Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Hongera kwa wote , kama Taifa tunakwenda vyema.
 
Kwa hiyo Upinzani mnapambana CCM au Magufuli? Kwa maana sielewi huku unamsifu Kikwete kwa kuiingiza nchi kwenye kipato cha kati na kumponda Magufuli, kwani Kikwete ni Chama gani?
 
Acha ufala Labda Mungu jiwe ila sio Mungu wa mbinguni.
Niambie gunia la mahindi sokoni ni shilingi ngapi na gunia la alizeti sokoni ni shilingi ngapi.
.
Pia niambie sukari kilo moja ni shilingi ngapi.
Ukimaliza tunahamia taifa jirani tu la Kenya hapo tuone maelfu ina nguvu kiasi gani kulinganisha na maelfu ya utopolo.
Wewe ndiye lofa mkuu, unauliza gunia la Maindi /alizeti, unataka kufungua duka? Mimi nazungumzia maisha ya kawaida ya uswahilini, mchele sasahivi sokoni hapa kawe kilo 1200-1500 chaguo lako, Maharage kilo 2000-2500 chaguo lako, unga kilo 1000 ', sukari kilo 1800, kibarua mtaani sh, 15000-20000,shuleni bure, kodi za nyumba zimeshuka, labda uwe mvivu ndio utashindwa maisha, wewe kaa hapo subiri Mbowe awe Rais akugaiwie pesa bure. Ila sisi huku uswahilini maisha raha tupu. Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki Rais Magufuli
 
Ama kweli mtaji mkubwa JPM ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake! And JPM anafanikiwa haya kwa sababu ile ile niliyowahi kuitaja siku za nyuma: Tanzania is full of people with average mind, and many more below the average!
Kabisa hawaanalyse mambo. Wanapokea kama yalivyo.
 
Nadhani kwenye shida na hapa "lower middle income"

So msifikiri tuna uchumi mzuri tunazidi kwenda shimoni sasa sijajua kama Mh Rais alitafsiriwa au alitafsiri mwenyewe.
 
Nchi ilishafika hapo since 2018, ww baki hapo na ubishi wako
Nchi ilishafika hapo since 2018
Ubishi wangu kwani mimi ndo naandaa data za WB?! Sasa wakati wewe unadai nchi ilishafika hapo since 2018, wenyewe WB wanasema hivi:-
2018.png

Sasa mimi na wewe mbishi hapo nani?!
 
Kwa hiyo Upinzani mnapambana CCM au Magufuli? Kwa maana sielewi huku unamsifu Kikwete kwa kuiingiza nchi kwenye kipato cha kati na kumponda Magufuli, kwani Kikwete ni Chama gani?
Sasa Mheshimiwa huoni maelezo yangu nimeanza kwa kauli "...huu ni ushahidi tosha kwamba JPM anavuruga uchumi!?" Au nikukumbushe kwamba in 2015 nilikuwa namuunga mkono JPM lakini nikaanza kuhitilafiana 2016 baada ya kuona anavyoivuruga sekta binafsi?!
 
Ubishi wangu kwani mimi ndo naandaa data za WB?! Sasa wakati wewe unadai nchi ilishafika hapo since 2018, wenyewe WB wanasema hivi:-
View attachment 1494677

Sasa mimi na wewe mbishi hapo nani?!
Tupo GNI per capita $1,063 ,siyo ya kuringia kutoka tulipokuwa $980 .Kumbuka JK alipandisha mpaka 720 mwaka 2010 kutoka kwenye $500 mwaka 2005.Mpaka hapa Magufuli hana maajabu yeyote.
 
Kila kitu ni hatua, hakuna sababu ya kubeza hatua hiyo moja, zingine zitafuata taratibu. Kumbuka tu kuwa nchi ni yetu sote, ikianguka hakuna atakayebaki salama.
 
Wewe ambaye uko above average mind umetusaidia nn....kwenye hili taifa....ushangae hata Kodi tu unakwepa!!? ......Hawa wajuaji wa mdomoni wanatuchelewesha Sana...
Mkuu Chige kazima ngebe na sherehe yenu, usicheze na watu wenye akili, Viva jf

Labda mkampe like jiwe huko twiter siyo huku kwa Ma GT
 
Sasa Mheshimiwa huoni maelezo yangu nimeanza kwa kauli "...huu ni ushahidi tosha kwamba JPM anavuruga uchumi!?" Au nikukumbushe kwamba in 2015 nilikuwa namuunga mkono JPM lakini nikaanza kuhitilafiana 2016 baada ya kuona anavyoivuruga sekta binafsi?!

OK kwa hiyo wewe siyo mpinzani bali tu haukubaliani na jinsi Raisi Magufuli anavyoendesha nchi? Kama ni hivyo basi hapo nimekuelewa kwa maana nilifikiri wewe ni mpinzani ndo maana ikawa inanichanganya kidogo, ...
 
Tupo GNI per capita $1,063 ,siyo ya kuringia kutoka tulipokuwa $980 .Kumbuka JK alipandisha mpaka 720 mwaka 2010 kutoka kwenye $500 mwaka 2005.Mpaka hapa Magufuli hana maajabu yeyote.
Dah! Ahsante, unajua nilikuwa kimya nikitafuta exact figure kwamba ni ngapi hasa! Sasa kama ndo kwanza $1063, an increase to less than $100, basi kwa speed hii tutafika 2030 lakini bado high middle income ikawa mbali sana kwetu kuifikia!!!
 
1593627068616.png

Inategemea hiyo graph unataka uisome vipi, uchumi wa Tanzania unapanda constant 2015; USD 980; 2016 USD 970 NA 2017 USD 970. Data za uchumi 2019, na 2020 hazipo kwenye graph. Hivyo sio sahihi kusema JMK alifanya zaidi ya JPM wakati data za JPM ni za miaka miwili tu.
 
Attachments

  • 1593625899982.png
    1593625899982.png
    3.5 KB · Views: 2
Kwa hiyo Upinzani mnapambana CCM au Magufuli? Kwa maana sielewi huku unamsifu Kikwete kwa kuiingiza nchi kwenye kipato cha kati na kumponda Magufuli, kwani Kikwete ni Chama gani?
Kikwete ni ccm asili Magufuli ni ccm mpya
 
Kenya leo awalali na awatakubali kweli pongezi kwetu sote kutoka least developed country kwenda middle income country sio jambo Dogo.
 
Back
Top Bottom