Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaanika Application 69 zilizofungiwa kwa utoaji mikopo kidijitali bila leseni
Screenshot_20241121-213706.jpg
Screenshot_20241121-213714.jpg
 
BOT wamefanya jambo kubwa sana na linalostahili kupewa uzito wake hapa jukwaani.

Hatima BOT wameto orodha ya makampuni hayo leo tarehe 21/11/2024 ambapo ni makampuni yapatoyo 69.

Nawapongeza sana BOT japo wamechelewa.

Orodha hiyo kwa sasa inazunguka kwenye ma-group ya WhatsApp.

My take:
Hela za haya makampuni zilizoko kwenye mabenki(kama wanawake) zitaifishwe kabisa.
Afadhali!
 
Hizi application ni rasmi sasa zimepigwa marufuku na Benki kuu ya Tanganyika.. Kwa hiyo kuanzia leo yeyote atakayejaribu kuziendesha anatafuta kesi na Jamhuri. Watu walipigwa sana kwenye hii mikopo ya mtandaoni.. Na mtandao uliokuwa ukitumika kwa asilimia 99 ni Facebook.. Labda pengine kwakuwa huo kuna wajinga wengi sana

Kilichonishangaza kwenye hizi application ni kwamba kuna mfanano wa ajabu namna majina yake yalivyo.. Yaani ni kama vile ni Kazi iliyokuwa inafanywa na mtu mmoja.. Hebu jionee mwenyewe hapa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANΙΑ

BENKI KUU YA TANZANIA

21 Novemba 2024

TAARIFA KWA UMMA

ORODHA YA MAJUKWAA NA PROGRAMU TUMIZI "APPLICATIONS" ZILIZOFUNGIWA KUJIHUSISHA NA UTOAJI WA MIKOPO KIDIJITALI

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi 'Applications" zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitall wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu tarehe 27 Agosti, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Kupitia taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu Umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi "Applications" zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali;

1. BoBa-Cash

19. Hewa Mikopo

37. Bomba la Pesa

55. Soko Joan

2. Mkopo wa Kifedha wa Bolla Kash Bolla Kash

20. Hi Fedha

38. Mpaso chap loan Mkopo kisasa

56. Sunloan

3. BongoPesa-Personal Online Loan

21. HiPesa

38. Mkopo wa mama

57. Mkopo wa jua

4. Cash Mkopo

22 Jokate Foundation imarisha Maisha

40. Mkopo wangu

58. Mfuko Mwepesi

5. Pesa taslimu

23. КОРАНAPA

41. Nikopeshe App

59. TALA

6. Fedha poa

24. Mkopo wa Kwanza

42. Mikopo ya Nutaika

60. TwCash

7. CashMama

25. L-Pesa Microfinance

43. Okoa Maisha Mkopofast

61. Mkopo wa Twiga
 
Back
Top Bottom