BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua

Kwa hiyo hao Sahara ndio wasemaji wa BBC? Kwanini BBC wasiseme wenyewe kama wenyewe?
Hao sahara wameripoti kama nilivyoripoti mimi.... Lakini BBc wameshaachilia teaser ya video..... Au ujaiona hapo, au unakaza Fuvu
 
Hivi kweli mtu unapokea muujiza wa pesa kwenye MPESA na hujiulizi?
 
Ripoti inahuzunisha sana. Wamehojiwa wadada wazuri waliokuwa wanananiliu na nabii kwa kulazimishwa na wakipata mimba zinatolewa. Inadaiwa mwingine alitolewa mimba 5. Halafu ni kama walikuwa kizuizini wanajaribu kutoroka lakini wapi. Kwa upande wa miujiza fake hata hapa bongo ipo kwa baadhi ya watumishi ambao hawataki kumtafuta Bwana na nguvu zake.
 
Gwajima yuko hai na anadai anafufua wafu. mbona wagalatia bado wanajaa kanisani kwake na kutoa fungu la 10 kwa huyo tapeli?

Heri ya mwaka mpya mkongwe...

Upo sahihi, lakini habari kama hizi zingekuwa na mashiko zaidi endapo zingetolewa kipindi muhusika akiwa hai naye tusikie utetezi wake...

Pamoja na kwamba SCOAN imepoteza ule umaarufu wake, kuzitoa habari hizi kwa sasa tutakuwa na maelezo ya upande mmoja tu...
 
Dini Iliyo Safi isiyo na taka Mbele Za Mungu Baba Ni kwenda kusaidia yatima viwete katika dhiki Yao YAKOBO 1:27

KWA MAANA KRISTO ALIFANYIKA MSAADA IMETUPASA KUSAIDIANA SISI KWA SISI KATIKA DHIKI ZETU NA KUPENDANA.
 
Umeandika ushuzi wa hali ya juu dogo. Tuliza kijambio hiko. πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜πŸ˜†πŸ˜…
I'm pretty sure you're one of those scatterbrains who've been heavily indoctrinated with religious teachings from the so called prophet and here you're trying to defend his irrational beliefs and moral misdeeds. Shame on you. Jinga kabisa. Na ulivyo mjinga unadhani hapa JF wote ni watoto.
 
Hatuna budi kuwa wafuasi wa Yesu Kristo, si wanadamu na dini zao hata kama ni za kikristo. Kamwe tusiwe wafuasi wao hata kama wana majina makubwa mno ya kidini na miujiza mingi, kwa kuwa Mchungaji Mwema ni Yesu pekee. Yesu tu atosha, wengine futilia mbali kabisa!
 
Mbona BBC wanachokonoa RC na ushoga kwa kuanika makasisi wao?
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini wamesubiri kuitoa wakati ameshafariki
Walikamilisha lini uchunguzi wao?
Fuatilia kisa cha Jimmy Savile utanue ubongo wako.
 
Inategemea wamepata habari lini. Kuna vitu/siri nyingine hujulikana baada ya mtu kufariki. Mimi huyu hata kabla hajafariki nilishajua ni mwongo. Kuna siku aliponya mtu kasema am,etoka Tanzania huku anazungumza ikiingereza kila cha ki-nigeria
Sahihi, kuna visa vingi sana duniani kama vya Jimmy Savile
 
Kwa babu wa kikombe yumoo.

Kwa TB Joshua yumoo.

Jamaa alikuwa na akili ya kuchotwa kirahisi sana huyu.
Aliahidi kumjengea barabara mzee wa Upako ya kwenda kanisani kwake!
 
Inayoitwa dini ya Kikristo ni Utapeli.
 
T
Tuliza kichwa. Unajua lengo la kuanzishwa kwa BBC? Fuatilia kisha uje tena hapa utuambie kama wanachofanya ni tofauti na lengo lao.

Kimsingi Waafrika tuamke!! Tuache kubabaikia vyombo vya Propaganda za wazungu kwa Waafrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…