Benki ya Dunia inatarajiwa kuidhinisha mkopo wa $500M kwa Tanzania baada ya Tanzania kutoa utetezi wake

Benki ya Dunia inatarajiwa kuidhinisha mkopo wa $500M kwa Tanzania baada ya Tanzania kutoa utetezi wake

Watanzania au Watu weusi tuna vichwa vigumu sana, na vilivyojaa hewa...ingawa kuna tofauti kwa Watu hao hao weusi waliokwisha lowea huko nje mfano USA n.k.

Tunaposhauriwa tuwaache Mabinti wenye mimba wasome tuna re act moja kwa moja kwenye ujumbe husika, basi tutatoa mapovu na mwenye sketi ndio ataipandisha juu ali mradi aonekane anajali sana maadili.

Hakuna anayewaambia muendekeze mimba au ushoga shubamiti zenu....wenye akili wanawazuia kuwaadhibu mara ya pili wale waliokwishaathirika...tena wakati mwingine wanaathirika kwa matokeo ya uzembe wenu wenyewe kama Wazazi na Walezi.

Kama mtaweza kuzuia nchi isiwe na mimba mashuleni au nchi isiwe na mashoga kabisa basi mbona hilo ni kheri.

Lakini kinyume chake tumekuwa watu wa kuficha udhaifu wetu wa kuwajibika nyuma ya lawama, na Mtu mwenye tabia ya muda wote kutafuta wa kumlaumu huyo ni sawa na mzigo tu, usimtarajie kwa chochote cha maana kwa jamii yake.

Mamlaka na jamii kwa ujumla tumieni akili na busara mlizopewa na Muumba mabinti zenu wabaki salama muda wote badala ya kukimbilia kazi rahisi, kazi ya Mtu dhaifu, kazi ya kuadhibu tu.
 
The government must have made concessions to appease the global multilateral lenders to change course. That's for sure.

If the regime will renege on its pledge to the WB then the latter may cancel the deal wholesale thus ending the euphoria. No loan comes without strings attached.
 
Mpaka hapo umenikatisha tamaa kujadili na wewe, unataka kulinganisha changamto na vipaumbele vya mataifa mawili ambayo moja (USA) limetimiza karibu miaka 350 au 400 ya kuwa huru na lingine (Tanzania) lina miaka 60 ya uhuru?
Au moja (UK) lina miaka zaidi ya 600 ya uhuru na lingine (TZ) lina miaka 60?

Unajua kama nchi masikini sana kama Cuba ilikuwa inakopa pesa kuwekeza kwenye afya kiasi cha kushika nambari moja duniani kwa baadhi ya huduma za afya? Iliipita Marekani na nchi zote za Ulaya kwenye maeneo flani.

Kwanini haikukopa kuwekeza kwenye mambo ambayo Marekani ilikuwa inawekeza?
Sababu vipaumbele na changamoto ni tofauti.
Cuba haikua na matumizi yasiyo na kichwa wala miguu kama ya ndege. Unakopa kujenga shule huku unanunua ndege cash? Kwa nini usikope kununua ndege ukatumia cash kujenga shule na hospitali?

Ccm ya Tanzania hata ikipewa miaka 500 hakuna mahala tutaenda kwa sababu ya sera mbavu, hakina mbinu mpya ya kututoa hapa na kutupeleka mahala pengine.

Tumepata uhuru uchumi wetu na Indonesia, Malaysia na baadhi ya nchi za Asia Pacific ulikua sawa kabisa, leo hata robo ya uchumi wao hatufikii. Malaysia ukiwapa miaka 300 kama ya Marekani watakua sawa na Marekani ila Tanzania hata tupate miaka 500 hatuwezi kua kama Malaysia.

Miaka 60 ya uhuru bado tunakopa kulipa mishahara?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Trump apokea ujumbe wa Rais Magufuli, uchaguzi huru ukisisitizwa.
===

Dar es Salaam. W
aziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais John Magufuli kwa rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana kwa umma, ujumbe huo ulipokelewa kwa niaba ya Rais Trump na naibu waziri anayehusika na mambo ya nje kwa upande wa Afrika, Tibor Nagy jijini Washington.

