Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati


Naona Tangazo tumetoa wenyewe na Kadiri ya taratibu za referencing ingetakiwa aweke link ya mtandao wa WB uliotusifia na aweke Ameusoma muda gani ( accessed)
 
Hivi ukienda kwenye kampeni ukawaeleza watu kuwa nchi yetu imefikia uchumi huo watakulewa wakati hawana maji,umeme,madawa hospitalini,mishahara duni,madeni ya ndani hayalipwi,n.k?


Kwenye kipindi hiki kigumu hivi.
Hakuna biashara, watoto wanarudi shule miili imekuwa mikubwa baadhi ya wazazi hawana hata pesa ya kuwanunulia nguo size zao, madeni kila mahali na huko unasikia uchumi umepanda kwenye makaratasi my foot!!!!!
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150-Fatma Karume on twitter
 

Dah! Umemwaga upupu mpaka aibu! Hivyo, huko shule mnajifunza ujinga?
 
Kwahiyo unataka kusemaje hapo mkuu.
 
Magu amesha-tweet kwa 'kidhungu' kushukuru!!

Tusubiri magazeti ya kesho na heading watazokuja nazo.

Wakiona watu wanafanya uchambuzi kwa kutumia data mitandaoni,wanatamani wawamalize maana wanaharibu uhundo!!
Hiki ni choo cha walimu wa masasi , ndani ya nchi yenye uchumi wa kati .
 
Patna wako Zitto Ruyagwa Kabwe mbona kimya?
 
Kagemro

Anyamaze watu wazidi kulishwa ujinga? Boss, Karne hii bado unajivunia watu kuongozwa kama vipofu kwa kulishwa propaganda? Halafu unaandika kiswahili na kuchanganya na kiingereza ili uonekane ni msomi, huku ukitetea watu waongozwe bila kujua ukweli!
 
Hawa Chadema kwanini wanapinga kila kitu? Kwanini serkali inawaangalia tu

Cdm walishaamka kwenye dunia ya giza boss. Wanapoambiwa kitu hawatii kama mbuzi, lazima wapime na kuujua ukweli ili kujiridhisha.
 
Kwahiyo unataka kusemaje hapo mkuu.

Anasema inatakiwa watu wapende kujisomea ili wawe na uelewa mpana wa mambo. Mtu anayependa kujisomea ni tofauti na wale watu wanaosimama kwenye mikutano ya propaganda mfu, na kuishia kulishwa taarifa za upotoshaji.
 
Chadema wana roho ya kutu.

Sio wana roho ya kutu, bali wameshaamka usingizini, hivyo wanajua matumizi sahihi ya bongo zao. Simply wao ni kizazi cha kuambiwa, na kupima wanachoambiwa, na sio washangiliaji kwa kila wanachoambiwa.
 
Duh! Hata Lesotho wamo mkuu?, Alaf mh Kabudi si alituambia inaitwa United Republic of Tanzania mkuu?

Nitaendelea kusema siku zote Rais Magufuli anaweka historia ambayo itachukua vizazi vingi hadi kuja kufikiwa na viongozi wajao wa taifa hili.

Kwenye mambo kama haya ndio unaweza kupima wenye uelewa mkubwa wa mambo, na wale wanaopewa taarifa bila kuichakata, na kuisifia bila kujiridhisha.
 
Ukiona unakopesheka jua unachakulipa, uwezi pata mkopo mkuu kama hauna kitu, nayo hayo ni maendeleo.

Kama tuna uwezo wa kulipa, hilo deni la taifa mbona linazidi kupaa? Inakuwaje tunaomba kusamehewa madeni badala ya kudhibisha uwezo wetu wa kulipa? Mkuu uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…