Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Kwanza aitenganishe CCM na serikali. Haiwezekani waziri wa Tamisemi ndiye msemaji na mpiga propaganda wa CCM, na Rais ndiye mwenyekiti wa CCM halafu hayo yawezekane.

Chama pia kijiendeshe kwa kutumia rasilimali za chama. Hali ilivyo sasa, mkutano wa chama na kampeni za CCM ni uporaji na ufisadi wa rasilimali za uma.

Lakini ni bahati mbaya sana kuwa Mkapa haongelei madhambi yake ya mauaji na uporaji wa chaguzi mbalimbali hasa huko Zanzibar.

Haya yanayotendeka ni mwendelezo wa alichoasisi mkapa na watu wake.
 
Vyama vya upinzani wala wasilikubali kuwe na Tume Huru wala kuhusishwa kwenye hiyo tume. Mkikubali tu, huo ndio utakuwa mwisho wenu wa kufanya siasa Tanzania.

Siku zote mmekuwa mkiwaaminisha wanachama na wafuasi wenu kuwa mnaibiwa kura. Na hicho ndicho kinawafanya waendelee kuwaamini. Sasa siku ikianzishwa hiyo tume na mkashirikishwa halafu mkashindwa. Mtawaeleza nini?
Si tutajua kuwa tumeshindwa kwa kuwa tulikuwa sehemu ya tume na tutaeleza kuwa tumeshindwa kwakuwa kura hazikutosha.
 
Huyu huyu aliyeita wapinzani malofa, shetani akizeeka hutamani kuwa malaika, ila haisahaulishi kuwa ni ukoo wa shetani!!
 
Na hii ndio aina ya Watawala wa Bara la Afrika ,hata Baba wa Taifa hili alijutia Katiba mbovu aliyo itumia katika Utawala wake wakati alikuwa na Mamlaka/Nafasi ya kuirekebisha.
Umenena vyema.
 
Mhe. Mkapa apumzike atuachie haya mambo tudeal nayo mbele kwa mbele. Yeye hakuona hivyo toka akiwa madarakani au wakati akikabidhi nchi kwa Mkwere? Alishasema wanaounga upinzani ni malofa. Tafadhali asitake kutonesha vidonda vya watu huku akijua hatuwezi kumfanya kitu maana ana uhakika na ulinzi wake.
 
Kuna siku yaja, huyu wa sasa naye atakuja kunena, 'natamani kama tungekuwa na sheria inayowazuia watawala kuwatumia wasiojulikana kuteka, kutesa na kuua raia; na inaoyozuia wanasheria ambao kazi yao ni kuwabambikizia kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha watu tunaotofautiana nao'

Tunajiuliza sana, hivi ndani ya CCM kuna nini hasa? Maana ukiwa humo inaonekana utu unapotea, akili zinaondoka, huoni wala kufikiri, uzalendo wa kweli unakukimbia; uwongo, ulaghai na unafiki vinakuzunguka kila kona. Ukitoka tu unapambazuka na kurudiwa na akili zako. Ina maana CCM ni shetani gani hata afifishe kabisa ufahamu wa kila anayekuwemo ndani yake?
 
Tanzania tunaitaji haraka sana vitu vikuu viwili tuu ; katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ,

Uoga wa Wananchi,Wanaharakati na Wapinzani katika kuvipigania hivyo vitu ndiyo umekuwa mtaji mkubwa wa ccm kufanya watakavyo.

Kwa kushindwa kuvipigania hivyo vitu viwili ni wazi kabisa utawala bora,uwajibikaji, uwazi na haki katika nchi hii vitakuwa ni ndoto.

Hayo yote ni kwa faida ya Usalama wa Taifa letu na siyo Usalama wa Serikali.
 
Back
Top Bottom