TANZANIA YAINGIA UCHUMI WA KATI KABLA YA LENGO LA DIRA YA TAIFA YA 2025.
Leo 21:15pm 01/07/2020
Kwa kadiri ya vigezo vya Benki ya Dunia uchumi wa kati una matabaka mawili makubwa. La kwanza ni lile la uchumi wa kati wa ngazi ya chini na la pili ni uchumi wa kati wa ngazi ya juu,
Kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa katika uchumi wa chini,chini ya hayo matabaka mawili niliyoyataja hapo juu,Sasa ukiwa Katika Uchumi wa chini kabisa lengo linapaswa kuwa kuelekea uchumi wa kati wa ngazi ya chini,hii ni hatua moja kutoka katika uchumi wa chini,
Baada ya kufikia uchumi wa kati wa ngazi ya chini ndipo tunapaswa kuelekea uchumi wa kati wa ngazi ya juu,Kufikia uchumi wa kati wa ngazi ya juu sio mwisho wa safari ya kwenda juu katika ngazi za uchumi kwa nchi.Ngazi inayofuata baada ya kufikia uchumi wa kati wa ngazi ya juu ni ile ya uchumi wa kipato cha juu.
Lower Middle income ama Uchumi wa kipato cha kati,ni sawa na kusema umepata shamba la kulima,trekta lipo na mvua inanyesha,Sasa tunatarajia utalima,utapanda mahindi au mpunga,utavuna utauza na utapata kipato kitakachokuwezesha kutumiza mahitaji yako na ziada,
Hapa tunaangalia miundo mbinu itayowezesha Mwananchi mmoja mmoja kupata kipato kitachomwezesha kula mlo kamili na kuweka hela ya akiba,Key word kwa hapa ni miundo mbinu itatotupeleka kwenye tokeo chanya.
Maendeleo ya vitu au watu ndiyo yanayopelekea kipato cha mtu kutosheleza mahitaji yale ya muhimu na ziada,Mfano Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji litalofagilia njia ya Ujenzi wa Viwanda vingi kutokana na uwepo wa nishati ya Umeme ya kutosha,
Hatimaye kuzalisha ajira na kuinua biashara kutokana na bidhaa tutazozalisha na kuingiza fedha ya kigeni na kuongeza mzunguko wa pesa na kumfikia kila mwananchi hivyo kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja,
Maendeleo ya vitu tunamaanisha uwepo wa miundombinu ya kufanikisha maendeleo, kama vile barabara na madaraja, reli, viwanja vya ndege na ndege, meli , vivuko, vituo vya afya, zahanati, hospitali, shule, walimu, na hata mifumo ya elimu isiyo malipo, Maendeleo haya ya vitu yatabaki kuwa ni uwekezaji muhimu kwa maendeleo ya watu.
Kipato ni mojawapo tuu ya vigezo vinavyotumika. Tabia nyingine za uchumi wa kati ni pamoja na maendeleo ya uchumi na teknologia, miundombinu, maendeleo ya viwanda, elimu, uwekezaji na kadhalika vilivyo juu ya uchumi wa chini lakini chini ya uchumi wa kipato cha juu.
Hivyo ni muhimu kwa wadau wote kuelewa njozi za kuelekea uchumi wa kati maana yake ni nini na tunatoka na kwenda wapi. Haya yasipofahamika tutakuwa tunasafiri kutoka na kwenda tusikopafahamu.
Kipato Cha mfukoni ni mchango wa mtu binafsi kwa nchi yake.Serikali inamtandikia miundo mbinu sahihi mwananchi, Kisha mwananchi kwa nafasi yake anachakarika kujiongezea kipato (Serikali haina uwezo wa kumfikia mwananchi mmoja mmoja na kumuwekea elfu kumi mfukoni kila siku).
Baada ya kipato cha mfukoni kuongezeka, kinachofuata ni mchango wa mwananchi kwa serikali yake;
1)Kulipa Kodi nyingi zaidi.
2) Kuajiri watu wengine wengi zaidi ambao nao watalipa Kodi.
3) Kuwekeza zaidi kutokana na serikali kuongeza ubora wa miundo mbinu ya kumwezesha huyu mwananchi azidi kuongeza kipato chake kutokana na Kodi inayokusanya kwake (it is a circle).
Jambo la msingi ni kuwa na jicho la kuiona hiyo miundo mbinu ambayo serikali inaitandika kama reli ya wananchi kupita kufanya shughuli zao za kuongeza kipato.
Swali na msingi la kujiuliza hapa, nini hujakifanyi mpaka kipato chako Cha mfukoni hakiongezeki!!!??.
This is lower Middle income after that we will come to Upper Middle income,Kwenye lower Middle Income ianaangalia vigezo vinne,
1-Uwezo wa nchi kupunguza umasikini kwa watu wake.
2-Uwezo wa nchi kukopesheka.
3-Uwezo wa nchi katika kupambana na maradhi kwa maana ya miundo mbinu ya afya kama hospitali,Madaktari na dawa.
4-Uwezo wa nchi katika kukidhi masuala ya elimu na kuondoa ujinga.
Kitakwimu kinachotakiwa ni kuongeza vipato ili wastani wa sasa uweze kupanda. Ni muhimu kuelewa kuwa wastani unakusanya mapato ya watu wote na kugawanya kwa idadi yao.
Bila shaka wapo wenye vipato vikubwa sana, vya kati na vidogo sana. Ili kufikia wastani wa juu wa vipato inabidi kuongeza vipato kwa kasi kubwa hata mnyonge,masikini awe na kipato cha kutimiza mahitaji yake na ongezeko la kipato liwe zaidi ya idadi ya watu.
Kiini cha uchumi wa kati ni kujali maslahi ya watu walio na vipato vidogo,Rais John Magufuli ametembea na wanyonge wenye vipato vidogo kwa miaka mitano ya muhula wake wa kwanza wa Urais kuongeza vipato vyao sambamba na vile vya wenye vipato vya kati na vya juu.
Mh Rais John Magufuli ana kipaji cha kuona sungura na bata kwa wakati mmoja,kiuongozi ana uwezo wa kumwona tajiri na masikini kwa wakati mmoja na wote wakapata haki sawa,kwa kuwajengea miundo mbinu wezeshi kwa kila mmoja kuweza kujipatia kipato,
Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana,Hivyo, inahusu uwezo wa kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.
Maendeleo ya vitu au watu ndiyo yanayopelekea kipato cha mtu kutosheleza mahitaji yale ya muhimu na ziada,
Maendeleo ya vitu tunamaanisha uwepo wa miundombinu ya kufanikisha maendeleo, kama vile barabara na madaraja, reli, viwanja vya ndege na ndege, meli , vivuko, vituo vya afya, zahanati, hospitali, shule, walimu, na hata mifumo ya elimu isiyo malipo, Maendeleo haya ya vitu yatabaki kuwa ni uwekezaji muhimu kwa maendeleo ya watu.
Lower Middle income ni sawa na kusema umepata shamba,trekta na maji yanatiririka masaa ishirini na Sasa tunatarajia utapanda hata miwa na magimbi ukishindwa kabisa kujiongeza kupanda mahindi au mpunga ili uweze kujipatia kipato,
Hapa tunaangalia miundo mbinu itayowezesha Mwananchi mmoja mmoja kupata kipato kitachomwezesha kula mlo kamili na kuweka hela ya akiba,Key word kwa hapa ni miundo mbinu itatotupeleka kwenye tokeo chanya.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.
-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.