Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Mara nyingi tukiandika humu kuhusu mambo haya huwa tunaitwa Pinga pinga , Lakini ni lazima ifahamike kwamba sisi kama binadamu wenye akili timamu , tuliosafiri hapa na pale duniani , ambao pia tu wasomi wenye macho yanayoona , hatuwezi kuacha kuhoji mambo yenye kutiliwa shaka .

Ni kweli kwamba Mabehewa yamefika na yameanza kupokelewa Bandarini , lakini bila kumung'unya maneno , Mabehewa haya ni DUNI , wala hayana tofauti sana na Mabehewa ya TRC yaliyotelekezwa pale Shauri moyo , Sasa ile Mikwara kwamba zinaletwa Treni za Kisasa wadanganyaji walilenga nini ?

Mbona watanzania hawajawahi kukataa chochote wanacholetewa , kwanini msiwaambie ukweli tu kwamba mabehewa yatakayokuja ni ya kawaida badala ya kuwapiga fix ?

Ni Dharau ya kiwango cha juu sana kudhani kwamba Watanzania ni Wajinga kiasi cha kudanganywa kibwege namna hiyo , Yaani kwamba sisi hatuoni hata kwenye sinema hizo treni za kisasa ?

Tambueni kwamba KILA UBAYA UTALIPWA
Wameleta mabehewa mtumba, Walamba asali. Magu asisingiwe.
 
Picha za hayo mabehewa mkuu

IMG_0955.jpg
 
mara nyingi sana ukiona tu kichwa huwa ni tofauti sana na kiwililiwili chake
 
Yaani walichoangalia chadema ni walau rangi ya combat zao iwepo kwenye behewa tu basi, kuhusu ubora hawajali kabisa
IMG_0955.jpg
 
Mtanikumbuka

Unaweza kukuta dalali ni Lisu

Hapa Godfather wako Meko ndiyo alicheza uhuni alitoa tenda kwa kampuni ya Kikorea na wahuni wenzake wakala 10%

IMG_9461.jpg


Meko alitoa tenda kwa kampuni ya Kikorea hii Hapa ndiyo imetuletea haya Mabati. Unayoyaona zilitakiwa kuja 36 naona wametuletea 14 tu.


Baada ya serikali ya Samia kutokuvutiwa na hizi chuma Chakavu ikatangaza tenda uuindaji wa mabehewa 1430 ambayo kampuni ya China wanaitwa CRRC ndiyo washindi wa hii tenda. y
IMG_9462.jpg


Mabehewa yake yataanza kuingia kuanzia September 2023.
 
Yaani kazi yako kubeba spika na bendera za Chadema kwenda mikutanoni, tayari umejua mabehewa hayana ubora.

Shule yenyewe ulikuwa mtoro, madaftari unafungia maandazi, na kazi kubwa ilikuwa kujificha makorongoni au vichakani ukivuta

Haichekeshi.
 
Ni kweli kwamba Mabehewa yamefika na yameanza kupokelewa Bandarini , lakini bila kumung'unya maneno , Mabehewa haya ni DUNI , wala hayana tofauti sana na Mabehewa ya TRC yaliyotelekezwa pale Shauri moyo , Sasa ile Mikwara kwamba zinaletwa Treni za Kisasa wadanganyaji walilenga nini ?
Ungetusaidia sasa sisi tusiojua kwa kuruonyesha picha ya kilichopokelewa na hizo za ulaya ulizo ziona.
P
 
Nachokiona kama usimamizi wa mali za serikali ni wakusuasua tutarajie majanga makubwa katika miradi yote inayoendelea pamoja na yote siamini kama mabehewa haya yaliyoletwa yana ubora kiasi gani kwa ajiri ya matumizi ya SGR.

Serikali tangu asubuhi mzigo unatolewa kwenye meli na watu miluzi imekuwa mingi hata kauli ya serikali hamna[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

FB_IMG_1669206905910.jpg
 
Back
Top Bottom