Mkuu umeona mbali sana, ukiona India na china hawafanyiwi figisu kwenye kununua mafuta ya bei chee ya urusi basi hapo jua makampuni ya beberu yapo ndani ya biashara hiyo, hapo beberu ataendelea kutengeneza faida kubwa huku urusi akiingia hasara kwa kudhani anamkomoa beberu namba moja marekani.Beberu ni mtu mbaya sana. Usishangae ndiye anayenunua mafuta ya Russia kwa mgongo wa India na wenzake.
Hata hivyo ushauri wako kwa nchi yetu ni muhimu sana. Sijui balozi wetu Moscow anafanya kazi gani.
Mbona China na India wameshindwa kuzipiga ban, sisi kwa nini ufikiri tutapigwa ban?Mwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka
Siyo kwamba Russia wanauza crude oil pekee. Ukitaka refined oil watakuuzia. Wanauza both crude oil and refined oil kama ambavyo Waarabu wanavyofanya.Hapo unazungumzia crude Oil. Sasa sisi tukinunua hiyo crude oil tutaiweka wapi. Hatuna refinery wala nini. Sisi tupambane na petroli zetu tu
Makini sana, kudos MkuuSiyo kwamba Russia wanauza crude oil pekee. Ukitaka refined oil watakuuzia. Wanauza both crude oil and refined oil kama ambavyo Waarabu wanavyofanya.
Na nchi nyingi duniani hununua crude oil badala ya refined oil kwani bei ya crude oil ni rahisi sana kuliko refined oil. Refinery hufanyika nchini kwao na ni much cheaper na wananchi wao kupata ajira. Viwanda vya refinery bei yake haizidi bei ya kujenga Tanzanite bridge wala Magufuli bridge ya Kigongo - Busisi huko Mwanza. Kama tumeweza kujenga Nyerere hydropower plant na SGR, tutashindwa vipi kujenga viwanda viwili au vitatu vya oil refinery? Tena kwa pesa yetu wenyewe, cash money. Ni utashi tu wa kisiasa. Wizara yetu ya uchumi na mipango inapaswa kuliona hili. Wabunge wetu wanapaswa kuliona hili na kuishinikiza serikali yetu kutekeleza hili. Wananchi wetu watapata ajira. Nchi jirani kama DRC na zingine zisizo na refineries wangalinunua mafuta haya kutoka kwetu. Ni kama tunavyotaka kufanya kwa madawa kupitia MSD kuuzia nchi za SADEC.
Hata sisi tunaweza kununua mafuta haya kimya kimya kutoka Russia au China. Kwa nini tunang'ang'ania kuyanunua toka Uarabuni pekee hata kama bei zao ni za juu zaidi? Kwani sheria yetu ya manunuzi inasemaje?Ukute aNanunua hukohuko then wanakuja kutuxia bei ya dubiani.
By the way USA mwenyewe ananunya gas kinyakinya huko then znawauxia Europe wajinga kwa bei ya soko.
Tukumbuke hicho kiwanda kilikuwepo, Kigamboni pale, kilikua kinaitwa TIPER.Kusimika mitambo ya kuchuja inagharama kiasi gani? Au kutafuta mwekezaji alete mzigo wa refinery na ifanyike hapa nchini
Uko sahihi kabisa. Na kama leo bei ya crude oil ya kutoka OPEC ni dola 130 kwa pipa, basi bei ya refined oil tunayonunua sisi itakuwa zaidi ya dola 250 kwa pipa. Hii huwa haitangazwi, hizo refineries ni za watu binafsi na nyingi ndogo ndogo za wamachinga wa huko na kila mmoja ana bei yake.Siku zote ukisikia bei ya mafuta kwenye soko la dunia hua wana maana ya crude oil na sio petrol, diesel nk. Well, OPEC kwa ujumla wake leo wanauza dola 130 hiyo hiyo crude oil
Ivi ile TIPER ilikuwa Kule upande wa Kigamboni? walikuwa wanafanya Refinery nakumbuka, sijaisikia bado ina exist??Hapo unazungumzia crude Oil. Sasa sisi tukinunua hiyo crude oil tutaiweka wapi. Hatuna refinery wala nini. Sisi tupambane na petroli zetu tu
Hio itakuwa Myopic thinking.... Yaani to cut your nose to spite your face.....Sasa kwa nini na sisi tusichangamkie fursa hii ( na kupenda iendelee kudumu) kwa kununua mafuta haya toka Russia? Kuna tatizo gani tukifanya hivyo? Tunaogopa nini? Au watalaamu wety wa uchumi mnasemaje?
Ni hyperopic thinking (kuona mbali) na si myopic (kuona karibu). Kwa wale tunaoona mbali (hyperopic), hii vita si ya Russia vs Ukraine bali ni vita ya USA vs Russia, yaani kati ya super powers wa dunia hii kutafuta mbabe wa dunia. Nchi ya Ukraine inatumika tu kama uwanja wao wa mapambano. Vifaa vya vita na askari kutoka USA na Ulaya vinaingia Ukraine kwenda kupambana na Urusi. Juzi rais wa USA alikuwa huko na alikutana na askari wake kuwapa morali. Alikula chakula pamoja cha jioni na askari wake. Hizo sanctions za kiuchumi dhidi ya Russia ni sehemu ya vita hiyo.Hio itakuwa Myopic thinking.... Yaani to cut your nose to spite your face.....
