Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaanika Application 69 zilizofungiwa kwa utoaji mikopo kidijitali bila leseni
Snapinsta.app_467643348_3005504132929993_4443511444619490263_n_1080.jpg

Snapinsta.app_468026372_1263485598693651_351666472821306841_n_1080.jpg
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa ikielezea kwamba imebaini kuwepo kwa majukwaa na programu tumizi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila kuwa na leseni au idhini kutoka kwa Benki Kuu.

Hali hii inahatarisha usalama wa wateja na ustawi wa sekta ya kifedha, kwani majukwaa haya yanashindwa kutimiza matakwa ya Mwongozo wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili kwa mwaka 2024.

Mwongozo huu, uliozinduliwa tarehe 27 Agosti 2024, unalenga kuimarisha usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha nchini na kuhakikisha watekelezaji wa kanuni zinazolinda wateja.

Hii inajumuisha uwazi katika utoaji wa huduma, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na kulinda faragha ya taarifa binafsi za wateja.

Benki Kuu imefafanua kwamba majukwaa na programu tumizi zinazohusishwa na utoaji wa mikopo kidijitali ambazo hazijapata kibali kutoka kwa Benki Kuu haziruhusiwi kuendelea na shughuli hizo.

Hivyo, inatoa wito kwa umma na wadau wote kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda haki za wateja na kuhakikisha sekta ya fedha inafanya kazi kwa uwazi na kwa maslahi ya wote.
 
Bora mtuokoe na kausha damu,kwani vichaa wamekuwa wengi sababu kausha damu
 
Imekula kwao sasa
HII NDIYO HASARA INAYO WEZA KUPATIKA POPOTE PALE AMBAPO SHERIA INAKIUKWA, UKIKIUKA SHERIA MOJA KWA MOJA UNAINGIA KWENYE KUKOSA UHALALI WA KUDAI CHOCHOTE KWA LOLOTE LINALOTOKEA, TUJIFUNZE KUFUATA TARATIBU HALALI TUACHE UBABAISHAJI HILI NI DARASA TOSHA KWA WABABAISHAJI, KIMSINGI KAMA HAUPO KIHALALI MAANA YAKE UNAIKOSESHA SEREKALI PASEE YAKE, INFACTS SIJUI KWANINI HAWACHUKULIWI HATUA?
 
Back
Top Bottom