Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Inategemea na account uliyofungua, kila account ina makato yake, ukienda kufungua account waambie nataka kufungua aacount ambayo makato yake ni madogo kuliko account zote.
Uzuri wa Barclays unapokea fedha kutoka paypal na unazitoa kabisa kwenye ATM, benki nyingine hazina hiyo huduma, ni Barclays peke yake nchi nzima ndiyo mwenye hiyo kitu.
Mh...kweli hayo? Ecobank wana CashXpress unavuta tu pesa yako toka paypal na waweza kuweka paypal pia toka CashXpress.
 
Bank gani nzuri kwa fixed account,nataka niweke visent vyangu.
 
Standard Chartered Bank! Nina Account uko, Jamaa hawana njaa kabisa sina ninchokatwa zaidi ya malipo ya kutoa hela kwenye ATM tu, Cheque Book bure na hata ukipoteza kadi unatengenezewa bure bila charge zozote.
Hawa jamaa nawakubali sana
Mwingereza huyo, watu wanasema Standard Chartered ina huduma nzuri kuliko hata mwingereza mwenzie Barclays.
Ina maana huchajiwi kabisa monthly charges?, kama unachajiwa kiasi kidogo unachajiwa sh. ngapi?, na account unayotumia inaitwaje?
 
Kwa uelewa wangu mdogo wa mabenki, karibia kila benki ina aina ya akaunti ambayo haina makato kabisa kama utakubaliana na masharti yake. Standard chartered wana akaunti inaitwa TAJIRIKA hii akaunti haina makato ya mwezi, lakini ina masharti wakati wa kutoa. Kama utatoa mara moja ndani ya miezi mitatu, ukienda kinyume makato yatakuwepo kama penalt. Akaunti kama hii ipo karibia kila benki ni majina tu yanatofautiana na features zinabadirika kidogo. Ecobank wao wanaiita Supersaver haikatwi chochote kwa mwezi na unaruhusiwa kufanya withdraw moja kwa mwezi, ukizidisha wanakulima penalt. Ushauri wangu kwa anaetaka kufungua, afanye window shopping kwanza, maana akiuliuza humu ataambiwa tu jibu jepesi kuwa fungua benki fulani,kumbe huyo mtu yuko na interest na benki hiyo lakini ki uhalisia atakutana na makato ambayo ni hiden.
Kuna akaunti hazina makato ya mwisho wa mwezi lakini kuna transactin fee, kwa hiyo kuna ambao hawafanyi sana transaction atakuambia haina makato,kumbe wewe ni mtu wa transaction halafu ukajuta.
 
nenda BARCLAY'S BANK monthly maintenance fee ni ndogo na kutoa hela kwenye Atms ni 600 tofaut na mwengine wanakata 800

Yaani hii ya kuchaji hela ya ATM inashangaza sana. Ukikaa foleni wanakata hela, ukitumia ATM wanakata hela, hivi maana yake ni nini?
 
Monthly fee ndogo ni kiasi gani? Tusaidie tuijue na sisi.
Alishasema kwenye comments zake zilizopita, amesema kwamba Barclays makato yake kwa mwezi ni 2,500/=, ila hakutaja hayo makato ni ya account gani. Ngoja aje atuambie hayo makato ni ya account gani.
 
Standard Chartered Bank! Nina Account uko, Jamaa hawana njaa kabisa sina ninchokatwa zaidi ya malipo ya kutoa hela kwenye ATM tu, Cheque Book bure na hata ukipoteza kadi unatengenezewa bure bila charge zozote.
Hawa jamaa nawakubali sana
Nakushauri ufanye review ya bank statement yako, SCB sio charity organisation kama unavyofikiri. Haijawahi kutokea SCB upoteze ATM ukapewa bure!!! Haitatokea Cheque book wakupe bure. Akaunti yako itakuwa kwenye bundled fee charges! Kati ya mabenki ambao yako smart kwenye kurecover charges ni SCB. Naongea nikiwa naijua vizuri,si kwa kuwa mteja bali ni kuwa mfanayakazi wake. Wako vizuri sana nakubaliana mfano kwa customer service ni excellent! Lakini bure bure hawana! Na hata ukichajiwa unafurahia makato sababu ya huduma zao nzuri!
 
Yaani hii ya kuchaji hela ya ATM inashangaza sana. Ukikaa foleni wanakata hela, ukitumia ATM wanakata hela, hivi maana yake ni nini?
Wasipokucharge watajiendeshaje? ATM machine wanalipia, ukiingia ndani wanakucharge pesa nyingi kwa sababu unawaongezea kazi,wamekupa ATM card ili upunguze foleni ndani na ndio maana makato ya ATM ni kidogo zaidi ya kuingia ndani.
 
Kuna hawa EcoBank nmekutana nao jana wanasema wanatoza 1% kwenye kutoa ktk ATM ila sijajua makato yao ya mwezi na gharama nyingine.. nahis watakuw wazuri
 
Mh...kweli hayo? Ecobank wana CashXpress unavuta tu pesa yako toka paypal na waweza kuweka paypal pia toka CashXpress.
Teknolojia inakuwa, siku za mbele kila benki kupokea pesa kutoka paypal litakuwa ni jambo la kawaida.
Hiyo account ya Ecobank ya CashXpress ni nzuri sana, Barclays walikuwa wanajivunia wao tu ndiyo unaoweza kupokea pesa paypal, sasa siyo benki moja tena unayoweza pokea pesa toka paypal. Pengine kuna baadhi ya benki nyingine unaweza pokea pesa toka paypal, tusubiri tuone comments za mbele.
Una account ya kawaida Ecobank?, makato sh. ngapi kwa mwezi?, na hiyo account ya CashXpress makato sh. ngapi kwa mwezi?
 
