Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Mkuu Chige ,nilikuwa nafanya analysis ili niweke hapa maana halisi ya hiki kitu kwa lugha nyepesi,nashukuru hilo umelifanya kwa uhakika kile kinachomaanishwa na report hii.
Mungu akubariki sana.
Kongole mkuu.
Ambaye hataelewa maandisho yako,hakika huyo atakuwa "low - middle mind citizen".
 
Jmos kutakuwa na party la wazalendo kadhaa kusherehekea hii hatua muhimu ya kuwaumbua mbulukenge wa ufipa na ofisi yao kama godauni za pamba zilizotelekezwa
 
Mheshimiwa Rais na wataalamu wengine wa masuala ya uchumi, kwa niaba ya Watanzania wote tusio elewa nini maana ya nchi kuwa katika UCHUMI WA KATI tunaomba mtufafanulie ili wote twende sawa.

Leo tumeona mheshimiwa akipongeza kuhusu nchi yetu kuingia kwenye UCHUMI WA KATI ila kwa bahati mbaya watanzania tulio wengi hatujui hili linamaana gani.

Hivyo tunaomba ufafanuzi kidogo wa hicho kinacho itwa uchumi wa kati ndio nini na kinafanya nchi yetu kulingana na nchi zipi za mabeberu kiuchumi?

Ni ngumu kumwambia tu mwanachi wa kawaida huko chini kuwa nchi yetu ipo katika UCHUMI WA KATI wakati huo kila kukicha anaona bora ya jana. Pesa mtaani hakuna, maisha magumu, ajira kwa vijana hakuna hata za huko serikalini hazitoki na mambo mengine kama hayo.

Tunaomba ufafanuzi kidogo ili na sisi tuweze kuwaeleza wananchi kuhusu hilo pindi wanapo tuuliza huku mtaani.

Yote kwa yote hongera Tanzania kwa kufikia UCHUMI WA KATI.
Mods msiunganishe huu uzi
 
heshima kwako mkuu! Ahsante kwa kutufungua macho mimi na vilaza wenzangu
 
We jamaa bhana... za kupika wakati nimeweka link ya WB kabisa?! Hebu tumia hiyo source yako halafu niambie ni figure zipi nilizoweka ambazo ni za kupikwa?! Btw, unasema zimewekwa hadi za 2018, kwani mimi nimeweka hadi za mwaka gani?

Tatizo lako ulikuwa unalinganisha kwa miaka 5 ya JPM wakati huna figures za 5 years. I am sure figures za 2019 and 2020 zikitoka kutakuwa na mafanikio mazuri Zaidi, usiwe na haraka yoyote yataonekana tu. Kilicho chini ya jua hakijifichi.
 
heshima kwako mkuu! Ahsante kwa kutufungua macho mimi na vilaza wenzangu
Kilaza huwa haelewi Mkuu! Kama umefunguka macho ina maana umeelewa, na anayeelewa hawezi kuwa kilaza! Vilaza ni wale ambao hata baada ya kuwawekea data, wanaishia kutukana!!
 
Zitto DJ Mbowe na genge lake walikuwa wanasema uchumi umezikwa WB wanasema umepaa mpaka tumefikia uchumi wa kati kudadadeki, hii ni furaha kwa CCM ni msiba mzito kwa wapinzani maana October hii hapa.
Maisha yako hapo ulipo yamekuwa bora kiasi gani kwenye huo uchumi w Wb
 
Pamoja Chifu!!
 

Tena ikibidi tuwekewe link ya WB ili tujiridhishe na hiki kinachosemwa.
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya #Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150.🙏🏾
 
Unaelimu gan???
 

Kwani link sikuweka?
 
Hii ni hatua nzuri, pongezi kwa watanzania na serikali ya awamu ya tano. Watanzania tusibweteke, ni imani yangu serikali itakayoundwa baada ya uchaguzi itakuwa na watu makini sana ambao watakao tusaidia kusonga mbele zaid.
 
Nafikiri wastani unahusika, ukitafuta wastani Wa tofauti ya vipato lazima iwe hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…