Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Kilaza huwa haelewi Mkuu! Kama umefunguka macho ina maana umeelewa, na anayeelewa hawezi kuwa kilaza! Vilaza ni wale ambao hata baada ya kuwawekea data, wanaishia kutukana!!

Mkuu watu wataacha kutukana wakati wanaamini kila wanachoambiwa na Yesu? Hata hivyo ufafanuzi wako murua umewaamsha wengi, na waimba mapambio unewaumiza vibaya sana. Kimsingi sifa kubwa ya utawala huu ni kuongoza wajinga wengi.
 
Takwimu tu mnashindwa kusoma itakuwa katiba?

Leo utatema hirizi nakuambia. Huku ujue data tu ndio zinakubeba, vyombo vya dola hapa vinawaangalia tu maana matumizi ya nguvu hapa hayawabebi bali facts tu.
 
You can change your earlier thoughts I presume.

Ongea tu kwa kiswahili tu boss, maana Yesu anawaangalia kwenye huu mjadala, ila anaona mnatepeta tu. Au kama vipi ingizeni vyombo vya dola kama game linabana.
 
Sasa BBC ndio source yako unayoiamini? Ina maana wenyewe WB ambao ndio wanatoa hizo data huwaamini? Au ndio kiwango cha darasa la pili?

Fanya hivi, lile kundi lenu la watu wasiojulikana ndio inabidi mlitumie kwenye maswala Mtambuka kama haya. Ww ni dhahiri gari limekata mafuta. Ingizeni lile kundi la nguvu bila akili, hapa mechi ishakuwa ngumu.
 
Aibu ni ya kwako sasa.

Yaani hapa nilipo ni kama nakuona vile. Halafu unaweza kukuta ww ndio wanakutegemea wamekuambia uje ufafanue! Yaani umewaangusha jamaa vibaya sana, maana kama ni samaki, basi wote wamechina. We rudi tu sasa kwenye kikao cha kuiba kura, maana kule ni matumizi ya nguvu zaidi, eneo ambalo mnalimudu vyema. Huku kwenye matumizi ya akili kunasumbua.
 
Aliyeleta link ya BBC ni wewe endelea kujishaua, kuanzia sasa naku-ignore rasmi kwa sababu huna hoja umejaa viroja. Umejaa uongo na uzandiki.

Unamuignore vipi? Umeshapanick tayari. Yaani kama ingekuwa ni kuongea, saa hii ungekuwa umekauka mate mdomoni vibaya.
 
Kuna wakati najiuliza zitto junior nia na dhamira yako ni nini? Hata kama wewe ni mpinzani kisiasa, ni aibu kuwa na mawazo yaliyomo kwenye hoja yako hapo juu (underlined). Una maana gani kama siyo kutusi jamii, au wewe ndiye hupendi kusoma?

Kwa suala la WB kuiorodhesha Tanzania kwenye nchi zenye kiwango cha chini cha Kipato cha Kati, si jambo la kubeza, ila la kila Mtanzania, kutambua fursa zilizopo za kukuza uchumi binfasi na wa Taifa kuelekea Uchumi wa Kati. Kama wewe ni mwanasiasa, basi kuweka Sera na Mikatati ya maendeleo (Kijamii, kisiasa, Kiuchumi na Kiteknolojia) ambazo zitalinda na kuendeleza kiwango hicho cha "Kipato cha Kati", na si kubishana kama ni kweli au
La.

Tabia ya kupinga kila jambo na/au kujadili matukio inawaondoa kwenye masuala ya kitaifa ili Chama kikubaliwe na wananchi. Hivyo nategemea, Mkuu zitto junior na wenye tabia na mawazo kama yako, utatafsiri mafanikio ya Tanzania kupanda kwa Kipato cha Kati kwa vitendo ili kufikia " Middle Income" kama Zimbabwe uliyoifagilia.

Unanilazimisha kusema yasiyohusika na mada kuu, kwamba viongozi unaodhani wana uwezo wa kuipandisha Tanzania kiuchumi ndio hao wenye tuhuma za ufisadi, uzinzi na ulevi wa kupindukia!!!

Hapa nilipo ni kama nakuona vile. Nimecheka vibaya sana hilo hitimisho lako kwenye paragraph yako ya mwisho, umemalizia kuchemsha kwenye hoja nzito kwa siasa nyepesi! Jitahidi usipanic kwenye hoja zinazohitaji matumizi mazuri ya akili.
 
Kitendo cha Nchi ya Tanzania kuingia katika daraja hilo LA nchi zenye Uchumi wa kati,Rais wetu mpendwa Dr Magufuli na watanzania wote wanahitaji kupewa pongezi.

Mbali na pongezi hizo,hapa pana jambo LA mhimu sana kuliko pongezi hizo nalo ni aina ya Rais alietuvusha kufika katika daraja hilo kutofikirika kuongezwa Mda wa Utawala wake ili aendelee kubuni na kusimamia mambo mengine ya mhimu katika ustawi wa nchi na wananchi kwa kigezo cha katiba ! Namaanisha hata baada ya miaka hii mitano tuitarajiayo ya kipindi cha Rais wetu Watanzania tufikirie kumwongezea Rais miaka mingine zaidi ya utawala ili azidi kupata mda wa ziada wa kitekeleza mipango mingine ya kimaendeleo kwa nchi yetu na watu wake! "Kidumu Chama cha Mapinduzi".
Kudos nini? Nyinyi ndio wanga kuletaleta thread za ajabuajabu usiku waway manane. Lalenibana
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============


View attachment 1494690View attachment 1494691
Naona Benki ya Dunia imeeunga juhudi za serikali ya awamu ya 5 kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150-Fatma Karume on twitter
Ndio kabisa, na elimu yetu ni bureee watoto wanafundishwa na walimu wa kutosha wenye ujuzi wa kutosha, wanapata bonge la elimu yaani! tukiugua tunatibiwa hospitali za serikali ambako kuna madawa kibao, ashindwe mgonjwa tu.. mambo ya kuambiwa tukanune dawa pharmacy ni historia.

Biashara zetu zimeshamiri maana mzunguko wa fedha unavutia balaa, kwa vijana waliomaliza vyuo ajira zipo kibao,ni wao tu ku apply yaani. Tatizo la ajira hakuna kabisa.

Umeme , maji bwerere, mabara bara ndio hayo tunaona hadi vijijini yanafika.

Shirika letu la ndege limenogaje yaani! maflights ya kufa mtu, yaani isingekuwa hujuma za mabeberu na wakenya leo hii lingekuwa linaongoza kwa huduma bora Africa mashariki na kati.

Viwanda 800 vipyaaaa bora kabisa vimejengwa ndani ya miaka mitano, yaani atayesema wilayani kwake hakuna kiwanda kipya hata kimoja huyo lazima atakuwa msaliti wa taifa anayetumiwa na mabeberu kuchafua nchi yetu.

Haki mahakamani napatikana bila mizengwe, watu wana uhuru wa kutoa mawazo yao bila kutishwa wala kutumia fake accounts, demokrasia imenyooka kisawasawa vyama vyote vina haki sawa yaani. nknknknknknk

Uchumi wa kati hoyeeee!!!!!!
 
Anasema inatakiwa watu wapende kujisomea ili wawe na uelewa mpana wa mambo. Mtu anayependa kujisomea ni tofauti na wale watu wanaosimama kwenye mikutano ya propaganda mfu, na kuishia kulishwa taarifa za upotoshaji.
Mkuu twende taratibu kwahiyo hii taarifa ni ya upotoshaji.?
 
Back
Top Bottom