Kuna hawa EcoBank nmekutana nao jana wanasema wanatoza 1% kwenye kutoa ktk ATM ila sijajua makato yao ya mwezi na gharama nyingine.. nahis watakuw wazuri
Hiyo itakuwa akaunti yao mpya inaitwa Express account, ukiwa na smart phone unadownload application yao ya ecobank unafungua akaunti wewe mwenyewe, haina ATM card ila ukitaka kutoa pesa unaweza kuihamia mpesa,tigo pesa au airtel money na unaweza kugenerate Token ambayo utatumia kutoalea pesa kwa ATM zao kwa card less. Hawa jamaa wana product nzuri mno ila nafikiri hawajitangazi sana. hiyo akaunti ni nzuri sana,sana sana kwa wanafunzi wa vyuo. Ni rahisi maana haina milolongo mara kwenda kwa mwenyekiti sijui kupata utambulisho. Ni wewe na smart phone yako unamalizana na akaunti.
 
Wasipokucharge watajiendeshaje? ATM machine wanalipia, ukiingia ndani wanakucharge pesa nyingi kwa sababu unawaongezea kazi,wamekupa ATM card ili upunguze foleni ndani na ndio maana makato ya ATM ni kidogo zaidi ya kuingia ndani.

Basi tu nikutokana na kutokuwa na taratibu nzuri za kujali haki za wateja, kuna benki hazi chaji ATM kwani ni huduma ya kuwasaidia wao kupunguza foleni. Kuna maeneo mengi sana ya wao wanakata hela kuweza kujiendesha.
 
Kwani Barclays ipo mpaka leo hapa Tanzania?, si' nasikia imesitisha huduma zake?
Kwa mwezi unakatwa sh. ngapi ya makato?
ELFU 10000
Kwa sababu kila mmoja anamiliki account ya kampuni moja au mbili, itakuwa ngumu huyu mmoja kutoa jibu kwa mabenki yote.
Naomba kila mmoja aseme anatumia benki gani na aseme kwa mwezi anaona makato ya sh. ngapi. Wakishataja wengiwengi, tutapata majibu kwamba benki gani ina makato kidogo kwa mwezi.
Haya sasa, njoo, useme unatumia benki gani, na unakatwa sh. ngapi kila mwezi.
 
Mambo kama haya watu hawayadadavui..ila ikiletwa mada ya mapenz,saivi uzi ungekuwa wa page kama 100..

Natumia crdb makato yake sio mchezo,si kushauri sana kuitumia
CRDB makato kwa mwezi ni 1888 ATM 944 SIM BANKING hii waweza toa ela kwenye account yako kwenda mtandao wowote wa simu 2360 kuangalia salio kupitia simbanking ni 354
 
ELFU 10000
Kuna mwingine kasema anachajiwa 2,500/=, nafikiri account yako na yake ni tofauti, ndiyo maana mnachajiwa gharama tofauti.
Hiyo account yako unayochajiwa sh. 10,000 Barclays inaitwaje?
 
CRDB makato kwa mwezi ni 1888 ATM 944 SIM BANKING hii waweza toa ela kwenye account yako kwenda mtandao wowote wa simu 2360 kuangalia salio kupitia simbanking ni 354
1,888/= na 2,360/= ni makato gani?
Na ni makato ya account gani?
 
Hiyo itakuwa akaunti yao mpya inaitwa Express account, ukiwa na smart phone unadownload application yao ya ecobank unafungua akaunti wewe mwenyewe, haina ATM card ila ukitaka kutoa pesa unaweza kuihamia mpesa,tigo pesa au airtel money na unaweza kugenerate Token ambayo utatumia kutoalea pesa kwa ATM zao kwa card less. Hawa jamaa wana product nzuri mno ila nafikiri hawajitangazi sana. hiyo akaunti ni nzuri sana,sana sana kwa wanafunzi wa vyuo. Ni rahisi maana haina milolongo mara kwenda kwa mwenyekiti sijui kupata utambulisho. Ni wewe na smart phone yako unamalizana na akaunti.

Yah ni nzuri mkuu nimefungua tayari na haina makato ya mwezi..
 
Teknolojia inakuwa, siku za mbele kila benki kupokea pesa kutoka paypal litakuwa ni jambo la kawaida.
Hiyo account ya Ecobank ya CashXpress ni nzuri sana, Barclays walikuwa wanajivunia wao tu ndiyo unaoweza kupokea pesa paypal, sasa siyo benki moja tena unayoweza pokea pesa toka paypal. Pengine kuna baadhi ya benki nyingine unaweza pokea pesa toka paypal, tusubiri tuone comments za mbele.
Una account ya kawaida Ecobank?, makato sh. ngapi kwa mwezi?, na hiyo account ya CashXpress makato sh. ngapi kwa mwezi?
CashXpress ni prepaid card, haina makato ila ni pale unapoitumia ndipo unakuwa charged. Na unaweza kuitumia kwa online purchase pia.
 
Back
Top Bottom