Bei ya mafuta ya petroli, dizeli toka Urusi sasa ni $30 kwa pipa. China na India wachangamkia fursa. Kwanini Tanzania isifanye hivyo pia?

Bei ya mafuta ya petroli, dizeli toka Urusi sasa ni $30 kwa pipa. China na India wachangamkia fursa. Kwanini Tanzania isifanye hivyo pia?

Beberu ni mtu mbaya sana. Usishangae ndiye anayenunua mafuta ya Russia kwa mgongo wa India na wenzake.
Hata hivyo ushauri wako kwa nchi yetu ni muhimu sana. Sijui balozi wetu Moscow anafanya kazi gani.
Mkuu umeona mbali sana, ukiona India na china hawafanyiwi figisu kwenye kununua mafuta ya bei chee ya urusi basi hapo jua makampuni ya beberu yapo ndani ya biashara hiyo, hapo beberu ataendelea kutengeneza faida kubwa huku urusi akiingia hasara kwa kudhani anamkomoa beberu namba moja marekani.
 
Mwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka
Mbona China na India wameshindwa kuzipiga ban, sisi kwa nini ufikiri tutapigwa ban?
 
Hapo unazungumzia crude Oil. Sasa sisi tukinunua hiyo crude oil tutaiweka wapi. Hatuna refinery wala nini. Sisi tupambane na petroli zetu tu
Siyo kwamba Russia wanauza crude oil pekee. Ukitaka refined oil watakuuzia. Wanauza both crude oil and refined oil kama ambavyo Waarabu wanavyofanya.

Na nchi nyingi duniani hununua crude oil badala ya refined oil kwani bei ya crude oil ni rahisi sana kuliko refined oil. Refinery hufanyika nchini kwao na ni much cheaper na wananchi wao kupata ajira. Viwanda vya refinery bei yake haizidi bei ya kujenga Tanzanite bridge wala Magufuli bridge ya Kigongo - Busisi huko Mwanza. Kama tumeweza kujenga Nyerere hydropower plant na SGR, tutashindwa vipi kujenga viwanda viwili au vitatu vya oil refinery? Tena kwa pesa yetu wenyewe, cash money. Ni utashi tu wa kisiasa. Wizara yetu ya uchumi na mipango inapaswa kuliona hili. Wabunge wetu wanapaswa kuliona hili na kuishinikiza serikali yetu kutekeleza hili. Wananchi wetu watapata ajira. Nchi jirani kama DRC na zingine zisizo na refineries wangalinunua mafuta haya kutoka kwetu. Ni kama tunavyotaka kufanya kwa madawa kupitia MSD kuuzia nchi za SADEC.
 
Makini sana, kudos Mkuu
 
Ukute aNanunua hukohuko then wanakuja kutuxia bei ya dubiani.

By the way USA mwenyewe ananunya gas kinyakinya huko then znawauxia Europe wajinga kwa bei ya soko.
Hata sisi tunaweza kununua mafuta haya kimya kimya kutoka Russia au China. Kwa nini tunang'ang'ania kuyanunua toka Uarabuni pekee hata kama bei zao ni za juu zaidi? Kwani sheria yetu ya manunuzi inasemaje?
 
Hii ndiyo fursa yenyewe,,,mama samia changamkia hiyo fursa.

Mama lamama nakuombea maisha marefu
Puttin babaa nakuombea maisha marefu, shikisha adabu hao killers/magaidi
 
Siku zote ukisikia bei ya mafuta kwenye soko la dunia hua wana maana ya crude oil na sio petrol, diesel nk. Well, OPEC kwa ujumla wake leo wanauza dola 130 hiyo hiyo crude oil
Uko sahihi kabisa. Na kama leo bei ya crude oil ya kutoka OPEC ni dola 130 kwa pipa, basi bei ya refined oil tunayonunua sisi itakuwa zaidi ya dola 250 kwa pipa. Hii huwa haitangazwi, hizo refineries ni za watu binafsi na nyingi ndogo ndogo za wamachinga wa huko na kila mmoja ana bei yake.
 
