Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Huyu Bwana ni Kati ya Wajamaa na Wazalendo wachache waliobaki katika Taifa letu.

Ili tuendelee tunahitaji wakina bashiru wengi kwenye Uongozi wa nchi na sio Wanufaika wa kuyengeneza matatizo ili wapate Fedha kupitia Matatizo.
Huyu ni mnadharia kama wanadharia wengine waliopo na waliotangulia akiwemo Nyerere. Nadharia zao zimelifikisha taifa hapa tulipo hivi sasa ambapo mkulima kwa miaka mingi amekuwa ndiyo mlisha taifa na yeye anaendelea kuvaa nguo za viraka na mazingira duni. Pindi kilimo chake kikianza kumlipa, hasa mkulima wa mazao ya nafaka na maharage ambao ndiyo wengi. Leo hii ahueni ingekuwa kubwa. Ona wakulima wa viazi mviringo na vitunguu ambavyo haviwekewi masharti wanavyonufaika.
So, wale wote wanaoshabikia kudhibiti usafirishaji wa mazao including huyu profesa mnadhanira, tunawaambia kuwa kama wana nia njema, basi suala la kukabiliana na upungufu wa chakula lisielekezwe kwa mkulima wa nafaka (mahindi) peke yake bali watu wote. Wabunge waanze kukatwa mishara na posho yao kuweka fungu la kukabiliana na njaa, serikali ipunguze matumizi na pesa inayopatikana ipelekwe kwenye huo mfuko wa njaa, wafanyakazi wote wakatwe mishahara yao na pesa iende kuimarisha food security, ipitishwe kodi maalumu ya kuchangia hili tatizo. Baada ya hapo tumpangie mkulima naye parcentange ya mazao yake kuchangia kama wengine. Bila hivyo kinachoendelea ni sawa na cha mkulima ni chako na chako ni chako.
Kwa hiyo tumwache mkulima apate haki yake hata kama kuna kiasi madalali wanapita lakini kwa kiasi kikubwa wakulima wanafaidika na wananadharia na wpenda short cut watuache na wamwache Rais na mtizamo wa kuibadilisha hii nchi.
 
Bashiru kaongea ukweli, japo watu wanamchukia ila njaa inashusha utu na heshima ya mtu
Yule waziri Bashe sio Kwamba hajui anajua Sana tu!

Sema ndugu zake watakula Nini!!?
 
Kuna binadamu wanajua ardhi ni chakula, hivyo kila wanapoona sehemu wanapanda chochote iwe miti ya matunda na hata mboga au chakula

Croatia kwa mfano wao wanaamini hivyo na wana 1.5m hectares kwa kilimo tu

Sisi ardhi kubwa namna hiyo tunalia njaa
Hakuna kulaumu mtu ni akili tu
 
Utashangaa wafanya maamuzi wanasema hawawezi ku intervene kwa kisingizio cha free market, kama ni free market kwanini mbolea ipo subsidized, je hiyo subsidy siyi kodi ya raia ambaye anatakiwa kupewa bei ya chakula inayoendana na kipato chake? Wanelezaje kuhusu externalities ambazo zipo kwenye kilimo chetu ambacho hakiko commercialized? Hiyo siyo induced scarcity kwakua yeye alishindwa kulinda externals kuchukua domestic food bila kuzingatia chakula ni security kwakua raia wenye njaa ni rahisi kuwa blackmailed?
Yale majibu ya Mh. Waziri sijui alishauriwa na experts wa nchi gani!
 
Kwa kweli ubunifu hauna kikomo. .
😅😅😅
Zile akili za Bashe alizokuwa nazo zimeishia wapi?
 
Uwezo wako wa kufikiri ndipo ulipoishia hapo kwenye ukabila.

Roho mbaya haitakufikisha popote
Sasa ukabila unatoka wapi!!?

Sinkweli kule hawalimi!!?

Roho MBAYA ipi Sasa kwani nimesema wanyimwe chakula!?nimesema waziri anajua kuwa akisitisha kwa tufani ya njaa ijayo nduguze watapata shida kwani shida iko wapi hapo!!?
 
Bidhaa ili zipungue bei maana yake uzalishaji uwe mkubwa na ununuaji uwe wa haraka... hii inasaidia mzunguko wa pesa kuwa mkubwa hata kama profit margin ni ndogo ila niwaharaka faida inaonekana.
Uzalishaji ukiwa mdogo na purchasing power (uwezo wa kununua) ukawa ndogo maana yake kwanza bidhaa zinapatikana kwa bei kubwa na chache na utokaji wake niwa taratibu hivyo muuzaji analazimika kupandisha bei pia kufidia muda ambao bidhaa hazitoki... ukumbuke kwake maisha yanaendelea kama ni kula na other essential needs zinaendelea bila yeye kuingiza kwa haraka. Kwenye uchumi tunaita... Price elasticity of supply.
 
