Basi Kampuni ya Baraka kutoka Newala - Dar lapata ajali na kusababisha vifo 14
Shida pia ipo kwa wale vijana Wahuni wanaosimamaga mabarabarani kushangilia haya mabasi,kwa kweli huwapa vichwa Madereva kuendesha mabasi kwa spidi kubwa,ningekuwa IGP ningetoa oda wale wahuni wawe wanakamatwa na kuwekwa Mahabusu. Ni aibu sana unakuta jitu zima linakesha mabarabarani kushangilia mabasi sijui kumwagia maji,huwa nakereka sana
 
Huyo koplo kajikosesha nyota kwa haraka zake scenario kama hiyo umepona na upo ndani ya gwanda ukasaidia uokoaji wa majeruhi na kutoa maiti unakosaje kupata salute kwa kikosi chako
Nakazia,

Hata kwenye ajali ya treni ile ya dodoma kuna msojaa aliruka na mtoto ololoyayee naamini kila mtu anarohoyake
 
Pole kwa majeruhi na familia za wahusika.
Tuache uchunguzi ufanyike, nyum ya hizo ajali kuna mengi japo Hakuna uchunguzi umewahi kusema kuwa tajiri alitoa kafara au alitaka alipwe na bima basi lingine>
200% correct. Lakini pia tukumbuke ni mwisho wa mwaka
 
Shida pia ipo kwa wale vijana Wahuni wanaosimamaga mabarabarani kushangilia haya mabasi,kwa kweli huwapa vichwa Madereva kuendesha mabasi kwa spidi kubwa,ningekuwa IGP ningetoa oda wale wahuni wawe wanakamatwa na kuwekwa Mahabusu. Ni aibu sana unakuta jitu zima linakesha mabarabarani kushangilia mabasi sijui kumwagia maji,huwa nakereka sana
Hao ni jobless ambao wametengenezwa na mfumo, ndio kazi iliyobaki kwao.
 
Duu aisee yaani kama muvi vile,Mungu awarehamu kwa kweli
Shida pia ipo kwa wale vijana Wahuni wanaosimamaga mabarabarani kushangilia haya mabasi,kwa kweli huwapa vichwa Madereva kuendesha mabasi kwa spidi kubwa,ningekuwa IGP ningetoa oda wale wahuni wawe wanakamatwa na kuwekwa Mahabusu. Ni aibu sana unakuta jitu zima linakesha mabarabarani kushangilia mabasi sijui kumwagia maji,huwa nakereka sana
Aise wale wanakera sana

Ova
 
Hiyo Ajali nikiitathmini.. Kama Bus la Allys lilikuwa Speed na kugongwa ubavuni kwanini limeanguka MITA chache karibu na RELI? em tushirikiane kdg kutathmini hii scenario.

Gari ipo let's say 100kph inagongwa ubavuni inaanguka mita chache karibu na reli? Kuna Maajabu mengi.
 
Ajali imetokea kijiji cha Mtama majira ya saa 2 asubuhi, gari ilifeli breki ikiwa inateremka mlima Kinolombedo kabla ya kuufikia huo mteremko gari ilikuwa kasi sana kiasi wananchi wa vijiji jirani wakawa wanajiuliza mbona baraka inatembea kama inaendeshwa na wezi.

Ilipofeli breki pale mteremkoni, konda aliamriwa kushuka na kukimbia kutupa mawe barabarani ili gari isimame lakini gari haikuweza kusimama wala kupunguza mwendo, ilipasua hayo mawe na ikaendelea kushuka kwa mwendo mkali, dereva akamuamuru Konda wa kike ambae alibaki ndani aende nyuma kabisa ya gari kwa sababu alishahisi gari inaweza kupata ajali.

Baada ya kumaliza mteremko gari ilifika eneo la Kona kali mbili (Kona ya Nyale), dereva alifanikiwa kuimaliza kona ya kwanza, alipoianza kona ya pili gari ikachepuka ikaingia kwenye karavati, kutokana na ilishafeli breki na iko kasi ilidunda tu kwenye ule mfereji wa karavati na ikarudi tena barabarani na ilivyofikia pale kwenye karavati ikatimua mzinga wa nyuki kwahiyo fungu la nyuki likaingia ndani ya gari, taharuki ikawa kubwa, wakati huo gari imechomoka kwenye karavati ipo barabarani imeinama inatembea kwa matairi ya upande mmoja.

