa anahisi unamdharau haraka sana anakuzimisha.. ndio wasiojiamini walivyo.
 
Swala hili halina suluhu ya muda mfupi, suluhu ya uhakika ni kutengeneza mifumo ya kilimo cha umwagiliaji ambayo itachukua muda na gharama
mbona wananchi wamepata suluhu,au ni wabunifu kuliko serikali yenye nyenzo zote muhimu?
Basi serikali iweke utaratibu wa kuwasikiliza wananchi
 
Sasa ukabila unatoka wapi!!?

Sinkweli kule hawalimi!!?

Roho MBAYA ipi Sasa kwani nimesema wanyimwe chakula!?nimesema waziri anajua kuwa akisitisha kwa tufani ya njaa ijayo nduguze watapata shida kwani shida iko wapi hapo!!?
Ukabila wa kumuunganisha Bashe na Wasomali kwa vile tu asili ya wazee wake ni huko, na wewe tayari umeshamhukumu kwamba atapindisha sera za nchi ili asaidie wasomali.

Hata kama hao wasomali hawalimi lakini nani alikwambia wanategemea chakula kutoka Tanzania?
 
Viongozi wamefikia pahala wanawafanya wananchi kama ''rubber stamp''
Kauli kama hizi za mtake msitake tutaunda dola,uku unapita mitaani kuomba kura maana yake nini?
Kauli ya kusema, hivi kuna mtu kama ..... 2025?
Wakati tunasubiri ifikapo 2024 kuona watu wanapita mtaa kwa mtaa kuomba kura ,maana yake nini?
Kauli kama hizi za uzandiki,hata ungekuwa wewe ndo mwenyezi Mungu ungefunga mvua ili uone kama wenye maneno hayo wataleta mvua ya kwao. Na tukileta jeuri ya kusema tutamwagilia na vyanzo vya maji vitakauka.
 
Ukisoma vitabu vya imani utaona watawala walipoenda kinyume na maagizo ya Mungu katika kutawala,Mungu aliwaadhibu kwa kufunga mbingu zisilete mvua,na magonjwa kama tauni n.k
habari ya kusema ni tabia nchi,kwani zamani za shibe tabia nchi ilikuwa imeenda likizo?
Ni muda wa kuitisha maombi ya kitaifa Mungu atunusuru na zahama hizi.
Tutasema ni vita ya urusi na ukraine,je ni kweli na unga wa muhogo ulitoka ukraine
 
Huyu mchizi anapata wapi moral authority au audacity yakuongea?
The beauty of hatred is contagious, even if you are told to bring evidence of the badness of the one you hate, you keep saying I heard...
 
Back
Top Bottom