Sasa kwa nini na sisi tusichangamkie fursa hii ( na kupenda iendelee kudumu) kwa kununua mafuta haya toka Russia? Kuna tatizo gani tukifanya hivyo? Tunaogopa nini? Au watalaamu wety wa uchumi mnasemaje?
Hio itakuwa Myopic thinking.... Yaani to cut your nose to spite your face.....

Ila all in all sanctions is a two edged sword na huenda baada ya yote haya USA will have lost more than what he has gained since USSR Collapse
 
Ni hyperopic thinking (kuona mbali) na si myopic (kuona karibu). Kwa wale tunaoona mbali (hyperopic), hii vita si ya Russia vs Ukraine bali ni vita ya USA vs Russia, yaani kati ya super powers wa dunia hii kutafuta mbabe wa dunia. Nchi ya Ukraine inatumika tu kama uwanja wao wa mapambano. Vifaa vya vita na askari kutoka USA na Ulaya vinaingia Ukraine kwenda kupambana na Urusi. Juzi rais wa USA alikuwa huko na alikutana na askari wake kuwapa morali. Alikula chakula pamoja cha jioni na askari wake. Hizo sanctions za kiuchumi dhidi ya Russia ni sehemu ya vita hiyo.

Kwa hiyo vita hii upo uwezekano mkubwa wa kuchukua miaka kadhaa kama ilivyotokea kule Syria na Afghanstan ambako miamba hii ilihusika. Na upo uwezekano wa vita hii kuwa vita kuu ya tatu ya dunia itakayotumia zana za kisasa za vita pamoja na nuclear weapon. North Korea imeanza kupasha pasha makombora yake ya nuclear ya kuelekea USA.

Hivyo vita hii bado iko kwenye infant stage. Tatizo letu ni kuwa tumeanza kulialia kwenye infant stage. Itakapofikia adult stage sijui hali yetu itakuwa vipi. Ni muhimu sana tukajipanga vizuri kukabiliana na changamoto zitakazoendelea kujitokeza. Hatupaswi ku panic bali kuwa watulivu na kufanya maamuzi ya busara.

Uamuzi wa kununua mafuta toka Russia kama ambavyo mataifa makubwa ya China na India yalivyofanya si wa kupuuza. Vita hii inaweza kuchukua hata miaka mitano. Pia uamuzi wa kujenga Oil Refinery Plant ya kutosheleza angalao mahitaji yetu ya oil si jambo la kupuuza. Bei ya Oil Refinery Plant kubwa kutoka China haizidi dola bilioni 2, sawa na bei ya software waliyokodisha tanesco kutoka India. Bei hii haizidi ya transformer kubwa moja la tanesco ambazo wame press order ya kujengewa toka ughaibuni matrasfomer kadhaa na vikombe ili mwaka 2024 umeme wetu uwe stable!

Tumwombe sana Mheshimiwa January alipe kipaumbele cha kwanza hili suala la Oil Refinery Plant toka China. Tumemwelewa kwamba mambo ya tanesco ni ya sayansi tusiyopaswa kuyaingilia. Hili la Oil Refinery Plant bila shaka siyo la sayansi sana kivile bali la kiuchumi.
 
Wabongo mna maneno mepesi sana. Hivi mnajua gharama za kujenga refinery au hata kuifufua hiyo ya zamani? Ni zaidi ya 10 billion USD. Huyo mwekezaji yuko wapi? Na mpaka hiyo refinery ikamilike bado Urusi watakuwa kwenye vikwazo tuu na kulazimika kuuza mafuta yao kwa bei ya chini?
USD billion 2 China anakujengea Oil Refinery Plant kubwa ya kuweza kusafisha crude oil hadi ya nchi majirani zetu! Nchi za mabeberu zitakujengea refinery ya ukubwa huo kwa zaidi ya dola billioni 7.
 
Hata enzi za Nyerere na TIPER refinery bado tulikuwa tunaagiza mafuta na bado kulikuwa na uhaba wa mafuta. TIPER ilikuwa ni refinery ndogo.
Angalao Nyerere alionesha njia na kazi aliianza kama ile ya kuhamia Dodoma na bwawa la Stiglers gauge. Tunaamini mama atamalizia kazi hiyo iliyobaki ya kujenga Oil Refinery Plant kubwa litakalotuwezesha kuuzia nchi za SADEC mafuta ya petroli, diseal na ya taa. Neema zaidi itakuwa pale tutakapokamilisha bomba la crude oil ya Museveni, Uganda, kwani crude oil hii tutakuwa tunaipata hapahapa Tanga kwa wasambaa! Kazi iendelee!!!
 