Gari inatembea kwa taili za upande mmoja + Nyuki wanawashambulia Presha ya abiria ikawa kubwa wakaanza kutaka kuruka kupitia madirisha, wengi wakawa wapo madirishani wameshatokeza vichwa nje kwa kuruka, ile gari kutokana na ilitembea kwa taili za upande mmoja kwa sekunde kadhaa na watu walishajaa madirishani kutaka kuchomoka ikadondoka kwa upande kwa bahati mbaya zaidi upande wa chini ulipofikia gari barabarani ndio upande watu walitaka kutokea, gari iliburuza ule ubavu ikiwa barabarani kipande kama cha mita 15 (kwa makadirio) mpka ikatoka barabarani ma kufika pembeni, Watu wakawa wameshasagwa vichwa na viungo vingine, barabara ilitapakaa maini, mautumbo, umeshuhudiwa moyo wa mtu unadunda kwenye nyasi, kuna maiti fulani ilikatika kiunoni vipande viwili, Rasta man mmoja alichinjwa shingo yake, dada mmoja alisafiri nae akabeba kichwa cha rasta kukileta kwenye ambulance. Waliosafiri pamoja ikitokea mmoja amepona anatafuta maiti ya mwenzake kwa kuangalia nguo aliovaa sio sura au mwili.

Usaidizi na utoaji abiria nje ulikuwa mgumu kutokana na nyuki ambao walijaa ndani ya gari wakifanya mashambulizi, wakazi walijitahidi kuwatoa abiria kwenye gari wakiwa maiti ma wengine majeruhi, pia majeruhi wengine ni wakazi wa mtama ambao wamenga'atwa na nyuki kwa kiasi kikubwa mpka wakazidiwa, Ambulance 2 na gari ya Polisi Mtama zilitumika kukimbiza majeruhi hospitali.

Ajali imeua pia mkazi mmoja wa mtama ambae ni mzee akienda shamba akiwa kwenye baiskeli yake, gari ilivyoanguka ilimkusanya na yeye.

Maiti 5 zilichelewa sana kutolewa kutokana na zilikandamizwa chini na gar, na kati ya hizo mbili ziliunganishwa Kama mshikaki na chuma kwahiyo kukata kile chuma ilikuwa ni kazi ya masaa, sijui walitolewa saa ngapi lakini mpaka saa 7 bado ngoma ilikuwa ngumu.

Braza mwanajeshi ambae ulichomoka kwenye ajali na ukutaka kukaa hata dakika 10 ukidai unawahi kuripoti kambini Zanzibar natumai umefika salama.

Ajali ya Baraka pale Mtama ni mbaya sana. Mungu awarehemu wote waliotangulia mbele za haki ma awaponye majeruhi wote waweze kurudi kwenye majukumu yao kwa haraka.
Habari ya kusikitisha sana. Umeileta kwa simulizi mwanana iliyoongezwa chumvi nyingi kwenye chai...

Wapumzike kwa amani watanzana wenzenu na majeruhi Mungu awafanyie wepesi wapate kupona mapema....
 
Umeona sasa, kwanini nasema KOSA ni la DEREVA? kwahiyo gari mbovu wewe kama Dereva unaendesha hivyo hivyo kisa BOSS?

Moja ya Majukumu ya Dereva ni kuhakikisha Chombo kipo salama, Abiria, na Yeye Mwenyewe pia na watumiaji wengine.

Ndio maana huku ktk Sekta ya Anga, kabla ya kutake off kuna Pre flight checks ambazo zinaambatana na Briefing after kufanya Airworthiness inspection. Na kama PIC siwezi kuanza/kuboard kama chombo kina shida, safety first.

Aende MAHAKAMANI alafu ajitetee et Boss alisema niendeshe hivyo hivyo.. utaenda kumpelekea Mikate na Soda.
Unaleta habari za ndege kwenye makampuni uchwara ya mabasi ya kibongo. Hivi unajua pressure wanayopewa madereva wewe? Unajua ni watu wangapi wanatafuta nafasi za kazi udereva?

Jumatatu tumetoka Arusha na Kilimanjaro, dereva tangu anaanza safari ana speed ndogo sana mpaka tunashangaa. Njiani kasimama mara mbili ananyoosha miguu na kufanya mazoezi, imagine!

Tumefika Mombo akashindwa kuendelea, mguu mmoja umekufa ganzi anatembea kwa shida. Akachukua simu ampigie mke wake kumbe hata kuona kwenye simu haoni muda huo ina maana kwenye gari hakuwa anaona vizuri. Kupewa huduma ya kwanza akajulikana BP imepanda.
Tukasubiri dereva mwingine ndio aje Mombo mpaka kuja kufika Dar ni saa saba usiku wakati Arusha tumetoka saa mbili asubuhi.