Ila all in all sanctions is a two edged sword na huenda baada ya yote haya USA will have lost more than what he has gained since USSR Collapse
USD billion 2 China anakujengea Oil Refinery Plant kubwa ya kuweza kusafisha crude oil hadi ya nchi majirani zetu! Nchi za mabeberu zitakujengea refinery ya ukubwa huo kwa zaidi ya dola billioni 7.Wabongo mna maneno mepesi sana. Hivi mnajua gharama za kujenga refinery au hata kuifufua hiyo ya zamani? Ni zaidi ya 10 billion USD. Huyo mwekezaji yuko wapi? Na mpaka hiyo refinery ikamilike bado Urusi watakuwa kwenye vikwazo tuu na kulazimika kuuza mafuta yao kwa bei ya chini?
Angalao Nyerere alionesha njia na kazi aliianza kama ile ya kuhamia Dodoma na bwawa la Stiglers gauge. Tunaamini mama atamalizia kazi hiyo iliyobaki ya kujenga Oil Refinery Plant kubwa litakalotuwezesha kuuzia nchi za SADEC mafuta ya petroli, diseal na ya taa. Neema zaidi itakuwa pale tutakapokamilisha bomba la crude oil ya Museveni, Uganda, kwani crude oil hii tutakuwa tunaipata hapahapa Tanga kwa wasambaa! Kazi iendelee!!!Hata enzi za Nyerere na TIPER refinery bado tulikuwa tunaagiza mafuta na bado kulikuwa na uhaba wa mafuta. TIPER ilikuwa ni refinery ndogo.
Ndo maana nikasema kama tulikuwa na refinery ndogo enzi za mwalimu, kwenye kutathmini hatua za kimaendeleo leo hii tulitakiwa tuwe na refinery kubwa ambayo ingeweza kusafisha hadi mafuta ya nchi jirani......
Kama Tanzania inaagiza mapipa 35,000 ya mafuta kwa siku, refinery gani hiyo utajenga kwa USD bilion 2 itakayotengeza hayo mapipa na ziada ya kuuza nje?USD billion 2 China anakujengea Oil Refinery Plant kubwa ya kuweza kusafisha crude oil hadi ya nchi majirani zetu! Nchi za mabeberu zitakujengea refinery ya ukubwa huo kwa zaidi ya dola billioni 7.
Crude ya Uganda itaenda China na iliyobaki itauzwa kwenye soko la dunia. Crude ya Uganda utainunua kwa bei hiyo hiyo unayoona crude oil inauzwa kwenye soko la dunia $130 kwa pipa.Angalao Nyerere alionesha njia na kazi aliianza kama ile ya kuhamia Dodoma na bwawa la Stiglers gauge. Tunaamini mama atamalizia kazi hiyo iliyobaki ya kujenga Oil Refinery Plant kubwa litakalotuwezesha kuuzia nchi za SADEC mafuta ya petroli, diseal na ya taa. Neema zaidi itakuwa pale tutakapokamilisha bomba la crude oil ya Museveni, Uganda, kwani crude oil hii tutakuwa tunaipata hapahapa Tanga kwa wasambaa! Kazi iendelee!!!
Kuna crude oil ya kutoka uganda itaanza kupelekwa nje kupitia bandari ya Tanga, unaonaje tukiwekeza kwa ajili ya kununua na kusafisha wenyewe na byproducts kama lami tukatumia kwenye kujenga barabara zetu.Nani atatoa mkopo wa kujenga hiyo refinery? Kama tungekuwa tunachimba mafuta yetu wenyewe ningekuelewa. Kwa mfano Dangote anajenga refinery Nigeria akijua hiyo 15 billion USD atakayotumia kujenga atairudisha kwa sababu Nigeria ina mafuta ya kutosha (guaranteed supply at fixed price). Nyie mnategemea tujenge kwa kutegemea Urusi watuuzie mafuta ya bei ya kutupa kila siku mtaleta hasara tuu na hiyo refinery itafilisika kama ile ya TIPER ilivyofilisika.
Utainunua kwa bei ya soko la dunia. Kwa nchi kukuuzia mafuta kwa bei ya chee lazima kuwe na makubaliano. Kwa mfano Iran na China wamekubaliana kuuziana mafuta kwa bei chee kwa sababu Iran imewekewa vikwazo. Urusi nayo iko hivyo. Nchi zinazochimba mafuta zinajua kuna siku mafuta yao yataisha. Kwa hiyo wanataka ku maximize their profits now. Hawakubali kirahisi kuuza tuu rasilimali yao kwa bei ya chini. Ikiisha watakula nini?Kuna crude oil ya kutoka uganda itaanza kupelekwa nje kupitia bandari ya Tanga, unaonaje tukiwekeza kwa ajili ya kununua na kusafisha wenyewe na byproducts kama lami tukatumia kwenye kujenga barabara zetu.
We juha kweli aliyekuambia Iran vikwazo vinamsumbua nani hivi irani pamoja na vikwazo vyote nchi gani ya Africa inayo mfikiaMwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka