Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Vyama vya upinzani wala wasilikubali kuwe na Tume Huru wala kuhusishwa kwenye hiyo tume. Mkikubali tu, huo ndio utakuwa mwisho wenu wa kufanya siasa Tanzania.

Siku zote mmekuwa mkiwaaminisha wanachama na wafuasi wenu kuwa mnaibiwa kura. Na hicho ndicho kinawafanya waendelee kuwaamini. Sasa siku ikianzishwa hiyo tume na mkashirikishwa halafu mkashindwa. Mtawaeleza nini?
Haya ni mawazo mgando ndugu yangu badilika Taifa liishi Kwa ukweli
 
Umeongea kama yule Philosopher Paschal alivyowashauri wale Atheists wa Uingereza karne kadhaa nyuma.

Ila, in the moment of truth, ktk free and fair elections, hii ccm tunayoiona hii, haiwezi kushinda hata wakiachwa na Hashim Rungwe peke yake.

Sure I tell you. Na hizi figisu figisu anazofanya Magufuli usifikiri ni mjinga, tayari ramli wameshapigiwa kuwa his party has outlived its popularity na sasa kinaishi kwa nguvu za dola tu hali ambayo hawawezi kudumu nayo kwa muda mrefu.
Nimetoa ushauri lakini. Na najua sikio la kufa ....!
 
Bora adui mwenye busara kuliko rafiki mpumbavu.
Che Mkapa anaoa mbali sasa ni bora apiganie amani ya nchi yetu!!
Kuna majamaa wanaona chaka kavu wanatamani kupiga kiberiti tuungue.
Ahsante mzee wa busara na wengine watie neno, Tanzania ni yetu wote!!
 
Kama nakosea Mungu anisamehe. Nachoamini huyu Mkapa ndio alimpora Maalim Seif urais wa Zanzibar.

Pili huyu ndio mwasisi wa ubavu ubavu na ubabe inakuwaje leo katoka madarakani na anaonekana kachoka ndio anatubu.

Kwanini asiwambie aliowaweka madarakani watende haki? Kwanini alazimishe kupendwa?
Ndio zao mkuu.Wakati ule alijua tume huru inaweza kumnyang'anya urais,kwa sasa anajua sio dili,kwa hiyo ikiwepo sawa tu.
 
Vyama vya upinzani wala wasilikubali kuwe na Tume Huru wala kuhusishwa kwenye hiyo tume. Mkikubali tu, huo ndio utakuwa mwisho wenu wa kufanya siasa Tanzania.

Siku zote mmekuwa mkiwaaminisha wanachama na wafuasi wenu kuwa mnaibiwa kura. Na hicho ndicho kinawafanya waendelee kuwaamini. Sasa siku ikianzishwa hiyo tume na mkashirikishwa halafu mkashindwa. Mtawaeleza nini?
Kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na tume huru mkuu?? Hii itakuwa ni ajabu
 
Aliyewaita wapinzani malofa ni nani, mbona anatonesha maumivu angetulia alee wajukuu ashatuletea majanga atuache tupambane nayo.
Sasa malofa wataruhusiwa vipi kukaa meza moja kuhesabu kura
Nadhani kauli ya kuwaita wapizani malofa ilitokana na hasira za mwenyekiti J K kuimbiwa kale ka wimbo tunaimani EL
 
Bams,
Kuna post Pascal kaandika kwamba ukiwa ndani ya box huoni yaliyo nje. Ukishatoka ndiyo anayaona ya nje. Ndani ya hili box linaloitwa CCM hata angeingia malaika lazima atageuka na kuwa shetani mpaka atakapotoka humo ndio atarudi tena kuwa malaika.

Hali hii ni kwa Sababu ya aina ya Katiba tuliyo nayo kutoa Madaraka Makubwa kwa aliye kikalia Kiti.Wataendelea tu kufanya wanavyo taka iwe na itakuwa.
 
