BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua

Breaking News: BBC inatazamia kuchapisha nakala ya uchunguzi wa kuacha vinywa wazi inayoeleza matukio ya kikatili, Miujiza ya Kughushi, uhalifu, na ubakaji uliofanywa na Marehemu Mchungaji Temitope Balogun Joshua, almaarufu Nabii TB Joshua!!!

Kupitia page ya twitter ya Sahara Reporters wameelezea matukio aliyofanya ambayo yanatarajiwa kupostiwa na BBC katika video
View attachment 2864719

Tizama kipande hiki cha BBC wakihoji watu waliokumbwa na unabii feki wa TB Joshua....
Hii inashangaza!!! 😱🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️💨

📺 Video Credit: BBC
View attachment 2864718

TB Joshua alikuwa ni mchungaji maarufu wa Kikristo na mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos, Nigeria. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na alihusika katika huduma za kiroho, uponyaji, na mafundisho ya Biblia. Hata hivyo, alifariki dunia mnamo Juni 2021.
Kwa hiyo hao Sahara ndio wasemaji wa BBC? Kwanini BBC wasiseme wenyewe kama wenyewe?
 
Sasa wafuate na hawa wahuni uku Tanzania wanaopotosha jamii haswa wanawake, akina mwakasege,mwamposa,gwajima,kakobe,mzee wa upako, akina masanja na mashekhe wote wawekwe wazi uhuni wao
 
Unauita unabii feki, unataka kusema BBC wanaleta unaa kwa TB Joshua?
 
Hivi yule sheikh mnajimu aliyekuwa anarundika waandishi pale nyumbani kwake magomeni jijini dar akitabiri mambo mazito yatakayotokea nchini/duniani utabiri wake ulikuwa sahihi kwa kiwango gani? Unafiki uachwe, abrakadabra ziko nyingi kwenye dini zote zilizoshika mentality za watu. Kuna dini zinaonekana zina waumini wengi na majengo makubwa yenye minara, tena waumini wake wakijinasibu wanamuabudu mungu wa kweli na dini yao ni ya haki kumbe ni abrakadabra zilezile tu za kina TB Joshua. BBC wasijitie wazimu kuchokonoa dini na imani za watu wakifikiri kuna dini mambo yake ni ya kweli halafu huko ikaacha kuchokonoa kwa kuhofia kuleta fujo duniani. Kuna dini duniani ni ya ajabu sana na imeteka fikra za watu wengi kwa mafundisho yake yasiyokuwa na uhakika, imekuwa kama ni mfumo tu wa kisiasa. BBC waache unafiki kuchokonoa dini/imani za watu wakati kuna dini nyingi tu wengine hawaziamini na maisha yanakwenda kama kawaida. Kuna dini ilichapishiwa mpaka kitabu kuonesha ushetani wake bado watu wanaiamini
 
Breaking News: BBC inatazamia kuchapisha nakala ya uchunguzi wa kuacha vinywa wazi inayoeleza matukio ya kikatili, Miujiza ya Kughushi, uhalifu, na ubakaji uliofanywa na Marehemu Mchungaji Temitope Balogun Joshua, almaarufu Nabii TB Joshua!!!

Kupitia page ya twitter ya Sahara Reporters wameelezea matukio aliyofanya ambayo yanatarajiwa kupostiwa na BBC katika video
View attachment 2864719

Tizama kipande hiki cha BBC wakihoji watu waliokumbwa na unabii feki wa TB Joshua....
Hii inashangaza!!! 😱🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️💨

📺 Video Credit: BBC
View attachment 2864718

TB Joshua alikuwa ni mchungaji maarufu wa Kikristo na mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos, Nigeria. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na alihusika katika huduma za kiroho, uponyaji, na mafundisho ya Biblia. Hata hivyo, alifariki dunia mnamo Juni 2021.

Tukiwaambia Mwamposa naye muhuni tu, hamuwezi amini
 
BBC waache unafiki, abrakadabra ziko nyingi hata kwenye dini zenye watu wengi, mbona huko hawachokonoi? Akina Rushdie walithubutu kuchimbua ushetani ulioko kwenye dini fulani kubwa duniani wakaishia kutangaziwa kifo popote walipo na juzijuzi huyo mwandishi wa kitabu hicho nusura wapoteze maisha yake huko alikokimbilia tangu miaka mingi. BBC wanaona hakuna madhara watayopata toka kwa wafuasi wa TB Joshua na yeye hayupo duniani kuwajibu ndio wanajitia wazimu kuchokonoa imani hiyo. Hebu wajaribu kuchokonoa ile imani ya dini ile machachari kama wataacha kuona rangi zote. Kila dini ina abrakadabra zake na watu wanaamini
 
Hii sio imani, huyu ni mtu, ficha upumbavu wako, aliyokuwa anafanya hayahusiani na yaliyoandikwa kwenye Biblia.
 
sijawahi kuwa mfuasi wa tb joshua na wala kuamini miujiza yake sambamba na wengine wa aina yake waliopo hapa nchini. Fahamu kuwa hata huko unakoamini/kuabudu mungu wako/dini yako ni abrakadabra tu inayotakiwa kuwekwa wazi na sio akina tb joshua tu
 
I respect your opinion Kaka
 
Naandika tena, BBC ni wanafiki, abrakadabra ni nyingi hata kwenye dini kubwa zinazoheshimika ni za kweli. Halafu mbona wafananao na TB Joshua ni wengi huko kwa nini hawatoi documentary, au wanasubiri wafe ndio watoe?
 
Sijui sababu kwa kweli, labda kuna legal issues, ila hauoni hii pengine itawasaidia watu kutafakari????? Better something
 
Back
Top Bottom