Mara nyingi tukiandika humu kuhusu mambo haya huwa tunaitwa Pinga pinga , Lakini ni lazima ifahamike kwamba sisi kama binadamu wenye akili timamu , tuliosafiri hapa na pale duniani , ambao pia tu wasomi wenye macho yanayoona , hatuwezi kuacha kuhoji mambo yenye kutiliwa shaka .
Ni kweli kwamba Mabehewa yamefika na yameanza kupokelewa Bandarini , lakini bila kumung'unya maneno , Mabehewa haya ni DUNI , wala hayana tofauti sana na Mabehewa ya TRC yaliyotelekezwa pale Shauri moyo , Sasa ile Mikwara kwamba zinaletwa Treni za Kisasa wadanganyaji walilenga nini ?
Mbona watanzania hawajawahi kukataa chochote wanacholetewa , kwanini msiwaambie ukweli tu kwamba mabehewa yatakayokuja ni ya kawaida badala ya kuwapiga fix ?
Ni Dharau ya kiwango cha juu sana kudhani kwamba Watanzania ni Wajinga kiasi cha kudanganywa kibwege namna hiyo , Yaani kwamba sisi hatuoni hata kwenye sinema hizo treni za kisasa ?
Tambueni kwamba KILA UBAYA UTALIPWA