Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Hakuweka akiba ya maneno huyu mtu.
Ndoto yake imetimia, mahakama zipo huru sasa

IMG-20211028-WA0011.jpg


IMG-20211028-WA0015.jpg


IMG-20211028-WA0014.jpg
 

Attachments

  • VID-20211028-WA0012.mp4
    102.2 KB
  • VID-20211028-WA0016.mp4
    2 MB
“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako ukadhani kwamba utaendelea kupiga miluzi na kufurahia kana kwamba wewe umefika Duniani kama Kiongozi au ndio mkubwa au Mungu Mtu, Mahakama Kuu ni jibu kwamba ukidhalilishwa fika Mahakamani uitafute haki yako nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu"

"Naomba wajue hili halitotokea tena, hasimami tena kudhalilisha Wazee na Viongozi wake, hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu, hasimami tena kuwatukana Watu walioifanyia kazi Nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wote, anasimama Mtu kwa kutumwa na kulipwa akadhani kwamba ataendelea kuishi Duniani katika hali hiyo hamtomuona tena akifanya hivyo na Musiba huko uliko naomba hela zangu"

Bernard Membe

Pia, soma=> Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

28 October 2021

Bernard Membe atoa angalizo kuwa kuanzia sasa hakuna tembo wala sisimizi
... ni baada ya hukumu kutolewa ktk Mahakama Kuu ya Tanzania




Source : Mwananchi Digital
 
Hizi hukumu za mfululizo zinazomkabili Cyprian Musiba kutoka kwa wanaccm wenzake hazina afya kwa chama.

Enzi za Mwalimu Nyerere huyu Musiba na Membe au na Fatma wangeitwa mbele ya vikao vya maadili vya chama na kusikilizwa na Uamuzi au Suluhu kupatikana

Ni aibu kubwa kuthibitishiwa na mahakama kuwa CCM ina watu wahuni wahuni wasioheshimu wazee wetu.

Kumtukana Membe au Kinana ndani ya chama ni ushenzi uliopitiliza.

Na nyie vijana mliobaki mjifunze kuheshimu waliowatangulia.

Maendeleo hayana vyama!
Hiyo suluhu ingetafutwa wakati Membe alipolalamika mara ya kwanza na kufungua kesi au lini? CCM ilikuwa ikifanya kazi kama chama cha siasa wakati ule?
 
Mdharirishaji mwingine ni "power kaaya"!

Kijana miaka 31 unamtongoza Mama mwenye miaka 60, huu ni udhalilishaji wa kijinsia!!

Nasubiri kusikia kutoka kwa Rais mwenye ngonjera ya jinsia ya kike atasemaje kuhusu Power kaaya!!
Mwanasesere wa Polepole a.k. a bi, Chokochoko, mitala ya Makunduchi imemuaribu, taarabu na ngonjera tu vimemjaa mkichwani. Hamna kitu.
 
Mzee Membe kumbuka pia kwamba deni kalifungi.
Hii sio sawa na deni la kukopa mzee..hii ni defamation. Ukishindwa kulipa unapigwa miaka, mradi aliekushitaki anaweza kukulipia chakula Cha jela
 
Toka maktaba :

11 April 2018
Bungeni, Dodoma

MBUNGE SELASINI: "Serikali Mmemtuma Musiba, Mbona Mnamkalia Kimya"

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, ameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Cyprian Musiba, ambaye huitisha mikutano na waandishi wa habari na kushutumu baadhi ya viongozi na kutoa maagizo kuwa angekuwa yeye angeweza hata kuua.

Mbunge Selasini amemuomba Waziri mwenye dhamana ya Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, kulichukulia hatua gazeti linalomilikiwa na mtu huyo.

Aidha Mbunge Selasini, amesema kwa ali ya sasa ilivyo ya matukio ya watu kupotea na kuuawa, halafu Musiba anasema hadharani kuwa angekuwa yeye angeua, lakini serikali inamsikia na haimchukulii hatua, hali hiyo inampelekea kujenga hoja kwamba, Serikali imemtuma mtu huyo na kwamba ni mtu wao, vinginevyo watoe taarifa juu ya mtu huyo kuwa ni nani.

