Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Mbona watanzania hawajawahi kukataa chochote wanacholetewa , kwanini msiwaambie ukweli tu kwamba mabehewa yatakayokuja ni ya kawaida badala ya kuwapiga fix ?
Hapana.

Kama "mabehewa yanayokuja" muonekano wake ni sawa na hiyo picha iliyowekwa hapo, (picha #2), hayo yatakuwa siyo "mabehewa ya kawaida" hata kidogo!
Hata yale ya 'mete gauge' mbona yatakuwa ni bora zaidi kwa mwonekano wake kuliko haya!

Bado siamini kwamba hiyo picha ndiyo mabehewa yatakayotumika kwenye SGR.
 
mmepigwaaa!! hayo mlioletewa ya mwaka 47..wameya renovate kwa rangi na viti. Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake...hamsikiii.
 
honestly nilikuwa simkubali jiwe 100%. ila sasa nimeanza kuona umuhimu wa ile kauli yake ya "mtanikumbuka".

pamoja na ukatili wake wote, hili la treni iliyochakaa, mgao wa umeme nk, asingekubali vitokee chini ya utawala wake. angetumbua watu kama hana akili nzuri.

ila kwa huyu mama, itakuwa ni business as usual, litapita kimyakimya. akiona mnampigia sana kelele mitandaoni, atajitungia trip ya wiki kadhaa europe.
Hiyo oda ilishatolewa na mwendazake muda mrefu tu. Usimsingizie Samia
 
Machadema yalaaniwe kwakweli hawa ndio wanasababisha tunaletewa mabehewa ya kwenye sinema za kihindi

Una tatizo kwenye ubongo wako. Unakaribia kuwa mwehu. Naona nchi imewashinda mmeamua kuwageukia CHADEMA. Bajeti ya kwenu, pesa mnazo nyie mnunue mabehewa mabovu wenyewe halafu lawama kwa CHADEMA. Kweli Tanzania vichaa wengi.
 
Machadema yalaaniwe kwakweli hawa ndio wanasababisha tunaletewa mabehewa ya kwenye sinema za kihindi

Ulaniiwe mwenyewe Mwehu usiye na haya. CHADEMA wangefanya Nini?. Unamlaumu CHADEMA aliyepo nje, halafu unawasifu CCM wwalionunua mabehewa mabovu. Kwa Hali hii Tanzania tutapiga mark time.
 
Mwenzako anaangalia rangi labda. Shida kubwa ya kwetu tunadhani kuwa mwanaharakati nikupinga kila kitu kwanini tusisubiri kutumia halafu tutoe hukumu zetu tunataka mabehewa kama ya ulaya lakini nauli za kibongo. Ndio maana hata kwenye ndege kuna Air Tanzania, Emirates, Precious, Qatar sijui Ethiopia zote ndege lakini hazifanani na nauli hazifanani.

Hayo mabehewa hayatapata wateja.
 
Back
Top Bottom