Dereva kama huyo alijua hayuko vizuri kiafya. Ila unaanzaje kuiambia kampuni yenye dereva mmoja kwenye basi, na hakuna dereva wa ziada kituo chao kikubwa kama Arusha kwamba sijisikii vizuri siendeshi. Watu wamekaa kwenye seats tajiri asikie eti dereva haendeshi "anajisikia vibaya" huyo dereva ana kazi?

Hizo haki za mfanyakazi huku kwenye transportation hamna. Hapo hatujasema madereva wa malori ya masafa marefu uko ndio kuna majanga zaidi.
 
T14 Armata bora na wewe useme huyu dogo Gentlemen_ analeta ujuaji kwenye kazi za watu. kaja mjini juzi shemeji yake kamfundisha gari wiki mbili tu tayari na yeye anajiona dereva anakuja kuandika uharo hapa.
 
Sikia Kijana..

Ndio maana kuna vyama vya WAFANYAKAZI kuna Vyamq vya Madereva.. kuna haki za wafanyakazi.

Usitetee ujinga.

Huyo angesababisha ajali kwa sababu ya kitu kinachoitwa HUMAN FACTOR.. ambayo moja ya kipengele chake ni Fatigue.. pia na visio-acute.

Kwa nature ya ajali ya BARAKA ni ubovu wa Chombo na sio shida ya dereva kuumwa, kingine DEREVA anaejielewa hawezi kurisk maisha yake kwasababu ya kazi/Boss.

Yaani kivyovyote usiingize upumbavu wa Boss atanifanya hivi au vile kisa nimefatq kanuni za udereva na Usalama barabarani. Hakuna excuses ktk maisha ya watu.
 
Umeongea/umesema maneno mazuri/ya busara kwa kutoa ushauri/maoni juu ya tukio/ajali iliyotokea asubuhi/alfajiri ilihusisha treni/kichwa cha treni na basi/gari la abiria na kupelekea majeruhi/vifo ambamo wameumia/kuvunjika na wengine kufa/kufariki katika hii/hiyo ajali ambayo imeleta huzuni/masikitiko katika jamii hususani/mahususi
Upewe maua/majani yako bibie/babue
Hahahahaha,naona umeamua kuendana na ujinga wake
 
T14 Armata bora na wewe useme huyu dogo Gentlemen_ analeta ujuaji kwenye kazi za watu. kaja mjini juzi shemeji yake kamfundisha gari wiki mbili tu tayari na yeye anajiona dereva anakuja kuandika uharo hapa.
Amekwambia kwenye ndege kuna briefings na pre flight check. Anadhani ndege na Super Feo vyote sawasawa kwenye ufuatiliaji na ukaguzi.
 
Sikia Kijana..

Ndio maana kuna vyama vya WAFANYAKAZI kuna Vyamq vya Madereva.. kuna haki za wafanyakazi.
Lini uliwahi sikia vyama vya wafanyakazi na madereva vinamtetea dereva. Tuanze na malipo yao ya umbali huwa wanalipwa hata nusu yake?

Wana bima?

Wanapumzishwa?

Wanapewa likizo?

Wote wanalipiwa mifuko ya hifadhi jamii?

Usitetee ujinga.
Wewe ndio unaleta ujinga kwa kulaumu madereva sehemu ya kulaumu LATRA, mamlaka za usalama barabarani, vyombo vya sheria na wamiliki.
Huyo angesababisha ajali kwa sababu ya kitu kinachoitwa HUMAN FACTOR.. ambayo moja ya kipengele chake ni Fatigue.. pia na visio-acute.
Hakuwa na fatigue, alikuwa na BP kwa mara ya kwanza na hakuwa anajijua. Kituoni hakuna vipimo, najua na hapa utamlaumu dereva kwanini hana personal physician au kwanini hana vifaa vya kujipima afya. Kaja kugundua ana pressure tukiwa Mombo.
Kwa nature ya ajali ya BARAKA ni ubovu wa Chombo na sio shida ya dereva kuumwa, kingine DEREVA anaejielewa hawezi kurisk maisha yake kwasababu ya kazi/Boss.
Dereva anayejielewa umpate Baraka? Yani huyu Baraka anayeokoteza madereva waliododa wasio na maisha ndio unatarajia apate madereva wanaojielewa na wasimamie sheria za barabarani? Bado hapo huoni uhusika wa mmiliki wa bus.
Yaani kivyovyote usiingize upumbavu wa Boss atanifanya hivi au vile kisa nimefatq kanuni za udereva na Usalama barabarani. Hakuna excuses ktk maisha ya watu.
Nani asimamie hiyo misingi. Ni hawa madereva ambao asipofanya kazi siku hiyo hali?
Na akifanya hivyo utajuaje. Maana ataondolewa yeye aletwe mwingine atakayefanya yaleyale yaliyokataliwa na huyo wa mwanzo so effect ni ileile.
 
