HOJA Benki ya CRDB inatuhumiwa kuibia watu hela kwenye akaunti zao. BoT ipo Kimya

HOJA Benki ya CRDB inatuhumiwa kuibia watu hela kwenye akaunti zao. BoT ipo Kimya

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ninatumia crdb tangu 2009 sijawahi pata changamoto hiyo. Wao walijichanganya wakaniingizia 18m na ikadumu kwa wiki nzima. Wamekuja kusanda 3m imeenda! Ikiwa Kila pesa yangu ikiingia nafekwa niliishi kama shetani maana ndo account ya mshahara
😂😂😂 mi mwenyewe mshahara napitishia huko na kila mwezi huwa na Extract Bank Statement wanaituma kwenye Email moja kwa moja kwa kweli sijawahi kuona muamala wa kuibiwa zaidi wana makato makubwa sana ukitoa kwa mawakala ila niligundua hilo ATM haziko mbali nami so now natoa kwa kutumia ATM nikiwa na Malipo makubwa naenda Branch
 
Kwa Nini benki ya selcom Ina huduma nzuri na makato kidogo lakini haifahamiki?
Kwa sababu Watanzania wana Ujinga mwingi.Hawajui kufanya Research.Mimi Primary Business Bankers wangu ni EQUITY BANK na Primary Personal Bankers wangu ni Selcom Microfinance.Benki za NMB na CRDB nazitumia kwa miamala midogo ya Binafsi na SIO ya BIASHARA Kabisa.Maana huwa nafuatilia sana kuhusu hizo Gharama zao na huwa sioni mantiki yoyote
 
Hili swala la Benki kukata hela kwenye akaunti ya mtu bila makubaliano si sawa. Wanatakiwa watoe taarifa kwamba kuna hela hii tutakata mwezi ujao.

Mtu unaweza pesa zako benki ukijua ni sehemu salama ukipatwa na shida ukaenda huikuti. So bora mtu angeiweka chini ya godoro tu?

Nashauri BoT ilazimishe benki zitoe taarifa kwa wenye akaunti kiasi wanachokata kwa mwezi. Na kisibadilike kwani mtu akitoa hela anakatwa pia.

Kumbuka CRDB ina wateja Milioni 7, wanachokata kwa kila mtu ni kikibwa sana ukizidisha kwa idadi ya wateja.

View attachment 3702135
View attachment 3702136
View attachment 3702137
View attachment 3702138
Mwaka jana waliwaibia sana wanafunzi
 
Back
Top Bottom