TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Sad indeed. Pumzika kwa amani baba. Ulikuwa mzalendo na mwenye mapenzi mema sana kwa nchi yetu. Mungu akupe pepo njema mzee wetu.
 
Duuh! huyu ndiyo alikua na nguvu yaani kama baba wa Taifa, sasa duuuh!
 
Sad indeed. Pumzika kwa amani baba. Ulikuwa mzalendo na mapenzi mema sana kwa nchi yetu. Mungu akupe pepo njema mzee wetu.
 
Kwanini unatokwa povu zito kuhusu swali rahisi kabisa kuhusu chanzo cha kifo? Duh! Baadhi ya Wabongo noma sana mtu anataka kuanzisha ligi kwa swali rahisi kabisa ambalo Watanzania wengi kama siyo Walimwengu wataliuliza!!! 😳😳😳
Hakuna hata matonye ya povu hapo.
Binafsi, Chanzo cha kifo cha mtu mwenye umri wake sio muhimu. At some point ilikuwa lazima afe kama sie wengine tutakavyokufa.

Sidhani kama kuna mtu asiye mwanafamilia aliyeumia kiasi kwamba, akijuzwa chanzo cha kifo chake, kitamsaidia kudeal na majonzi yake.
Sema kama kupata topic yakuongelea na kutengenea conspiracy theories jinsi wanamitandao tulivyozoea, sishangai wapo wanaosubiri kujuzwa chanzo chake, ili na wao watoe ujuzi wao juu ya hili.
 
Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiun(Sote ni wa Mungu na sote kwake tutarejea)

Hii ndio kauli tuliyofundishwa na imani yetu pale tupatapo misiba.

Hakika kila jambo huwa na sababu lkn bado mauti kwa kila mmoja wetu ni jambo la faradh (lazima), tumefundishwa kuwa, kullu nafsin dhaaiqatul mawt ( kila nafsi itaonja umauti)

Tusijisahau kutafuta makosa na sababu ya vipi mtu au watu hufa na kujisahaulisha kuwa kumbe kifo ni lazima kwa kila mmoja wetu.

Ni jambo la muda tu kufika, iwe umeumwa ndio sababu ya kifo chako au umepata ajali au, au, au mauti(kifo) yatatakufika tu. Kubwa ni kujiandaa kwa wale wenye Imani kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa.

Mungu amuweke Mzee wetu anapostahili.
 
FB_IMG_1595543230441.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom