Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Bila kumsikia Martha mwenyewe haya ni majungu Tu.

Halafu niwaambie kama huna msimamo ndugu wanakupanda kichwani ,unaweza kuta nusu ya pesa zako zinaishia Kwa ndugu ,na ndugu shida haziishi.

Halafu hawa wazazi baadhi huwa hawaridhiki yaani kwakuwa alikuzaa na Una kipato basi anahisi kila kitu chako ni chake.

Nashukuru wazazi wangu wote wawili siyo ving'ang'anizi yaani , kwanza hata kama wanashida huwa wanaomba Kwa aibu mno.ni Mimi tu nitambue mahitaji Yao.

Lakini kuna familia ukiwa nacho watataka uwalipe Mshahara,tena kama mama hajielewi ndiyo Kwanza atakusagia kunguni
 
Katika maisha kuna mzunguko wa vitendo tunavyo fanya sasahivi baadae vitendo hivyo huturudia sisi yaani ukiwasafiri wazazi wako wakakosa msaada huko mbeleni kuna uwezekano na wewe watoto wako waka kusafiri pia

Hapo tujifunza kwamba hapo Huyo mama mwaipaja analipwa kwa vitendo alivyo wafanyia wazazi wake na kama si hivyo basi Martha atakuja kulipwa na watoto wake the same anavyofanya sasa hivi haijalishi una hali gani kiuchumi ipo siku tu utatamani wanao wawe karibu yako
 
Mama zetu Hawa wa kitanzania watatafutaje pesa mkuu unakuta mama umri umeende ana presha ana kisukari doctor anampa ushauri asifanye kazi kulinda afya yake ni wakuonewa huruma tu
Tatizo mojawapo kubwa la Waafrika hawajiandai na maisha yao ya uzeeni, ni muhimu mtu ajipange kivyake kwa maisha ya uzeeni badala ya kusubiria kutegemea watoto na ndugu.
 
Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake akidai kuwa Martha Mwaipaja ana fedha nyingi sana lakini hamsaidii mama yake vilevile akidai kuwa amejitenga na ndugu zake

Tazama Video hizi kwa utulivu
Ugomvi wa familia tuuuachie wenyewe
 
Nimeshangaa sana huyo jamaa kuwasema wadada. Wengi sio wachoyo na wanatunza wazazi wao. watakuwepo ambao sio wema lakini ni wachache.
Nimeshangaa sana, ninapokuwa na dada zangu hupenda kugharimia kila kinachohitajika, ukitoa pesa unaambiwa rudisha mfukoni, sisi tutafanya!! Nimeshangaa mwenzangu dada zake wachoyo!!
Kuna situation moja niliishangaa sana, dada alikuja na shemeji, wakiwa pamoja wakanipa pesa, baadaye kila mmoja kwa upekee akanipa pesa, kwa kweli sikuelewa maana yake.
 
Back
Top Bottom