Source : Global tv online
 
Kwenye ule msiba Musiba alilia kwa uchungu akijua kabisa kinachoenda kutokea.

Ila hizo pesa mbona nyingi mpaka zinapoteza uhalisia?...huyo bwana akidaiwa milioni hamsini tu zinatosha kumpa adabu.
Ndo akome..alipe mpaka vitukuu vilipe
 
Waliokuwa wanamshabikia na hata wale waandishi waliokuwa wanaenda kumripoti bila kumuuliza maswali Cypria Musiba sasa wamemkimbia wala hawajitokezi tena kumsifia uanaharakati wake

Toka maktaba

10 May 2021


Cyprian Musiba azungumzia uhuru wa kuzungumza






25 Julai 2019
Mwanaharakati Cyprian Musiba katika mojawapo ya press conference nyingi alizofanya kuputia waandishi wa habari



Reach the goal2 years ago
Wanamwita JPM mshamba kwa kuwa hajui kupiga madili wanamuona hajui maisha ya akili na ujanjaujanja. Jamani watanzania tungeweza hao tungewaacha Mungu atulipie kisasi juu ya waliyowafanyia watanzania na wana CCM. Ila sasa kwa kukosa nidhamu kwao watakwenda na mkondo wa sheria. Waliichafua sana nchi yetu lkn kwa kuwa huwa km tuna asili ya kusameheana waliachwa ili tuendelee mbele na kurekebisha. Tumempata rais anaeturudishia maadili na kurudia kwenye hayo ya msingi tuliyoyaacha. Kama ni nyumba iliachwa kuwa danguro. Mtoto wa Nne wa nchi baada ya baba wa taifa, ameonekana kuweza kuibomoa na kuanza kuijenga upya na kuhakikisha watoto wote wa TANZANIA wanafaidika na urithi aiouacha baba wetu wa taifa. Watoto wengine walikumbwa na dhoruba mawimbi yakawalemea. Ebu tuunganeni kuwaweke kando watoto wa Tanzania wenye ulafi na uchoyo tuungane kurejesha urithi wetu mikononi mwa wengi. Tupo tuliojaribu kurejesha mali za chama tulipata joto ya jiwe. Kuchukiwa kusiko kwa kawaida na jela tunazinusa, tukasema ya nini, endeleeni lkn SIKU itakuja. Mungu ni mwema SIKU ilishafika bila wao kujua, sasa joto imerudi kwao. Tulichelewa kumpata Magufuli ebu tumuungeni mkono atutoe hapa shimoni tulipokuwa tumetumbukia. Mungu Bariki Tanzania na watu wake!
5


kuryanga makeseni makeseni2 years ago
Huyu jamaa Musiba naanza kumeelewa, yuko right kabisa!

20
Princepius Mutaihwa2 years ago
Kwa kweli nashauri mmojawapo kiongozi mkuu mwandamizi wa CCM ajitokeze hadharani aombe radhi watanzania kwa kulea wezi, mafisadi na walanguzi. Hongera JPM
45

7
ALBERT Nshunju2 years ago
Ubarikiwe sana kaka.

11
lemonade soldier2 years ago
Mm nakuelewa sana kaka musiba ......timua vumbi timuaa
 
Vipi mbona hamumongelei kigogo na Mange kimambi wenyewe walikuwa na haki ya kudhalilisha watu na kuwatukana mitandaoni mbona mnamona Musiba peke yake
 
Hii sio sawa na deni la kukopa mzee..hii ni defamation. Ukishindwa kulipa unapigwa miaka, mradi aliekushitaki anaweza kukulipia chakula Cha jela
kama ni hivyo basi kijana wangu kaisha, mimi nilifikiri kama haya madeni yetu tunayopelekana police kila leo mara nimeshindwa kulipa kodi mara uliniuzia mbuzi nikalipa nusu nk
 
Back
Top Bottom