Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaanika Application 69 zilizofungiwa kwa utoaji mikopo kidijitali bila leseni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi 'Applications" zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu tarehe 27 Agosti, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

Pia, Soma:
Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Kupitia taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu Umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi "Applications" zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali;
Snapinsta.app_467740930_1096011921898029_9130454150160145278_n_1080.jpg

Snapinsta.app_467738818_925613839011749_1043893919364520484_n_1080.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa ikielezea kwamba imebaini kuwepo kwa majukwaa na programu tumizi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila kuwa na leseni au idhini kutoka kwa Benki Kuu.

Hali hii inahatarisha usalama wa wateja na ustawi wa sekta ya kifedha, kwani majukwaa haya yanashindwa kutimiza matakwa ya Mwongozo wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili kwa mwaka 2024.

Mwongozo huu, uliozinduliwa tarehe 27 Agosti 2024, unalenga kuimarisha usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha nchini na kuhakikisha watekelezaji wa kanuni zinazolinda wateja.

S1.jpg


s2.jpg

Hii inajumuisha uwazi katika utoaji wa huduma, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na kulinda faragha ya taarifa binafsi za wateja.

Benki Kuu imefafanua kwamba majukwaa na programu tumizi zinazohusishwa na utoaji wa mikopo kidijitali ambazo hazijapata kibali kutoka kwa Benki Kuu haziruhusiwi kuendelea na shughuli hizo.

Hivyo, inatoa wito kwa umma na wadau wote kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda haki za wateja na kuhakikisha sekta ya fedha inafanya kazi kwa uwazi na kwa maslahi ya wote.
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa orodha ya Majukwaa na Programu Tumizi 'Applications 69 zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka BOT.


Katika taarifa iliyotoa kwa umma, BOT imesema majukwaa na programu hizo hazijakidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 walioutoa Agosti 27 mwaka huu (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2


Microfinance Service Providers, 2024).


"Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa


Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao," imeeleza taarifa hiyo.
IMG_1739.jpeg
IMG_1740.jpeg
 
DAR-ES-SALAAM: BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa orodha ya Majukwaa na Programu Tumizi ‘Applications 69 zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka BOT.

Katika taarifa iliyotoa kwa umma, BOT imesema majukwaa na programu hizo hazijakidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 walioutoa Agosti 27 mwaka huu (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

“Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao,” imeeleza taarifa hiyo.

-#Orodha ya applications hizo ni kama zinavyooneshwa hapo chini,
FB_IMG_17321850422638673.jpg
 
Kwahy kama ulikopa ndo itakuwa gia ya kutokulipa?
Inawezekana,kuna jamaa aliwahi kunipa stori sijui kama ilikuwa na ukweli au ilikuwa chai wajuzi watatia neno, ni muda kidogo ilikuwa 2016 PBZ ilikuwa inakopesha kwa riba ndogo sana, wafanyakazi wakaanza kumiminika huko sasa sijui Benk nyingine wakaweka figisu masuala ya ushindani PBZ wakafuatiliwa wakakutwa vibali vyao havipo sawa wakafungiwa kukopesha, jamaa waliokopa walijikuta tu ghafla mshahara uneingia bila makato na paysleep imekuja nyeupe haina deni
 
Back
Top Bottom