Najibu hoja kama ifuatavyo.
Naomba usome kwa makini tafadhari.

Lini uliwahi sikia vyama vya wafanyakazi na madereva vinamtetea dereva. Tuanze na malipo yao ya umbali huwa wanalipwa hata nusu yake?

Wana bima?

Wanapumzishwa?

Wanapewa likizo?

Wote wanalipiwa mifuko ya hifadhi jamii?
1> Umetoka kwenye HOJA ya Msingi ya DEREVA ndie mwenye makosa na kugeukia upande wa MASLAHI Binafsi ya Dereva.

Hoja inabaki kuwa solid DEREVA hajapractice alichofundishwa DARASANI (Kitu kilichompa Leseni/Dhamana ya Kubeba Roho za Watu).
Wewe ndio unaleta ujinga kwa kulaumu madereva sehemu ya kulaumu LATRA, mamlaka za usalama barabarani, vyombo vya sheria na wamiliki.
2> naomba uniambie hapo... ktk hiyo ajali LATRA anakosa gani labda.

Hakuwa na fatigue, alikuwa na BP kwa mara ya kwanza na hakuwa anajijua. Kituoni hakuna vipimo, najua na hapa utamlaumu dereva kwanini hana personal physician au kwanini hana vifaa vya kujipima afya. Kaja kugundua ana pressure tukiwa Mombo.
3> Kitendo cha kuugua ni cha kawaida na inajulikana, tujikite ktk uchambuzi wa ajali ya BARAKA je Dereva wake alikuwa na BP pia?

Dereva anayejielewa umpate Baraka? Yani huyu Baraka anayeokoteza madereva waliododa wasio na maisha ndio unatarajia apate madereva wanaojielewa na wasimamie sheria za barabarani? Bado hapo huoni uhusika wa mmiliki wa bus.

4> UMEONA Akili yako ilivyo ndogo/fupi na unajua kwanini kuna muda nalazimika kutumia Lugha KALI/yenye MATUSI kwa watu kama dizaini yako?

Umesema mwenyewe MADEREVA wa kampuni ya Baraka:
1- Hawajielewi
2- Wamedoda
3- Wasio na Maisha
4- Hawawezi kusimamia Sheria za Barabara.

Mie nilisema kosa lipo kwa Dereva, ukanipinga ukaweka utetezi kwake, hapa ktk maelezo yako unaonyesha ni Weakness za DEREVA zq wazi kabisa.

(Naomba siku nyingine usikurupuke kujibu hoja za watu wenye akili timamu)

Aisee naona niishie hapa tu najichosha bure na kazi nyingi sana za msingi kuliko kuendesha mijadala ya kutumia akili na watu wasiokuwa nazo ni kujaza maji ktk tenga.
 
Amekwambia kwenye ndege kuna briefings na pre flight check. Anadhani ndege na Super Feo vyote sawasawa kwenye ufuatiliaji na ukaguzi.
Kitu ambacho hukijui uwe unanyamaza sometimes inakupunguzia kuonekana Mpumbavu hadharani.. inaheshimisha sana.

Operations za Airlines zote zimetoholewa ktk sekta ya Mabasi. Unayoyaona ktk Ndege basi yamechukuliwa ktk practices za mabasi.

1- Leseni
2- Pilot in Comand + First officers (Kwa mabus ndio kuna Dereva Mkuu na Msaidizi)
3- Flight attendants (Cabin Crew) ktk mabus wapo Bus attendants mfano yule Dada wa Tilisho..
4- Booking and kukata Ticket ni same kwa bus
5- Rules na regulations zinatofautiana kwa uchache sana.. mfano right of way rule ya Anga tofaut na right of way rule ya ardhini. But Same semantics.

6- Boarding procedures za Airlines zinafanana na za Bus kuna utofauti mdg sana baada ya Airlines kuongeza safety hasa ya kipengele cha Dangerous goods.

7- Flight plan same as kwa upande wa mabus kwa kias chake.. na lazima log books zijazwe etc..

8- Recording ya wasafiri wa Airlines zimetoholewa kwa mabus pia, ndio maana kuna ukaguzi wa abiria walio ktk vitabu na majina yao na details zao na zinakaguliwa na matrafic.

Na mataka taka mengine meengi.. sitamaliza kuandika hapa.

Kinachotenganisha ni jinsi GHARAMA zilivyo, SENSITIVITY, UHARAKA na USALAMA. hapo ndio kunaleta utofauti kiasi ila standards kwa 80% ni same.

Pata exposure ya pande mbili za hoja ndio ujitumbukize kujibu kwa kujiamini.

Nimefunga MJADALA na Wewe.
 
Back
Top Bottom