Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiun(Sote ni wa Mungu na sote kwake tutarejea)
Hii ndio kauli tuliyofundishwa na imani yetu pale tupatapo misiba.
Hakika kila jambo huwa na sababu lkn bado mauti kwa kila mmoja wetu ni jambo la faradh (lazima), tumefundishwa kuwa, kullu nafsin dhaaiqatul mawt ( kila nafsi itaonja umauti)
Tusijisahau kutafuta makosa na sababu ya vipi mtu au watu hufa na kujisahaulisha kuwa kumbe kifo ni lazima kwa kila mmoja wetu.
Ni jambo la muda tu kufika, iwe umeumwa ndio sababu ya kifo chako au umepata ajali au, au, au mauti(kifo) yatatakufika tu. Kubwa ni kujiandaa kwa wale wenye Imani kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa.
Mungu amuweke Mzee wetu anapostahili.