Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Kiufupi ni kuwa wakristo tunamuabudu Mungu wa Israel, Isaka na Yakobo,

Alieumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo
 
Zinauzwa shilingi ngapi? Nataka zile zenye ubora na wapi zinapatikana?
 
Nadhani ni namna ya watu kuonesha upendo kwa Mungu aliyejidhihirisha kupitia Taifa la Israel.
MATENDO YA MITUME 10:34,35 "...Mungu hana upendeleo bali katika kila Taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye "
Watu wanasoma matendo ya Mungu aliyoyafanya kupitia Israel, na Mungu amechagua Taifa mojawapo duniani ili kudhihirisha uwepo wake na nguvu zake.
Angeweza kuchagua Taifa lolote. Waisrael sio viumbe special tofauti na watu wengine, Muisrael asiyemwamini Yesu kama Bwana wake na Mwokozi wake ataenda jehanamu kama wasioamini wengine, kulingana na Biblia.
Hamna sababu ya msingi kulaumu mtu anayetumia uhuru wake kuelezea hisia zake pasipo kuhalifu sheria za nchi.
 
Hiyo nchi ilibalikiwa from beginning that's why. Unavoona sayansi na teknolojia, chanzo ni Israel. na wavumbuzi wa mambo mengi duniani ni Wayahudi. so unavoona bendera nyingi kwa daladala ni wanapata mibaraka coz Israel. maana Sir God alisema JAMAA ZOTE ZA DUNIA ZITABARIKIWA KUTOKANA NA TAIFA LA ISRAEL
 
Mungu mbaguzi huyu! Waja wake kawapanga madaraja, ya mabwana na watwana sio? Amakweli dini ni kilevi, lazima uwe mlevi ndio ukubaliane na upuuzi huo.
 
Mbona hamsemi mnavaa kofia hamsemi zemeandikwa NY (New york)
 
Waafrika wengine ni kama ng'ombe tu.
Waisraeli wanamuita mtu mweusi NYANI halafu Nyani hao hao wanashangilia Waisraeli.
Dah....
Utumwa wa akili mbaya sana
 
Huja sikia kama ubalozi wa Israel utafunguliwa tanzania au umeshafunguliwa, tangu kufungwa 1967.

Sasa hii ni njia ya kusukuma hiyo ajenda.
pesa zimetumika na kwa watanzani watafanya hivyo ikiwa utapewa viji senti na hata kuiweka juu kabisa kwenye gari hata nyumba
 
Mungu mbaguzi huyu! Waja wake kawapanga madaraja, ya mabwana na watwana sio? Amakweli dini ni kilevi, lazima uwe mlevi ndio ukubaliane na upuuzi huo.
Mungu ametumia Israel kufikia watu wa ulimwengu wote. GALATIA 3:28 "...Hapana myahudi wala myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. " Hakuna madaraja hapo, Muisraeli anayefanya dhambi ya ubaguzi atahukumiwa sawasawa na matendo yake, mkristo yeyote hapaswi kumchukia mtu yeyote na isitoshe Yesu mwenyewe alisema wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi... MATHAYO 5:44
 
Tafuta kwenye Biblia mwanzo hadi mwisho hukiti jina la Tanzania wala Tanganyika,,

Israel ni jina teule limetoka kwa MUNGU YEHOVA mwenyewe kapewa mzee Jacob,, Tanzania ni jina tu kama ulivyo jiita wew Emmadogo,,

Mataifa yote yanayo ichukia Israel hulaaniwa na Mungu ,, vita haiishi nchi mwao,, Libya, Misri,, Syria,, Iraq,, Lebanon,, Yemen,,Afganstan,, Somalia,, Sudan nk.

Lakini nchi zote duniani zenye mapenzi mema na Israel zina wingi wa Amani na furaha kwa raia wao,, na ndio limbo lip kwa watu wa mataifa yenye chuki dhidi ya Israel,,
 
Mkuu shikamoo.
Duh sio vizuri kunivunja mbavu zangu usiku huu
Hahahaaaa
 
Umenena vema. Huenda si maneno yako bali ni roho aliyekuongoza.

ISRAEL maana yake ni USHINDI.

 
Siyo hivyo tu, bali Mungu hufanya vyote ili ukuu na utukufu wake upate kuonekana. Mbona hujiulizi kwa nini wewe una miguu miwili, mikono miwili, macho, n.k. wakati wengine ni walemavu? Kwani wamekosa nini? Je, wewe umefanya nini cha pekee hadi uwe na viungo vyote? Je, waliopungukiwa na viungo hawakuumbwa na Mungu? Jibu lipo wazi na ni jibu la kiimani wala siyo la kimantiki - Hekima ya Mungu, siyo hekima ya mwanadamu.

Mungu alipowaangamiza Wamisri, aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Mmisri katika kila familia, unadhani kweli kila familia ilikuwa ina kiburi cha farao? Na je, hao waisrael ambao wote walivushwa kwenye bahari ya Sham wakati Wamisri wakiteketea, walikuwa ni watakatifu? La hasha! Mkono wa Mungu wenye nguvu ulimuokoa kila Muisrael bila ya kujali matendo yake. Kwa nini? Hatuna majibu, bali ni hekima yake Mungu isiyohojiwa na kiumbe wake.

Mungu anabagua viumbe vyake?Wengine watakatifu,wengine si watakatifu,ubaguzi wa rangi wa wazi.
 

.....


......salute !!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…