Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Nimeshangaa sana huyo jamaa kuwasema wadada. Wengi sio wachoyo na wanatunza wazazi wao. watakuwepo ambao sio wema lakini ni wachache.
Actually watoto wa kike siku hizi ndiyo wanajali sana wazee wao kuliko hata wa kiume. Na hii haijalishi kama hao wazazi wana pesa ama la! Nina mifano mingi sana.

Mabinti mna mioyo mizuri sana; na kama mzazi ulikuwa mwema kwao na wakaona jinsi ulivyokuwa unampenda mama yao, wala hawana figisu kabisa. Daughters are the best!
 
Hizi ndio harakati za mtu mweusi
Naam!

Na watu wanachukulia kusaidiwa kama ni haki yao. Halafu sasa hawana shukrani. Unaweza kabisa jitu ukalisomeshea watoto wa lenyewe na kulifanyia kila kitu lakini siku ukiacha tu jiandae kuchukiwa na kusemwa sana. Ndiyo maana wengine hatutaki kabisa kusikia mambo ya ndugu. Wanaweza kukukwamisha pakubwa usipojiangalia.

Harakati za mtu mweusi indeed!
 
Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake akidai kuwa Martha Mwaipaja ana fedha nyingi sana lakini hamsaidii mama yake vilevile akidai kuwa amejitenga na ndugu zake

Tazama Video hizi kwa utulivu
Kumbe ni imani ya mambo ya "mapepo"? Simlaumu kwa kujitenga nao.

Amandla...
 
Nachojua huyo Dada ana abudu katika Giza sio pesa tu anatembelea latest cars .

Ukienda Mbezi Kwa zena anakopanga Simba la masimba utamkuta trip hazikauki .

Inshort huyo anayelalamika aachane na hayo mambo ya kulalamika hizi pesa asione watu wanazo

Kuna hidden sacrifices ambazo sio kila MTU anaweza kufanya .
Ahsante kwa uchangia!
 
Nimeshangaa sana, ninapokuwa na dada zangu hupenda kugharimia kila kinachohitajika, ukitoa pesa unaambiwa rudisha mfukoni, sisi tutafanya!! Nimeshangaa mwenzangu dada zake wachoyo!!
Kuna situation moja niliishangaa sana, dada alikuja na shemeji, wakiwa pamoja wakanipa pesa, baadaye kila mmoja kwa upekee akanipa pesa, kwa kweli sikuelewa maana yake.
Wadada wengi wapo hivyo. Ukikuta ni mchoyo basi amerogwa kama dada yetu Martha Mwaipaja😀
 
Tatizo ni hao wanaojidai kumtoa mapepo na hawana uwezo huo
Wachungaji sio Waganga wa Kienyeji.....! Wala Mungu hafanyi kazi Kwa namna ya Kibinadamu...!

Yesu alipokua akiponya Watu... aliwaambia nenda ila USITENDE DHAMBI TENA...!

Sijui kama unaelewa maana ya maneno hayo, na Biblia inasema Mapepo yanapomtoka Mtu, huenda kutangatanga na yakikosa pa Kukaa, hujaribu kurudi kwa Mtu yule yule, yakikuta Mtu yupo Msafi hayawezi kuingia Tena, ila yakikuta Mtu Yuko mchafu, yanaiingia yakiwa na Nguvu mara 7.

Kanuni za Mungu zipo wazi Ndugu, Sasa unakuta Mtu ana Mapepo kaombewa Mapepo yameondoka, anarudi kwake, kumbe anaishi na Mwanaume hajafunga nae Ndoa, ama anaishi na Mwanamke hajafunga nae Ndoa, means anaendelea kuzini, ama hajaacha njia zake Mbaya ambazo zilipelekea tatizo lake... Mapepo hayataondoka...

Mafuta ya Upako hayatakusaidia, Keki ya Upako haitakusaidia.
Kitu pekee kitachokusaidia ni kuamua kuishi Maisha safi ya kumpendeza Mungu ama Kwa Lugha nyingine Maisha Matakatifu...!

Tena ukiamua kuishi Maisha Matakatifu Huna haja kupoteza muda kuombewa, hayo Mapepo yataondoka yenyewe haraka Sana (Mimi ni Shahidi)

Tatizo letu Binadamu tunataka Mungu atufungue na akishafanya hivyo tunataka kuendelea na Maisha yetu ya zamani, Starehe, Ngono, Na Dhambi zingine Mbaya...!

Always huwashauri Watu, kama Kuna Watu wanatakiwa kuamua kumgeukia Mungu Moja Kwa Moja ni Watu wenye Mapepo na Majini Mahaba....! Na ipo sababu Kwa Nini baadhi ya Watu husumbuliwa na hizo Spirit, na siku wakijua Sababu.... WANGEACHANA NA UCHAFU WA HII DUNIA NA KUMTEGEMEA MUNGU.
Tatizo ni hao wanaojidai kumtoa mapepo na hawana uwezo huo
 
Back
Top Bottom