Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Habari ya mchana wakuu, niko hapa maeneo ya kariakoo kuna ajali imetokea gari ya mwendokasi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke imemgonga mtu na mwili kusagika hapo hapo, inasemekana huyu ni mtu wa tatu anagongwa na kufa hapo hapo na huyu mwanamke.

Mwenye maelezo zaidi kuhusu huyu mwanamke dereva wa mwendokasiatujuze.

====================

UFAFANUZI WA DART
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), William Gatambi:

Bodaboda alikuwa anakatisha Mtaa wa Mafia wakati Taa za Kijani zimeruhusu, akagongwa na Basi akapoteza Maisha palepale, baada ya tukio hilo baadhi ya waendesha Bodaboda wakaanza kuponda basi kwa mbele, wakavunja vioo.

Baada ya hapo wakamvamia Dereva wa Basi na kuanza kumpiga na kumuibia pochi yake. Baadaye Dereva ambaye aliongoza wenzake kushambulia basi na kumjeruhi Dereva amekamatwa na yupo Polisi.

Pia, Dereva naye yupo Polisi muda huu kwa ajili ya kutoa maelezo.
Lilikuwa linaona Taa haziruhusu lenyewe likajiona mjanja.

Bodaboda wafyekwe kwa namna hiyo hiyo maana yanaona barabara zote zao peke yao
 
Waweke vizuizi halafu magari yanayotoka upande A kwenda upande B yapite juu ama?
Bila shaka alikuwa na maana ya kuweka uzio pembeni ya barabara kwenye hayo maeneo.

Lilikuwa linaona Taa haziruhusu lenyewe likajiona mjanja.

Bodaboda wafyekwe kwa namna hiyo hiyo maana yanaona barabara zote zao peke yao
Uwe unasoma vizuri mkuu na kuelewa!
Nimesoma taarifa inasema aliyegongwa alikuwa sahihi maana taa zilimruhusu apite, ila gari la mwendokasi ndiyo likaja kumchota.
 
Hapana......

Nadhani sehemu za junction wataalamu watajua wanafanya nini ili kusudi kila watumiaji wa barabara wasiwe na bugdha....... takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwenye mavukio yasiyokuwa rasmi.......
Nadhani una maanisha hivì au mfano wa aina hii
images (13).jpeg
 
Lilikuwa linaona Taa haziruhusu lenyewe likajiona mjanja.

Bodaboda wafyekwe kwa namna hiyo hiyo maana yanaona barabara zote zao peke yao
Tuwe na ubinadamu kidogo, Nina hakika mtu wako wa karibu akiwa kwenye boda hutataka hii hukumu uliyoitoa iwe juu yake hatakama amefanya hilo kosa.
 
Hao bodaboda Mwenzao akigongwa hata kwa uzembe wake mwenyewe wao wanamshambulia Mwenye Gari.Vipi na wao wakigonga Mtu jamii iwadunde?Na huyo aliyekamatwa ndio awe mfano,ikiwezekana awataje walioshirikiana nao waungane nae.
 
Tuwe na ubinadamu kidogo, Nina hakika mtu wako wa karibu akiwa kwenye boda hutataka hii hukumu uliyoitoa iwe juu yake hatakama amefanya hilo kosa.
Kosa moja barabarani totally linagharimu maisha.

Yule dreva wa Costa ya wana kwaya alisinzia kidogo tu, angalia gharama ya matokeo ya kusinzia kwake kidogo.
 
Watasema billion 200 🤣
Huo mradi walipoufungua vitu kibao vilikuwa havijakamilika
Ila kwa sababu nchi kama ina laana ndy hivyo tena
Mpaka ndani ya vituo tu mabenchi yale ya kukaa hayajawekwa ya kutosha

Ova
 
Kosa moja barabarani totally linagharimu maisha.

Yule dreva wa Costa ya wana kwaya alisinzia kidogo tu, angalia gharama ya matokeo ya kusinzia kwake kidogo.
"Bodaboda wafyekwe kwa namna hiyo hiyo maana yanaona barabara zote zao peke yao"

Hii sentensi umeiongea baada ya boda kukanywagwa na basi na kufa hapo hapo.

Hapa unamaanisha wenye magari wawakanyage wafe. Ni sentensi iliyokosa ubinadamu mkuu. Isome tena utaona mistake.
 
Ajali zote za mwendokasi nilizoshuhudia ni kama vile hao madereva wanakuwa wana dhamiria kuua kabisa maana huwa wanakimbia sana hata sehemu ambazo zinaonekana kuwa ni hatarishi......

Kipande cha kutoka gerezani mpaka kufika kituo cha fire huwa ni mshike......mwenda kwa miguu unakuwa macho juu kama nguchiro.....huku mwendokasi kule boda boda waliochanganyikiwa.......hujakaa Sawa umegongana na mmachinga........

Mimi nadhani kuanzia pale gerezani waweke vizuizi mpaka fire.....na pia kuanzia fire mpaka kivukoni waweke vizuizi.........
Kuna siku nipo kwa daladala boda akajichanganya ku overtake bila tahadhari. Aiseee dele wa ile costa akamsogezea chuma ili akajibamize kwenye roli upande wa pili, kwa bahati akamkosa.

Jamaa akaanza kuongea bila aibu, “ana bahati sana, habari yake ingeishia hapa”.
 
waendesha mwendo kasi ni washenzi sana, walishanikosa mara chupu chupu, yoyote anaewatetea hajayaona.
 
Sehemu za kupita njia watu wameweka biashara, hizi huruma za kipuuzi eti watauzia wapi ndo zinamaliza maisha ya watu. Kariakoo kunaboa sana, biashara zimejazana hadi barabarani kanjia kadogo sana kwaajili ya watembea kwa miguu, hapo hatuongei kuhusu uchafu hii nchi watu wanapelekwa kimayai mayai sana
RIP mwamba aliyegongwa🙏
 
RIP mwamba🙏
Mwamba gani mkuu?
Maana Magufuli ndiyo aliwapa ruhusa waachinga wazae kila engo.
 
Back
Top Bottom