Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Wakitupiga za uso wanaitwa majina yote, wakitusifia tunakenua mpaka jino la mwisho.
Btw, hivi kuingia uchumi wa kati (whatever it means) inabidi "watutangazie"? Yaani bila kutangaziwa huingii? Lakini si tulianza kujiita nchi tajiri, sasa hili tangazo "lao" kwa nini litupe raha hivi?

Naona Tangazo tumetoa wenyewe na Kadiri ya taratibu za referencing ingetakiwa aweke link ya mtandao wa WB uliotusifia na aweke Ameusoma muda gani ( accessed)
 
Hivi ukienda kwenye kampeni ukawaeleza watu kuwa nchi yetu imefikia uchumi huo watakulewa wakati hawana maji,umeme,madawa hospitalini,mishahara duni,madeni ya ndani hayalipwi,n.k?


Kwenye kipindi hiki kigumu hivi.
Hakuna biashara, watoto wanarudi shule miili imekuwa mikubwa baadhi ya wazazi hawana hata pesa ya kuwanunulia nguo size zao, madeni kila mahali na huko unasikia uchumi umepanda kwenye makaratasi my foot!!!!!
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150-Fatma Karume on twitter
 
Ukweli uko hivi:

Tanzania imeingia kwenye list ya LOWER MIDDLE INCOME COUNTRY
Na sio MIDDLE INCOME COUNTRY kama wanavyodanganya.


NENO LOWER linaharamisha hizo shamrashamra zao.

Anyway ni mwaka wa uchaguzi lazima wadanganyika wasioelewa wapigwe tu.

Yaani nchi imejaa mazuzu mpaka aibu.

Tungekuwa tumeingia middle Income ingetupasa kuanzia sasa hatuombi tena nje na mara nyingi manunuzi yetu nje ni CASH.

Budget yetu ingepaswa kuwa haina utegemezi 100% na tungekuwa tunalipa madeni sana tunayodaiwa nje.

Ngoja niishie hapa....nivae na barakoa yangu.😷😷😷

Dah! Umemwaga upupu mpaka aibu! Hivyo, huko shule mnajifunza ujinga?
 
Unajua mtaji wa CCM ni waTz ambao hatupendi kusoma. Sijaona uzi mzima watu wakiomba methodology, au classification basis ya hizo takwimu. No wonder hamshangai Zimbabwe ni middle income!!
View attachment 1494836
Nadhani hiyo footnote kutoka kwenye hiyo ripoti inajieleza yenyewe.

Tupende kusoma wanaJF
Kwahiyo unataka kusemaje hapo mkuu.
 
Magu amesha-tweet kwa 'kidhungu' kushukuru!!

Tusubiri magazeti ya kesho na heading watazokuja nazo.

Wakiona watu wanafanya uchambuzi kwa kutumia data mitandaoni,wanatamani wawamalize maana wanaharibu uhundo!!
Hiki ni choo cha walimu wa masasi , ndani ya nchi yenye uchumi wa kati .
2444028_IMG_20200630_091115.jpeg
 
Uchumi wa kati ni kipato cha wastani wa kuanzia dola 1,036 ambayo ni sawa na shs takribani milioni 2,500,000 kwa mwaka.

Mtanzania wa kawaida mnyonge ni kweli anapata kipato kinachofika takribani shilingi 7,000 kwa siku na kwa mwaka shilingi 2,500,000?

Kufika uchumi wa kati unaotangazwa ni kweli ndio hali halisi au makaratasi yanayopelekwa bemki ya dunia yamedanganya?
Patna wako Zitto Ruyagwa Kabwe mbona kimya?
 
Kwahiyo unataka kusemaje hapo mkuu.

Anasema inatakiwa watu wapende kujisomea ili wawe na uelewa mpana wa mambo. Mtu anayependa kujisomea ni tofauti na wale watu wanaosimama kwenye mikutano ya propaganda mfu, na kuishia kulishwa taarifa za upotoshaji.
 
Chadema wana roho ya kutu.

Sio wana roho ya kutu, bali wameshaamka usingizini, hivyo wanajua matumizi sahihi ya bongo zao. Simply wao ni kizazi cha kuambiwa, na kupima wanachoambiwa, na sio washangiliaji kwa kila wanachoambiwa.
 
Duh! Hata Lesotho wamo mkuu?, Alaf mh Kabudi si alituambia inaitwa United Republic of Tanzania mkuu?

Nitaendelea kusema siku zote Rais Magufuli anaweka historia ambayo itachukua vizazi vingi hadi kuja kufikiwa na viongozi wajao wa taifa hili.

Kwenye mambo kama haya ndio unaweza kupima wenye uelewa mkubwa wa mambo, na wale wanaopewa taarifa bila kuichakata, na kuisifia bila kujiridhisha.
 
Ukiona unakopesheka jua unachakulipa, uwezi pata mkopo mkuu kama hauna kitu, nayo hayo ni maendeleo.

Kama tuna uwezo wa kulipa, hilo deni la taifa mbona linazidi kupaa? Inakuwaje tunaomba kusamehewa madeni badala ya kudhibisha uwezo wetu wa kulipa? Mkuu uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Back
Top Bottom