Bila kumsikia Martha mwenyewe haya ni majungu Tu.
Halafu niwaambie kama huna msimamo ndugu wanakupanda kichwani ,unaweza kuta nusu ya pesa zako zinaishia Kwa ndugu ,na ndugu shida haziishi.
Halafu hawa wazazi baadhi huwa hawaridhiki yaani kwakuwa alikuzaa na Una kipato basi anahisi kila kitu chako ni chake.
Nashukuru wazazi wangu wote wawili siyo ving'ang'anizi yaani , kwanza hata kama wanashida huwa wanaomba Kwa aibu mno.ni Mimi tu nitambue mahitaji Yao.
Lakini kuna familia ukiwa nacho watataka uwalipe Mshahara,tena kama mama hajielewi ndiyo Kwanza atakusagia kunguni