Na hii ndio aina ya Watawala wa Bara la Afrika ,hata Baba wa Taifa hili alijutia Katiba mbovu aliyo itumia katika Utawala wake wakati alikuwa na Mamlaka/Nafasi ya kuirekebisha.

Katiba hiyo mbovu iliwekwa hivyo makusudi kwa dhamira njema na matarajio kuwa busara kubwa itatumika kuepusha matumizi mabaya ya madaraka. Dhamira ilikuwa kuwezesha ujenzi wa utaifa. Sasa tumefikia mahali hata kipofu anaona matumizi mabaya sana ya hayo madaraka. Badala ya kutmika kudumisha na kuimarisha utaifa sasa madaraka hayo yanatumika kudhibiti washindani wa kisiasa.

Yaani kulinda wenye madaraka ya kisiasa kwa sasa dhidi ya wenzao wanaotamani nao kushika hayo madaraka. Pamoja na ubovu wake kwa mfano, hiyo hiyo katiba mbovu kuna mambo imekataza lakini hata hayo bado yanakiukwa. Kwa kifupi kiongozi amekuwa ndiye katiba!

Katika hali kama hiyo mtu makini aliyepata kushika madaraka katika nchi hii dhamira itamsuta kwa sababu atakuwa amechangia katika uharibifu huu wa nchi. Bila shaka yoyote mtu mwenye upeo mkubwa kama Mkapa hawezi kupata amani kuona mihimili kama Bunge na Mahakama inatumika kwa maslahi ya kisiasa ya watawala badala ya maslahi ya nchi. Hivyo ndivyo ninavyotazama haya mawazo ya Mzee Mkapa.
 
Naunga mkono hoja. Now Mkapa the wise one.
P

May be. Lakini nadhani kubwa zaidi ni kwamba mambo yameharibika kwa kasi kubwa mno. Nani alitarajia kuwa nchi hii itakuwa na chaguzi kama zile za kuunga mkono juhudi au hizi za serikali za mitaa.
 
Mnyanyembe wa Mboka,Usihukumu sana mkuu, kuna mambo ambayo ungekuwa wewe pengine hungeona best possible options zaidi ya zilezile alizochukua bwana Mkapa. Kumbuka maamuzi mengine hakufanya yeye kama yeye bali alikuwa na timu ya washauri. Mambo mengine ni magumu sana, ni rahisi kuropoka uliwa nje ya uwanja lkn ukiwa ndani unaweza cheza vibaya kuliko mchezaji uliekuwa ukimdhihaki
 
Anajaribu kunawa Lakini kamwe mikono yake haijawahi kutakata! Dhamiri inamsuta. Iweje leo awakumbuke MALOFA! Tena aliwaita MALOFA kipindi cha uchaguzi. Kuna njia moja tu ya kujisafisha, ni kuomba msamaha! Vinginevyo atanawa pipa zima la maji Na mikono yake Itabaki kuwa michafu! Ni mwasisi wa sheria Mbovu ya madini iliyomgharimu Sana mkuu wa sasa kuibadilisha, Tunamshukuru Mungu mkuu wa sasa amefanikiwa kuibadilisha!
 
Wazungu wamefanikiwa sana kwenye uongozi sababu uwasikiliza watu, hushaurika, huwatumia watu kama kioo kujitathmini, wameruhusu uhuru wa habari wameruhusu kukosolewa ili wajisahihishe, Waafrika ni kinyume. Utachezea risasi.
 
ukiona mtu anatubu na aonekane mtu mwema mbele ya jamii ana maswaibu makubwa yanamzonga yamkini israeli anamwita
Kwa nini sasa? kaona nini ambacho kipindi cha hapo nyuma hakukiona? teh,teh,teh.
Can't imaging Magufuli saying the same come 2030s.
Sipati mfano wake akiicha haya madaraka na yeye si hiyo copy ya hicho kitabu kapewa anaona Mzee mzima anavyoungama midhambi yake kiaina yeye itakuaje na mizigo kibao aliyonayo kwa mgongo wa rais wa masikini.
 
Back
Top Bottom