Baada ya kupokea ujumbe huo, Nagy aliahidi kuwa Marekani itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania uliodumu kwa miaka mingi.

Ingawa ujumbe huo ulitolewa na waziri mwenye dhamana, haukuweka wazi kwa kina ni ujumbe gani aliowasilisha Rais Magufuli kwa Trump, lakini wakati akipokea ujumbe huo, walijadili umuhimu wa kudhibiti vitendo vya ukiukwaji haki za binadamu na kuimarisha mazingira ya kibiashara. Katika ukurasa wake wa Twitter jana, Nagy aliandika kwamba “Marekani inapokea ahadi ya Rais Magufuli katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki. Watanzania wanatarajia kwenda vituo vya kupiga kura Oktoba mwaka huu kuchagua Rais, wabunge na madiwani”.

Januari 22, Rais Magufuli aliahidi uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu utakuwa huru, wa haki na wazi. Alisema Serikali itaruhusu mashirika ya kimataifa na waangalizi wa uchaguzi kuja Tanzania kwa ajili ya kuufuatilia.

Ahadi hiyo ilitolewa katika kipindi ambacho vyama vya upinzani vilikuwa vikilalamikia uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kuwa wasimamizi waliwabagua, kuwanyima fomu za kugombea, na kuwaengua wagombea wap hali iliyosababisha vyama hivyo vijitoe.

Hali hiyo ilisababisha Marekani kutoa tamko la kutoridhika na uendeshaji uchaguzi huo.

“Marekani inasikitishwa na ukiukwaji wa taratibu katika uchaguzi wa Novemba 24,” ilisema Marekani katika taarifa yake ya Novemba 27 mwaka jana.

“Maofisa wa uchaguzi waliwaondoa wagombea wa upinzani katika mchakato wa uchaguzi. Mazingira haya yanayosumbua yanaweka maswali katika kuaminika kwa mchakato wa uchaguzi na matokeo.”

Katika uchaguzi huo, wagombea wa CCM walishinda kwa zaidi ya asilimia 98 kutokana na wapinzani wao kuenguliwa na hivyo sehemu kubwa ya uchaguzi kutohusisha upigaji kura.
 
Trump apokea ujumbe wa Rais Magufuli, uchaguzi huru ukisisitizwa Trump apokea ujumbe wa Rais Magufuli
Chezeya beberu wewe! Ohh China ndo rafiki wa kweli misaada yao haina mashariti, beberu katupia korona Kule wahangaika Mayo mpaka kesho, huku beberu anawacheka tu. Wale vibaraka waliokuwa wanategemea China hawana pa kushika zaidi ya kujisalimisha kwa beberu.

Waswahili husema usitukame mamba kabla ya kuvuka mto, magufuli aliongea shit nyingi sana dhidi ya beberu, beberu alikaa kimya tu

Sasa beberu anataka uchaguzi Huru na wa haki, na deokrasia, zile tambo zao sijui sisi ni dona kantri au sijui sisi ni sovereign country hatupangiwi sizisikii tena
 
Kwahiyo hatowaita tena lile Jina Beberu?
 
Haya mambo ya awamu zingine sio hii ya Magufuli.
Serikali sasa haikopi kulipa mishahara.
Mkuu uwe unajitahidi kusoma taarifa za serikali ndio uwe unabisha.

Taarifa za mkaguzi wa serikali hua zinatoa mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka husika.

Uwe unasoma bajeti, makusanyo, matumizi ya mishahara, matumizi ya malipo ya madeni ya nyuma na matumizi mengine kabla ya mikopo uone kabla ya mikopo hua tunajitosheleza kwa asilimia ngapi.

Vijana mjitahidi kusoma na kuchambua maandishi. Ukisubiri usomewe halafu utangaziwe kwenye mikutano ya wanasiasa ndio matokeo yale inakua kama hivi, unakuta unabisha bisha tu kama juha.
 
Back
Top Bottom