Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Mwl Nyerere ambae ni mwl wa Mkapa alishawishi Tanzania iingie katika mfumo wa vyama vingi, ni zamu ya mwanafunzi sasa kulivalia njuga hili hadi tume huru ya uchaguzi ipatikane!

Asiogope kunangwa, mara ooh mbona wewe ulikuwa hivi na vle...!
Hapo tutamuelewa, la sivyo tutajua anajikosha tu!...

Lakini yy kutokana na kitabu chake anajutia aliyoyafanya hajakataa kuwa hakukuwa na mabaya kwenye kipindi chake maana ya kitabu chaje ni kujutia
 
Brother p ujuwe huwaga sikuelewi kabisa IPO kama kinyonga au bendera fuata upepo
Mkuu Hito, pole!. Kwenye hoja hii, mimi nimeunga mkono hoja, unasema hunielewi, sasa hapa hunielewi nini?.
P
 
Kama nakosea Mungu anisamehe. Nachoamini huyu Mkapa ndio alimpora Maalim Seif urais wa Zanzibar.

Pili huyu ndio mwasisi wa ubavu ubavu na ubabe inakuwaje leo katoka madarakani na anaonekana kachoka ndio anatubu.

Kwanini asiwambie aliowaweka madarakani watende haki? Kwanini alazimishe kupendwa?
Hata kama ilikuwa hivyo, Wazungu kusema better late than never. Tungemlaumu sana mathalani katika uhai wake asikiri kuwa kuna upungufu kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan kwenye Ibara inayohusu muundo wa Tume ya Uchaguzi.

Kufanya kosa ni kitu kimoja ila kukiri kosa ni kitu kingine. Tuanzie hapo alipoishia BWM
 
Ku maintain status kwa sasa hivi ni shida ni vyema viongozi wetu wakubaliane na wananchi walio wengi kubadili katiba ambayo italeta uwazi na usawa katika chaguzi zetu.
 
Kawaida pesa na madaraka ukiwa huna unawaza mema ila ukipata unatenda tofauti. Ukikosa pesa utaomba uzipate uitunze familia vyema lkn ukizipata unawatuza mabarmaids nakuhonga wanawake familia utaikumbuka vikiisha
 
Vyama vya upinzani wala wasilikubali kuwe na Tume Huru wala kuhusishwa kwenye hiyo tume. Mkikubali tu, huo ndio utakuwa mwisho wenu wa kufanya siasa Tanzania.

Siku zote mmekuwa mkiwaaminisha wanachama na wafuasi wenu kuwa mnaibiwa kura. Na hicho ndicho kinawafanya waendelee kuwaamini. Sasa siku ikianzishwa hiyo tume na mkashirikishwa halafu mkashindwa. Mtawaeleza nini?
Umeongea kama yule Philosopher Paschal alivyowashauri wale Atheists wa Uingereza karne kadhaa nyuma.

Ila, in the moment of truth, ktk free and fair elections, hii ccm tunayoiona hii, haiwezi kushinda hata wakiachwa na Hashim Rungwe peke yake.

Sure I tell you. Na hizi figisu figisu anazofanya Magufuli usifikiri ni mjinga, tayari ramli wameshapigiwa kuwa his party has outlived its popularity na sasa kinaishi kwa nguvu za dola tu hali ambayo hawawezi kudumu nayo kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom