Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Mzee wetu Mkapa kwani hii Tume ya Uchaguzi unayotamani iwe huru siingewezekana wakati wa Utawala wako?
 
Kuna kitu kitaandikwa kwenye hicho kitabu kitakuwa kigeni masikioni mwa Wanatanzani labla iwe mambo ya Familia yake ila sio siasa ya Tanzania.

Ukiongea ukweli kutoka hewani bila rejea watakuhukumu kwa kukuonea.

Ukirejea ya wakwao upo salama
 
Umenikumbusha mchekeshaji wa Kenya mzee Ojwang' alitimua watu wote ndani akajikuta ,amebaki mwenyewe mwisho akasema na Mimi mwenyewe out nae akatoka nyumba ikanaki empty

🙌🙌🙌🙌
 
Hawa Wazee Wastaafu wakae kimya muda wao wa kuongoza ulishapita, sasa wanakuja na staili hii mpya ya kujitakasa na huenda kunasababu kuu na za msingi wasipuuzwe hawa wastaafu. Moja ni tabia ya Mh. Rais Magufuli kulaumu waziwazi viongozi waliopita utendaji wao hali inayowapelekea kujitokeza kujitetea mbele ya umma.

Na kwa sasa marais wote wastaafu washatoa matamko kwa namna moja ama nyingine. Pili suala la tume huru ya uchaguzi ni mtego kwa rais magufuli wa kumuondoa madarakani kwani inaonekana dhahiri hawafurahishwi naye na hivyo wanaweza kupandikiza mamluki wao kwa kigezo cha tumr huru . Sasa mambo yasipofanyika kwa umakini itakula kwake.
 
Karma kweli Mkapa ameyasema hayo kweli atakuwa ameamua kutubu na Mimi nimemsamehe kabisa maana kausema ukweli big up dady BWM
 
Mkapa anadhihirisha kwamba maisha ya kiafrika hata ukiwa kiongozi mkubwa wa nchi yamejaa unafki mtupu. Kwani kipindi ana force king ile mwaka 2000 hakuyajua hayo ya ulingo sawa wa kisiasa kati ya maccm na wapinzani au umri wa kuwa na busara haukuwa umefika.

Na hatujasahau mwaka 2015 alivyotuita wapumbavu na malofa. Na sasa amejidhihirisha kwamba na yeye ni lodilofa kipeo cha 2.
 
Huku ni kukumbuka shuka mawio wakati jua limeshachomoza!
 
Shetani akizeeka anakuwa malaika.
 
Huwezi kula ng'ombe mzima kwa mara moja

Ni utaratibu wa kawaida kula kipande kimoja baada ya changine, hatimae ng'ombe mzima kuisha.

Tutajadili kitu kimoja baada ya chengine hatimaye kitabu chote kitaisha.

Issue ni quoting ya mstari then ukatoa maana yako. Sura nzima au ni katika muktadha upi ameongelea hilo?. Hiyo ndio italeta maana iliyokusudiwa.
 
Issue ni quoting ya mstari then ukatoa maana yako. Sura nzima au ni katika muktadha upi ameongelea hilo?. Hiyo ndio italeta maana iliyokusudiwa.

Hakuna kikao cha wewe, mimi na yule kukaa eti tutoke tafsiri ya pamoja.

Weka tafsiri yako nitakupinga kwa hoja

Nitaweka yangu utanipinga kwa hoja

Hiyo ndio maana sahihi ya mjadala.
 
Hapana shetani kamwe hawezi kugeuka kuwa malaika bali ana uwezo wa kujifanya kama malaika ili kuhadaa watu. La muhimu hapa ni kwamba tusimpuuze shetani anaposema kweli, tuangalie tu ukweli wake na tumwache na ushetani wake.
Shetani hawezi kusema ukweli kamwe kama unaona ni ukweli basi ujue ni mtego
 

Sawa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…