Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Ajali zote za mwendokasi nilizoshuhudia ni kama vile hao madereva wanakuwa wana dhamiria kuua kabisa maana huwa wanakimbia sana hata sehemu ambazo zinaonekana kuwa ni hatarishi......

Kipande cha kutoka gerezani mpaka kufika kituo cha fire huwa ni mshike......mwenda kwa miguu unakuwa macho juu kama nguchiro.....huku mwendokasi kule boda boda waliochanganyikiwa.......hujakaa Sawa umegongana na mmachinga........

Mimi nadhani kuanzia pale gerezani waweke vizuizi mpaka fire.....na pia kuanzia fire mpaka kivukoni waweke vizuizi.........
Boda boda ndio wapuuzi sana wao hawana cha mataa wala foleni, muda wote wanapenya halafu wabishi sana
 
Waweke vizuizi halafu magari yanayotoka upande A kwenda upande B yapite juu ama?
Hapana......

Nadhani sehemu za junction wataalamu watajua wanafanya nini ili kusudi kila watumiaji wa barabara wasiwe na bugdha....... takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwenye mavukio yasiyokuwa rasmi.......
 
Tatizo ni wale machinga waliojazana pembezoni mwa barabara halafu wanajiona wana haki kuliko watembea kww miguu,, nchi ya kifala hii
Hii nchi sijawahi ona. Wamachinga wanatakiwa waondolewe kwa lazima. Na serikali ipige marufuku bodaboda mjini. Nchi imejaa bodaboda wengi wenye akili visoda. Itafikia wakati mji wa Dar haupitiki kwa magari
 
Hii nchi sijawahi ona. Wamachinga wanatakiwa waondolewe kwa lazima. Na serikali ipige marufuku bodaboda mjini. Nchi imejaa bodaboda wengi wenye akili visoda. Itafikia wakati mji wa Dar haupitiki kwa magari
Mi kwasasa hata kariakoo naiogopa nikiwa na kitu cha kunipeleka huko napata mawazo sana napita wapi? Nitarudi salama? Je sitaibiwa, hapo bado kupigwa bei ya bidhaa,, aah yani huko imekuwa kama dampo,
 
Huyu ni mtu wa 3 anagongwana huyu mwanamama na kupoteza maisha.
Mwingine ni mwanamke amemgonga juzi maeneo haya haya.
Kwahiyo sina chuki na huyu mwanamke hata kidogo
Kwani hao anaowagonga wanakuwa wapi? Kama wanakuwa kwenye njia ya huyo dereva basi wao ndo wanamgoñga.
 
Habari ya mchana wakuu, niko hapa maeneo ya kariakoo kuna ajali imetokea gari ya mwendokasi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke imemgonga mtu na mwili kusagika hapo hapo, inasemekana huyu ni mtu wa tatu anagongwa na kufa hapo hapo na huyu mwanamke.

Mwenye maelezo zaidi kuhusu huyu mwanamke dereva wa mwendokasiatujuze.

====================

UFAFANUZI WA DART
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), William Gatambi:

Bodaboda alikuwa anakatisha Mtaa wa Mafia wakati Taa za Kijani zimeruhusu, akagongwa na Basi akapoteza Maisha palepale, baada ya tukio hilo baadhi ya waendesha Bodaboda wakaanza kuponda basi kwa mbele, wakavunja vioo.

Baada ya hapo wakamvamia Dereva wa Basi na kuanza kumpiga na kumuibia pochi yake. Baadaye Dereva ambaye aliongoza wenzake kushambulia basi na kumjeruhi Dereva amekamatwa na yupo Polisi.

Pia, Dereva naye yupo Polisi muda huu kwa ajili ya kutoa maelezo.
Safi sana,hao madereva mwendokasi hawanaga utu utadhani sio raia wa Tz,wangemuua tu nayeye ili iwe fundisho, kama kweli ashagonga raia watatu na kuua.
 
Back
Top Bottom