Watakuja na hoja za kufunga mipak ni kuharibu soko [emoji23].
 
Jukumu la Serikali. Ni kulinda. Raia wake.

Ila kama serikali inaruhusu raia wa kigeni kununua chakula kiholela toka kwa wakulima moja kwa moja na kusababisha mfumuko wa bei inakua imefeli.

Haya ndio matatizo ya kuwapa mamlaka watu ambao sio wa asili yetu hawana uchungu wa nchi hata ikiharibika.
 
Naomba kujuzwa je taifa letu limeshatangaza habari za njaa au kilichopo ni bei za bidhaa za nafaka kupanda?, wakurungwa kilio kimekuwa kikubwa sasa, liangaliwe kwa macho manne!
 
Kwa taarifa zisizo rasmi PM amekalia kuti kavu mbele ya bi mkola yupo tu muda usogee aangalie issue zingine... kuna viwaziri vinanguvu kwa mama kuliko hata PM mara 1000. Vikijikombakomba vinawekwa mgongoni na kupulizwa taratibu... simsemi kwa ubaya bi hindu ila hana courage i mean sio shupavu kwenye kusimamia maamuzi mazito sio kwamba hawezi tu ila hana huo ujasiri ni mtu laini... she is too mother instead of leader... ndio alivyo mpole anaetaka kuwapet pet watoto wake maisha yaende. Anaumia lakini hataki kukuumiza pia na nchi inakuwa ya kipuuzi ukiwa legelege. Atakaejaribu kusimama kukemea anaoneka ame under rate maamuzi ya mkuu wake kwa hiyo inabidi wacheze kwenye bit moja kuweka maisha rahisi kwao. Bi mkola hana maamuzi kwenye mambo ya msingi ila ukimkosoa anahisi unamdharau haraka sana anakuzimisha.. ndio wasiojiamini walivyo.
 
Swala hili halina suluhu ya muda mfupi, suluhu ya uhakika ni kutengeneza mifumo ya kilimo cha umwagiliaji ambayo itachukua muda na gharama
mbona wananchi wamepata suluhu,au ni wabunifu kuliko serikali yenye nyenzo zote muhimu?
Basi serikali iweke utaratibu wa kuwasikiliza wananchi
 
Sasa ukabila unatoka wapi!!?

Sinkweli kule hawalimi!!?

Roho MBAYA ipi Sasa kwani nimesema wanyimwe chakula!?nimesema waziri anajua kuwa akisitisha kwa tufani ya njaa ijayo nduguze watapata shida kwani shida iko wapi hapo!!?
Ukabila wa kumuunganisha Bashe na Wasomali kwa vile tu asili ya wazee wake ni huko, na wewe tayari umeshamhukumu kwamba atapindisha sera za nchi ili asaidie wasomali.

Hata kama hao wasomali hawalimi lakini nani alikwambia wanategemea chakula kutoka Tanzania?
 
Viongozi wamefikia pahala wanawafanya wananchi kama ''rubber stamp''
Kauli kama hizi za mtake msitake tutaunda dola,uku unapita mitaani kuomba kura maana yake nini?
Kauli ya kusema, hivi kuna mtu kama ..... 2025?
Wakati tunasubiri ifikapo 2024 kuona watu wanapita mtaa kwa mtaa kuomba kura ,maana yake nini?
Kauli kama hizi za uzandiki,hata ungekuwa wewe ndo mwenyezi Mungu ungefunga mvua ili uone kama wenye maneno hayo wataleta mvua ya kwao. Na tukileta jeuri ya kusema tutamwagilia na vyanzo vya maji vitakauka.
 
Ukisoma vitabu vya imani utaona watawala walipoenda kinyume na maagizo ya Mungu katika kutawala,Mungu aliwaadhibu kwa kufunga mbingu zisilete mvua,na magonjwa kama tauni n.k
habari ya kusema ni tabia nchi,kwani zamani za shibe tabia nchi ilikuwa imeenda likizo?
Ni muda wa kuitisha maombi ya kitaifa Mungu atunusuru na zahama hizi.
Tutasema ni vita ya urusi na ukraine,je ni kweli na unga wa muhogo ulitoka ukraine
 
Huyu mchizi anapata wapi moral authority au audacity yakuongea?
The beauty of hatred is contagious, even if you are told to bring evidence of the badness of the one you hate, you keep saying I heard...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…