Ndo maana nikasema kama tulikuwa na refinery ndogo enzi za mwalimu, kwenye kutathmini hatua za kimaendeleo leo hii tulitakiwa tuwe na refinery kubwa ambayo ingeweza kusafisha hadi mafuta ya nchi jirani......

Nani atatoa mkopo wa kujenga hiyo refinery? Kama tungekuwa tunachimba mafuta yetu wenyewe ningekuelewa. Kwa mfano Dangote anajenga refinery Nigeria akijua hiyo 15 billion USD atakayotumia kujenga atairudisha kwa sababu Nigeria ina mafuta ya kutosha (guaranteed supply at fixed price). Nyie mnategemea tujenge kwa kutegemea Urusi watuuzie mafuta ya bei ya kutupa kila siku mtaleta hasara tuu na hiyo refinery itafilisika kama ile ya TIPER ilivyofilisika.
 
USD billion 2 China anakujengea Oil Refinery Plant kubwa ya kuweza kusafisha crude oil hadi ya nchi majirani zetu! Nchi za mabeberu zitakujengea refinery ya ukubwa huo kwa zaidi ya dola billioni 7.
Kama Tanzania inaagiza mapipa 35,000 ya mafuta kwa siku, refinery gani hiyo utajenga kwa USD bilion 2 itakayotengeza hayo mapipa na ziada ya kuuza nje?
 
Angalao Nyerere alionesha njia na kazi aliianza kama ile ya kuhamia Dodoma na bwawa la Stiglers gauge. Tunaamini mama atamalizia kazi hiyo iliyobaki ya kujenga Oil Refinery Plant kubwa litakalotuwezesha kuuzia nchi za SADEC mafuta ya petroli, diseal na ya taa. Neema zaidi itakuwa pale tutakapokamilisha bomba la crude oil ya Museveni, Uganda, kwani crude oil hii tutakuwa tunaipata hapahapa Tanga kwa wasambaa! Kazi iendelee!!!
Crude ya Uganda itaenda China na iliyobaki itauzwa kwenye soko la dunia. Crude ya Uganda utainunua kwa bei hiyo hiyo unayoona crude oil inauzwa kwenye soko la dunia $130 kwa pipa.
 
Nani atatoa mkopo wa kujenga hiyo refinery? Kama tungekuwa tunachimba mafuta yetu wenyewe ningekuelewa. Kwa mfano Dangote anajenga refinery Nigeria akijua hiyo 15 billion USD atakayotumia kujenga atairudisha kwa sababu Nigeria ina mafuta ya kutosha (guaranteed supply at fixed price). Nyie mnategemea tujenge kwa kutegemea Urusi watuuzie mafuta ya bei ya kutupa kila siku mtaleta hasara tuu na hiyo refinery itafilisika kama ile ya TIPER ilivyofilisika.
Kuna crude oil ya kutoka uganda itaanza kupelekwa nje kupitia bandari ya Tanga, unaonaje tukiwekeza kwa ajili ya kununua na kusafisha wenyewe na byproducts kama lami tukatumia kwenye kujenga barabara zetu.
 
Utainunua kwa bei ya soko la dunia. Kwa nchi kukuuzia mafuta kwa bei ya chee lazima kuwe na makubaliano. Kwa mfano Iran na China wamekubaliana kuuziana mafuta kwa bei chee kwa sababu Iran imewekewa vikwazo. Urusi nayo iko hivyo. Nchi zinazochimba mafuta zinajua kuna siku mafuta yao yataisha. Kwa hiyo wanataka ku maximize their profits now. Hawakubali kirahisi kuuza tuu rasilimali yao kwa bei ya chini. Ikiisha watakula nini?
 
Mwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka
We juha kweli aliyekuambia Iran vikwazo vinamsumbua nani hivi irani pamoja na vikwazo vyote nchi gani ya Africa inayo mfikia
 
Back
Top Bottom