Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Watembea kwa miguu tujihadhari dadeki, huwa nashangaa mtu anavuka barabara kisa yupo kwenye zebra basi anatembea bila tahadhari yoyote kwa mwendo wa madoido yote.

Hawa madereva wetu ni kua na tahadhari muda wote, hata zile one way kuna boda vichaa huwa wanaenda uelekeo tofauti.
 
Wewe kila siku upo hapo hapo unamsubilia huyo mama agonge mtu

USSR
Kwani point yako ni ipi hapa mkuu?
Mimi nimeleta taarifa kwakuwa nimeishuhudia mbele yangu,
Hapo hapo kuna watu biashara na shughuli zao wanafanyia maeneo hayo ndiyo wametoa maelezo kwba huyu mama ni mtu wa tatu leo anagonga na kuua, mmoja ni somewhere huko kimara, wawili ndiyo kawagonga hapa Kariakoo
 
Kusema kweli kwa akili za boda boda wengi unaweza kuamini kabisa huenda marehemu kazingua,kwasababu kutokana na uzoefu wa matukio ambayo boda wanafanya mpaka unajiuliza hivi huwa wanawaza nini?

Hata Songea nimekuta mambo wanayofanya boda wa dar nao wanafanya hivyo hivyo,huwa sijui ukiwa na boda huwa unajikuta wewe ni nani

Lakini upande wa pili,madereva nao wa mwendo kasi wana shida nao,sijui kile kitendo cha kujijua wanaendesha mwendo na wana barabara zao naona wanajikuta kama wanaendesha treni kwa maana hata wakogonga mtu maadamu wapo katika road yao basi wewe ndio umewagonga wao

Kwasababu kutokana na uzoefu wa ajali za mwendokasi na boda ingetosha kabisa wangebadili namna ya uendeshaji wao katika maeneo ya pilikapilika kama hayo

Yani hili nalo linahitaji katiba mpya?
 
Watu hamsomi maelezo vizuri mnakurupuka tu kujibu.
Huyo dereva wa boda aliegongwa alikua anavuka makutano ya nataka,taa ziliruhusu upande wake kuvuka..mwendokasi sababu ya sababu ya kuwa rafu na kutotii Sheria kamgonga na kumuua huyo jamaa.
Na hapo naona alijiamini hata akimgonga hakuna atachofanywa maana imezoeleka boda ndo wabaya barabarani.
Makutano hata mbabsi ya mwendokasi yana taa nyekundu wasimame kupisha wengine.kwenye zebra wasimame kupisha wapita njia.kwenye makutano wasimame kupisha upande mwingine uvuke.kama upande wao umewaka nyekundu
So kama anaua na kujikita mwamba ana haki ya kupelekwa moto.huyu anaweza ua hata ndugu yako kesho.
 
Boda huwa hawana subira kabisa aisee. Kujichomeka chomeka tu wanapasuka kama hivi.
 
Tatizo ni wale machinga waliojazana pembezoni mwa barabara halafu wanajiona wana haki kuliko watembea kww miguu,, nchi ya kifala hii
Anatakiw kichaa mmoja aje aweke utaratibu wa kuwanyoosha. Kwanza wanawazibia rizik wenye frem.. hiki kilio lilikuw cha siku nyingi.
 
Hapana nakupinga. Watu waheshimu sheria za barabara. Huwa najiuliza traffic hawaruhusiwi kuwakamata watembea kwa miguu wanaovunja sheria? Watembea kwa miguu nao wanavunja sheria mno. Huko Kkoo watu hawayaogopi magari kabisa.
Sasa sijui umenipinga au umekubaliana na mimi?
 
Anatakiw kichaa mmoja aje aweke utaratibu wa kuwanyoosha. Kwanza wanawazibia rizik wenye frem.. hiki kilio lilikuw cha siku nyingi.
Ni kero kubwa mno, kuongeza msongamano usio wa lazima, wizi, kelele, bei kubwa ya bidhaa, kukosekana utulivu, mtu kuingia kufanya manunuzi unawaza km unaenda vitani vile
 
Ajali zote za mwendokasi nilizoshuhudia ni kama vile hao madereva wanakuwa wana dhamiria kuua kabisa maana huwa wanakimbia sana hata sehemu ambazo zinaonekana kuwa ni hatarishi......

Kipande cha kutoka gerezani mpaka kufika kituo cha fire huwa ni mshike......mwenda kwa miguu unakuwa macho juu kama nguchiro.....huku mwendokasi kule boda boda waliochanganyikiwa.......hujakaa Sawa umegongana na mmachinga........

Mimi nadhani kuanzia pale gerezani waweke vizuizi mpaka fire.....na pia kuanzia fire mpaka kivukoni waweke vizuizi.........
Waweke vizuizi halafu magari yanayotoka upande A kwenda upande B yapite juu ama?
 
Back
Top Bottom